Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Mimtu mingine kulalamika tu hata kwa yale yasiyolalamikiwa! Kama ingekuwa rahisi hivyo huu ugonjwa usingeingia marekani na mataifa mengine yaliyo na technolojia na uchumi mkubwa!
 
Kwa ufupi ni kuwa sasa utasambaa zaidi kuliko ilivyokua mwanzo maana wa mjini wanawapelekea wa vijijini!!
 
Mimi sijaelewa au nashindwa kutofautisha kati ya kusitisha masomo vyuoni na kufunga vyuo unaweza ukasitisha masomo na wanafunzi wakabaki chuoni bila kuingia madarasani lakini pia ukifunga chuo hakuna masomo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafunzi wa boarding schools wangebaki huko huko maana hawa hawachangamani na watu wengi kutoka nje ya shule zaidi ya walimu wao hasa hawa form six ambao wamekarbia kumaliza wangebaki hdi watakapo maliza mitihani yao...
 
Nyinyi ni aina ya walalamikaji tu kwani jambo likifanywa huwa wa kwanza kulalamika na lisipofanywa hulalamika pia. Hatuna muda nanyi endeleeni tu wakati wenzenu wanapambana usiku na mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…