Serikali yasistiza wanandoa kumiliki ardhi pamoja kuepuka migogoro ya ardhi

Serikali yasistiza wanandoa kumiliki ardhi pamoja kuepuka migogoro ya ardhi

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
★Wanawake watakiwa kuachana na dhana potofu kuwa ardhi ni mali ya wanaume

Serikali imewasisitiza wanandoa kumiliki ardhi kwa pamoja ili kuepuka na kupunguza migogoro ya umiliki wa ardhi na mirathi isiyo ya lazima ambayo inaweza kujitokeza baada ya mmoja wa wanandoa kufariki.

Akizungumza kwenye Banda la Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Lindi Septemba 16, 2026, wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Madini, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amesema baadhi ya migogoro ya ardhi imekuwa ikijitokeza baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa, hali inayoweza kuhusishwa na namna umiliki wa mali ulivyowekwa.

Mmuya amesema Serikali kupitia sera na sheria za ardhi inatambua haki ya wanawake kumiliki ardhi na ameitaka jamii kuachana na mila na dhana potofu zinazoamini kuwa mwanamke hawezi kumiliki ardhi.

Amesema umiliki wa pamoja kati ya mke na mume ni miongoni mwa hatua zinazoweza kuweka msingi wa usalama wa umiliki wa ardhi ndani ya familia na kusaidia kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika mazingira ya mirathi.

Kwa upande wake, Afisa Ardhi, Bi. Anastazia Mahalu, amewataka wanawake kuchangamka na kutumia fursa zinazotolewa na Serikali katika kupata haki ya kumiliki ardhi, akisisitiza kuwa kutokufahamu haki zao kunawafanya baadhi yao kubaki nyuma katika masuala ya umiliki wa ardhi.

Bi. Anastazia amesema Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Toleo la mwaka 2023, inatambua haki sawa kwa wanawake na wanaume katika kumiliki ardhi, hivyo wanawake wanapaswa kuondokana na mtazamo wa kusubiri na badala yake kuchukua hatua kuhakikisha wanapata haki yao ya umiliki.
 
Ni sahihi.

Indirect unapowaambia wanawake wamiliki Ardhi au Mali unawapa wajibu wa kuzitafuta hizo mali kwa kufanya kazi za uzalishaji. Kama ambavyo tumeona wengine wakiwa madaktari, wauguzi, waalimu, fundi nguo na kazi zingine.

Sio kukaa nyumbani na kutegemea mwanaume afanye kazi, atafute mali then wanawake watake haki ya kumiliki mali wakati kazi hawataki, wamekaa nyumbani.

Ukifanya kazi automatically utamiliki Mali. Na migogoro itapungua kwa kiasi kikubwa.
Migogoro mingi ipo pale ambapo mmojawapo sio mzalishaji alafu anataka haki sawa na aliyezalisha. Huo ni uhuni.

Kuna swali la muhimu, mwanamke anazaa na kulea watoto. Je atawezaje kushika majukumu yote?
Hilo swali ni muhimu lakini sio kigingi cha kumnyima mwanamke nafasi ya kufanya kazi.

Wapo wanawake wanafanya kazi za uzalishaji na wana watoto wengi tuu.
 
Back
Top Bottom