Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
On point.
Sifa zikizidi mgema hutia maji,ndio hii sasa!yani Kenya walikuwa wanasali usiku na mchana hoi project ikwame!kukwamisha genetation defining project Kama hii ni uhaini grade one!bandari za aina ya bagamoyo hazijengwi hovyo.na hata zilijengwa,hazijengwi karibu karibu.sasa ikitokea wakenya wakawaconvince wachina wahamishie hii kitu kwao.sie tutabaki na kijibandari cha kichuuzi cha dar ambacho hata kwa mombasa hakifuo dafu.halafu tunataka kushindana,how?

Magufuli will ruin our economy akiendelea hivi.mark my words.dunia ya sasa sio lazima ushinde kila argument, sio lazima utunishie msuli kila MTU/taifa,sio lazima usifiwe kila kona.moderation is important.yataja kutukuta ya Mugabe.tuna raisi anayetutetea na yukp right lakini we keep making suicidal decisions in the name of being correct .
 

Cant they kill two birds with one stone?
 
Ni lazima ukose la kujibu kwa sababu umeuona ukweli. Sikushangai.

kifupi kuna project mbili zilipelekwa bagamoyo kwa sababu tuu ya ubunafsi wa wa tu fulani ya kwanza walilazimisha ikabuma ilikuwa ni ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa bagamoyo na ndio sababu hata project ya JNIA termanl 3 ilichelewa sana sasa na hili la bandari kutolewa ndo limepigilia nyundo ya mwisho.

kilichobaki bagamoyo na kujenga mahotel kuboresha utalii pamoja bagamoyo ubaki kuwa mji wa utalii na kulima mananasi ila sio walicho taka kukufanya
 
Walipe gharama waliosaini hiyo mikataba bandari hiyo ilikuwa na lengo jingine afadhari serikali iliyopita ilikuwa haina hata chembe ya huruma kwa mali za umma. Wengine wakusanye wengine watumie iwe mwisho serikali za aina hii
 


Mkuu paso sijui kwanini uamuzi wa kusitisha Bandari ya Bagamoyo umeniuma sana tena sana.

Kama nitakuwa mbali na ukweli tafadhali nisahihishwe Bandari ya Bagamoyo fedha zake hazitatoka hazina yetu bali wawekezaji kama sikosei China ambayo ingegharimu 10 bilion u$ zingeingizwa na wawekezaji.Najua kungekuwa na muda mrefu labda 50 years ya kumilikiwa na wawekezaji yamkini mimi na wewe including Kikwete hatutakuwepo lakini watoto na wajukuu wetu wangekuja kufaidi matunda ya maamuzi ya serekali ya awamu ya nne.

Bandari ya Bagamoyo ingetoa majawabu yote ya ushindani na bandari ya Mombasa.Majirani zetu Kenya walikuwa wakiogopa sana ujio wa Bandari ya Bagamoyo ambao ungefungua fursa nyingi za kiuchumi.Uwekezaji wa aina hii unagombewa dunia nzima nashangaa sana mtu mmoja waziri Prof Mbarawa ana uwezo kuondsha mradi mkubwa kiasi hichi na waTanzania wakamchekea kisa eti Bagamoyo nyumbani kwa Vasco watu wanasahau Bagamoyo ipo Tanzania si Uganda au Rwanda.

Sababu za kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo lazima ziwekwe wazi masuala ya kijinga jinga hayana nafasi karne ya 21.Sasa naanza kuamini Dr Magufuli atashindwa mapema iwapo atakuwa anafanya maamuzi ya aina hii.Kama mkataba ulikuwa na kasoro nadhani serekali ingekaa chini na wadau wote na kurekebisha kasoro hizo.Kama Bagamoyo panaonekana si sehemu nzuri basi wengetafuta eneo jingine lakini si kuufyeka mradi.Siku zote Tanzania itabaki nyuma linapokuja suala la ushindani kwakuwa viongozi wetu wengi wanaonekana hawajali sana usatawi wa Tanzania zaidi ya kuwekeana vinyongo.
 

Badala ya kukimbia kujenga bandali mpya bagamoyo wakati kina cha bagamoyo ni kifupi na meli kubwa ni ngumu kuingia ilipaswa bandali ikajengwe mtwara ndiko haswa kuliko pendekezwa toka wali na pia ni rahisi sana kuhudumia mizigo kutokea kule kwenda DRC na zambia pamoja na malawi lengo lilikuwa kupunguza msongamano dsm ila jamaa aliamua kupelekwa ule mladi kwao makusudi kabisa najua intime hiyo project itatekelezwa ila sio kwa sasa coz watu wanalazimisha
 
Mkwele ni jipu la hatari sana,hata utumbuaji wake Dr.inabidi awe na tahadhari usaha usiingie machoni.Kila pahali ukigusa,jipu.Achunguzwe pamoja na familia yake,watakuwa wamechukua % nyingi ya miradi ya hovyo kama hii ya bandari ya Bagamoyo na ile mikataba ya Gesi.
 
