Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Nilishangaa sana niliposikia inajengwa bandari nyingine Huko Msoga nikasema hivi viongozi wetu wanafikiria kweli vizuri, kwanza ukiangalia Bagamoyo na Dar ni pua na mdomo, pili Ukiangalia foleni za dar halafu ijengwe tena bandari nyingine ambayo inategemea barabara zile zile, binafsi niliwaza na kushauri kwa nn wasiboreshe bandari ya dar, tanga na mtwara coz ya mtwara ingeboreshwa kwa ajiri ya kuhudumia nchi za kusini mwa Afrika, halafu hii ya dar ibaki inahudumia nchi kama za Congo, Rwanda na Burundi.
 

Yap mkuu umejaribu kutokuwa mshabiki kama wengine humu,, hili suala watu wanarijadili kiushabiki sana mkuu..
tumeshaambiwa inaweza kuwa one of the big port in Africa, bila shaka mapato yake yangeweza kabisa kuzijenga Tanga na Mtwara kwa takribani kipindi cha miaka 20... Hii sio project yakuacha iende hivi hivi labda kama tuna solution inayofanana na hii project. Dar sio mji tena wakuutegemea kwa project yoyote kubwa baadala yake lazima tuwe na backup plan ya karibu na mji wa dar, bagamoyo port ingeamsha mji wa pwani, moro na tanga na kuunganisha dar,pwani,moro na tanga kimaendeleo, maana naona pia bandari ya tanga kutumika kama backup plan ya bandari ya bagamoyo kukiwa na congestation ya meli maana dar haitaweza tena, mtwara port itajijenga yenyewe maana tayari njia imeshaanza kufunguka kwenye oil na gas, lazima mapato yatapafikana tu maana hata makampuni ya mafuta na gas hayawezi kukubali kuteseka yatatujengea tu hii mtwara port kwa makubaliano fulani..
 
Wacha jipu litumbuliwe,huyu jamaa na mikataba yake feki ya kichina inabidi akalale lupango ili kurudisha heshima ya hii nchi
 
Ngoja niwaite rafiki zangu Nguruvi3 Pasco JokaKuu Kichuguu naomba maoni yenu.
Eric, kwa hili kuna mengi sana ya kujifunza.

Moja, kama Taifa hatuna dira. Mtu mmoja anaweza kuamka na dira yake na ikawa ya Taifa. Dira ya JK imefeli tunasubiri ingine ifeli kwasababu zote zinaongozwa na dira ile ile iliyoshindwa miaka mingi

Pili. inaeleza tusivyoweza kusimama na kupanga mipango yetu kwa kutumia wataalam na utaalam bali wanasiasa

Tatu, inatukumbusha hakuna kilichobadilika, CCM ni ile ile. Hawa akina Magufuli, Mbarawa n.k. walikuwemo katika cabinet.
Hakuna hata mmoja aliyeoonyesha kutoridhishwa na madudu. Leo awanatuaminisha wana maono zaidi. T

Nne, tuliandika sana hapa JF na kuishauri serikali kuimarisha bandari zilizopo kwanza. Tulisema ile ya Tanga ina infrastructure nzuri kwanini haiiimarishwi sambamba na ya Mtwara?

Kwanini hatuimarishi ya Dar ikafanya kazi at capacity? Tulichoona miaka 10 uongozi uliachia watu wagawana magati.
Uongozi uliwaacha wahuni waliosaidia kampeni kuendesha bandari. Wao walikuwa angani

Tano, uamuzi wa kujenga bandari ya Bagamoyo ilikuwa knee jerk reaction baada ya CoW kujenga ya Malindi.
Tofauti na Kenya wenye dira, sisi tulikuwa na wapiga soga na bla bla, ujanja ujanja wa kariakoo, maneno maneno tuu n.k.

Wakasema wamepata pesa n.k. leo tunagundua ulikuwa ni udanganyifu tu

Sita, inaonekana kuliwa hakuna pesa, sasa mradi ulipangwaje kukiwa hakuna resource? Tunarudi pale pale bla bla, projo porojo

Saba. huu mradi ulipelekwa Bagamoyo kwasababu za kisiasa tu. Ni kama ule wa chuo cha IFM Msata.
Yote hayo nikukosekana kwa vision, tukaishi kwa hadithi na maneno neno porojo porojo na uzururaji ilimradi siku zinakwenda

Hawa wanaokataa mradi wa Bagamoyo ni CCM ile ile walioshindwa kusema hapana.

Ndio maana tunasema felia ipo pale pale tunabadilisha bega.

Hakuna sababu zilizoelezwa na kwamba nini kitafanyika tofauti kukabiliana na changamoto zilizopo bandari ya Dar.
Ni maamuzi yale yale yalifeli na sasa tunasubiri felia nyingine. Hakuna vision kwanini tusifeli? Felia ipo pale pale
 



Tatizo kubwa la sisi Waafrika ni kwamba hatuna akili na ndiyo maana ni ngumu sana kuendelea ingawaje tuna kila kitu!
Nchi yenye uchumi mdogo kama Tanzania hahitaji Bandari kubwa kama hiyo ya Bagamoyo sijui ya kuchukuwa mega ships hizo, hiyo Bandari ya Bagamoyo mnaing'ang'ania ili isafirishe nini?

Ngoja nikusaidie kidogo nchi yetu inamport na export bidhaa za thamani ya dola kama bilioni 16 (Na hapa ni jumuisho ya kila tunachoingiza na kutoa na kuna bidhaa nyingi hazisafirishwi kwa meli nyingine br. nyingine ndege hivyo Bandari peke yake ni chini ya hapo )na hii ni pamoja bidhaa zote za nchi zinazotumia Bandari yetu sasa uchumi kama huu wa dola bilioni 16 ni wa kujengea Bandari ya dola bilioni 10 kweli? hiyo ni economics ya wapi? Halafu hizo mega ships zitasafirisha nini?
Unaafifikri wamiliki wa Mega ships wataleta meli zao kwenye nchi inayosafirisha bidhaa za Dola bilioni 10?

