On point.Nyie watu mna vituko sana! Kwamba kwa miaka 40 hatungekuwa na mapato yahusuyo bandari, unazungumzia mapato yapi hasa? Hivi umeshawahi kujiuliza hiyo bandari ingekuwa na uwezo wa kuhudumia mzigo kiasi gani na kodi ingekusanywa kwa kiasi gani? Au ndo unataka kusema na hiyo kodi ingechukuliwa na Wachina?
Halafu kwanini unasema bandari ya Dar es salaam ingesimama na kuhoji ikijengwa Bandari ya Bagamoyo halafu ya Dar ipelekwe wapi!!! Are you serious?! Yaani ndo ushaona tutakuwa ni mibandari mikubwa mikubwa mingi?! Kenya tu hapo, wana mradi mkubwa sana kama ule wa Bagamoyo ambapo wao wanataka kujenga bandari nyingine kubwa zaidi kule Lamu! Kwahiyo unataka kusema bandari ya Mombasa wataipeleka wapi? Hivi we unadhani kuna banadari hapa zaidi tu kwavile kuna umasikini wa kutisha kwahiyo ukifanya massive imports utakosa walaji na kile cha ku-export hatuna.... halafu unadhani bandari ya Dar es salaam inatosha sana! Hivi uliwahi kuona ile picha ya Wachina wakipanga foleni kabla store haijafunguliwa wakisubiria kununua iPhone 6!! Hivi tuwe na angalau 20% ya uchumi wa China bado unaamini bandari ya Dar inatosha sana na kuongeza nyingine "sasa hii tutaipeleka wapi?!" South Afrika hapo, ni kwavile tu na sisi ni masikini wa kutisha lakini uchumi wao ni kawaida sana tena ukikishikiwa na watu wa jamii moja! Population yake wala hawajatuacha sana lakini bado wana bandari 5+!
Kwamba baada ya miaka 40 eti bandari itakuwa imeshachakaa; hivi umeshapata kujiuliza hii bandari ya Dar es salaam ambayo leo tunaitegemea ina miaka mingapi?
FYI, hii habari kama ni kweli basi hili litakuwa kosa kubwa sana kwa serikali ya JPM na watani zetu Wakenya wakisikia hii kitu watafurahi sana na sitagombana tena na Wakenya wakituita Watanzania ni mabogasi manake huwa nakwaruzana nao mara nyingi sana lakini tukiuacha mradi wa Bagamoyo, basi ni kweli tuna kila sifa za kuitwa mabogasi! Hii habari akiipata Bepari Uhuru Kenyatta lazima afungue Champagne asubuhi asubuhi!
Kama kuna terms zisizofaa jibu ni kukaa mezani na sio ku-abandon the whole project! Nimeshasema na hapa nitasema tena-- Dar es salaam haina eneo la kuweza ku-handle bandari yenye uwezo wa ku-handle idadi kubwa ya makontena for the next 50 years. Kule Mtwara kutakuwa bize sana na mimeli ya mafuta.
Sifa zikizidi mgema hutia maji,ndio hii sasa!yani Kenya walikuwa wanasali usiku na mchana hoi project ikwame!kukwamisha genetation defining project Kama hii ni uhaini grade one!bandari za aina ya bagamoyo hazijengwi hovyo.na hata zilijengwa,hazijengwi karibu karibu.sasa ikitokea wakenya wakawaconvince wachina wahamishie hii kitu kwao.sie tutabaki na kijibandari cha kichuuzi cha dar ambacho hata kwa mombasa hakifuo dafu.halafu tunataka kushindana,how?
Magufuli will ruin our economy akiendelea hivi.mark my words.dunia ya sasa sio lazima ushinde kila argument, sio lazima utunishie msuli kila MTU/taifa,sio lazima usifiwe kila kona.moderation is important.yataja kutukuta ya Mugabe.tuna raisi anayetutetea na yukp right lakini we keep making suicidal decisions in the name of being correct .