Usikute hii ingekuwa kama iptl inalipwa Pesa izalishe umeme au isizalishe.


Hahahahahahahaa vere fantastic

Hiyo nchi haina majipu ina kansa kuna sehemu zinatakiwa zikatwe
 
Kujengwa banadari mpya na ya kisasa kupisha bandari ya dar ambayo haina nafasi ni uharibifu?

Hakika shule mlienda kusomea ujinga.
Kuna ujinga na ujinga.
Ujinga zaidi ni kuacha kukarabati reli ya kati inayotuunganisha na nchi 4, ukaacha kukarabati /kupanua bandari ya Dar ambayo kwake zinanaanza reli mbili na kutuunga na nchi 5, ukaacha upanuzi wa Mtwara itakayotegemewa kwa export ya chuma na mkaa wa kusini, na badala yake ukakimbilia kuanza kukopa kwa ajiri ya bagamoyo.
 


kama hela zinatoka china kama unavyo dai sasa kwanini Tanzania wasitishe ujenzi huo na badala yake hela ziende kuboresha bandari zilizopo mie sipingi sana swala la kujenda hiyo bandari bagamoyo lakini je kina cha bahari upande wa bagamoyo kinatosha au ndo tena kazi ya kuchimbw inaanza.
kwanini wasijenge mtwara kama mapendekezo ya mwanzo yalivyo tolewa? y bagamoyo
 
Mawazo yako ni mazuri na ndy lengo la serikali lkn huna kitu unamadeni unaanza kukidisha kila kitu kwa wenzio utaibuka lini. Imesimamishwa kupisha uimalishaji wa miundo mbinu kwanza hakuna reli yaani unawaza kuwa na benzi hata baiskeli huna. UTUMWA WA MAWAZO
 
Kimweri,

Kuhusu possibility ya Magufuli kuja ku-ruin uchumi wetu endapo ataendelea hivi nakubaliana na wewe na kuna mtu nilishawahi kumwambia all you need to agree with everything kwa haya yanayoendelea ni your preferred management style. Kama management style yako ni ile ya kuhakikisha mtu yupo kwenye kiti chake ofisini na hata akienda kunywa maji anaenda kwa kukimbia basi lazima leo hii aone Magufuli anatupeleka nchi ya Ahadi!

Yaani kabisa kuna wengine wanasema eti bandari zote hizo za nini huku akisahau kwamba moja ya sababu ya kwanini Dar inapokea mzigo mdogo kuliko Mombasa ni kwa sababu hata hao walaji na wauzaji wa ku-attract mzigo mkubwa Dar es salaam hawapo!! Yaani watu hawafahamu kwamba ni umasikini wetu ndio unaofanya bandari ya Dar es salaam ionekane inatosha!
 
Mikataba iliyoingiwa ikoje....???
Mkataba haukuwa umesainiwa ila ulikuwa katika stage ya mwisho ya negotiations, wachina washenzi sana wale yani wao wajenge mashed sisi tufanye dredging sasa hapo uwiano ni upi wakati wao walipaswa wafanye dredging sisi tujenge majengo na Berth tu ukizingatia ya kwamba wao ndio walikuwa na shares kubwa kuliko serikali yetu.
 
Dunia binadamu na Wanadamu.....................................................Mungu tu anajua zina kitu gani??????????????????????CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA Sijui imeroga vijana,sijui ni viroba??????????????????
 
watu tulisema m.kwere iw yake ilikuwa ni level ya udiwani..yeye alichojua ni kupiga dili za pesa tu,hakuwahi kuwapenda watanzania
Kwahiyo maada yako ndiyo inatufundisha nini au unataka kueleza nini.
 
Kuna Mtu anaongelea mambo ya 3G na 4G ambazo bandari za wenzetu zinalenga kuanzisha na hivyo kama nimemuelewa vizuri anasema tutashindwa kuingia katika ushindani na bandari za wenzetu. Swali langu ni Je, bandari za Dar, Tanga na Mtwara haziwezi kuboreshwa na kuingizwa hiyo mifumo ya 3G na 4G? (kama ni mifumo/technolojia anyway). Au hili lingewezekana tu kwa kujenga bandari ya Bagamoyo. Ni maoni yangu kuwa serikali imefanya tathimini ya kutosha juu ya hasara na faida za ujenzi wa bandari mpya kwa sasa kabla ya kufikia hatua iliyochukuliwa ya kusitisha ujenzi huo. Hivyo binafsi napongeza uamuzi uliochukuliwa na serikali wa kusitisha mradi huo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…