Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Shukuru hata kwa hatua ambayo serekali inachukua sasa...unalalamika utadhani mwanamke aliyetelekezwa....!!!?
 
Hapa serikali imezingua kwa namna moja ama nyingine

Huu ugonjwa naamini ni wa kawaida sana tofauti na unavyotangazwa

Sasa serikali imeshindwa kuvuta vuta muda kidogo ndo watangaze masuala ya kufunga vyuo na shule za msingi na sekondari!?

Binafsi nimekua nikipiga hela kupitia hii sekta ya elimu sasa kitendo cha serikali kutangaza zifungwe kwa mwezi mmoja ni kuninyang'anya tonge mdomoni

Serikali mmechukua maamuzi ya haraka mno kufunga hizi taasisi za elimu

Kama Leo tu nimekosa dili la kuingiza laki 2 kisa Corona

Mjue hali ya uchumi itayumba sana miongoni mwetu kwa hofu yenu ya Corona.

Naishauri serikali itengue hili tangazo la kufunga shule na vyuo Mishe Mishe ziendelee .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yap!
Carantin ingewekwa vyuoni na mashule ya bweni!

Day schools postponed, prayers gathering prohibited, sports event paused and daladala trans. Restricted! Mwendokasi abandoned.
Atawalisha nani uko karantini
 
Vipi mkuu ulikuwa una maanisha nini?
Au unawezakuta wamebeba vimelea?[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Sigara Kali utakuwa umetumia hiyo sigara kabla ya kuanzisha huu uzi...

Unafikiri serikali haikuwaza athari za kiuchumi??

Hao wanafunzi na wanachuo wakiwa na uhai utatengeneza pesa haina shida ila wakiwa wafu, hakuna wa kufanya naye biashara...

Wengi sana tumeathirika, lakini katika hili, ngoja tukubaliane na maporomoko kidogo ya kiuchumi kwa uhai wa wananchi.

Everyday is Saturday.................... 😎
 
Umeshindwa kueleza ni kivipi serikali imekuathiri,au ni namna gani ulinufaika na hao wanafunzi ,umeishia kulialia,wakati wewe unalia bodaboda na wamiliki wa magari wanashangiri,hapa ndo naamini kuwepo wa nguvu ya asili ambayo husawazisha mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…