Wachumi wote wa Dunia wanasema kwamba sababu kubwa ya nchi zetu za kiafrika kutokuendelea ni kwamba nchi wanafanya projects ambazo hazimake economic sense yaani wanatumia fedha nyingi sana kwenye white elephants projects kama hii la Bandari ya B'moyo badala ya kuwekeza fedha hizi kwenye mambo ambayo yangeweza kuzinufaisha nchi kwa haraka, kwa mfano kama ukichukuwa hizo bilioini 10 ukazigawa bilioni 2 ikaenda Tanga, Bilioni 2 ikaenda Mtwara, bilioni 3 ikaenda kwenye reli na barabara, biloni tatu zilizobaki zikaenda kujenga bandari ya Ziwa Tanganyika ambapo itahudumia Burundi, Kongo na Zambia na zingine zikapelekwa Ziwa Viktoria zikawekezwa kwenye bandari pia huoni kwamba kutaifungua nchi kwa kiasi kikubwa sana klk kuzitumia biloni 10 kwenye Bandari mpya ambayo wala kwanza haipo, na nchi wala haina uwezo wa kuitumia kwa maana ni kubwa sana ukilinganisha na Uchumi wetu?
 
bila kuwa na uhakika wa sababu za kusimamisha ujenzi huu ni vigumu kuchangia. Serikali isifanye kazi kwa kusikiliza makelele ya siasa kama wachezaji wanaocheza kwa kusikiliza kelele za mashabiki.

wazo la kujenga bandari ya bagamoyo ambayo ni ya kwanza kwa afrika ikijengwa na wachina ni best proposal kwa Tanzania kwa maana kwa kuangalia jinsi wachina walivyotapakaa afrika nzima ingekuwa ni business opportunity ya kuifanya dar ikue sana kibiashara, ingekuwa rahisi wachina hawa kuvuta mizigo katika nchi nyingi za afrika magaribi, kati na kusini kupita bandari ya bagamoyo.

kwa mtizamo wa juu juu nadhani kulikuwa na uwezekano wa kukuza biashara katika nchi yetu na nchi nyingi za afrika na nje ya afrika na tungepata mapato mengi yasiyo ya moja kwa moja kutoka katika bandari.

baada ya hapo tuangalie katika business wanayofanya wachina sisi tunge pata nini kutoka bandarini moja kwa moja kwa kuangalia, kodi, au kama tuna asilimia katika mapato ya bandari, tuangalie kutengeneza ajira.

haya yote tulinganishe na kukumbatia bandari tulizonazo ambazo ni bandari holela kama yalivyo makazi yetu holela, hazina maeneo ya kutosha, hazina vitendea kazi, hazina wataalamu waliokaa kibiashara bali watu wa dili na mengine.
 
Twende Mtwara kuna bandari yenye kina kirefu ni namna tu ya kuimarisha si lazima ujenge mpya wakati tunayo ya kuboresha na gharama zake haziwezi kuwa kama kujenga upya kwa mkataba wa namna ile lazima tujionee huruma na tuonew huruma vizazi vyetu vijavyo dhidi ya mzigo wa madeni ambayo yanaepukika.
 
Ni kweli haukuwa na mantiki yoyote. Lakini mmeshasaini mtaweza kuwalipa hao wawekezaji fidia ya kuvunja mkataba?
ni kweli mkuu watu wana mikakati ndo maana jamaa aliandaa kabisa na kampuni yake ili bandari ikijengwa Msoga basi Home wawe wanapakua na kutoa mizigo yao bila kulipa kodi, ndio maana Mzee wa msoga alifanya kila linalo wezekana Mdogo wake apate uraisi lakini Mungu naye mkubwa akaharamisha mipango ya wezi.
 


Ninachotaka kukisema ni kwamba Katiba haimmzuii Raisi kuwa mbaya na mwizi na ushahidi uko wazi, bali kinachotofautisha nchi moja na nyingine ni Utamaduni wa jamii husika na kamwe siyo Katiba, kama Raisi akitaka kutumia madaraka yake vibaya atayatumia tu hata kama Katiba hairuhusu atakachokifanya ni kupeleka mswada Bungeni kubadilsha kipengele ambacho hakitaki Wabunge wa Chama chake wanapitisha na anafanya anayotaka kuyafanya!

Hivi sasa Uhuru Kenyata ameshabadilisha mambo mengi tu ambayo yalikatazwa kwenye Katiba original kwa kutumia hilo hilo Bunge lao hata Kagame amebadilisha Katiba na huwezi kumlaumu kwa maana watu wamepiga kura ya maoni zaidi ya 90% wamependa abadilishe Katiba na hilo likafanyika hivyo Katiba siyo suluhisho bali ni Jamii yenyewe na utamaduni wake, kwa mfano sisi kwetu ni nini kilimzuia Kikwete kama kweli angeamua kubakia kuwa raisi mpaka leo hii?

Lakini hajafanya hivyo ni kwanini? Siyo kwa sababu ya katiba tu bali ni Utamaduni wetu hasa wa CCM waliojiwekea hivyo automatic unajiona haupaswi kuukiuka, Katiba haiendelezi nchi hata siku Moja asikudanganye mtu!
 
Mkuu ukijenga bandari bagamoyo bado kutakuwa na mlundikano wa watu katika mikoa hii miwili ambayo kiuhalisia ishajaa, tuijenge kusini na mikoa ya pembeni ili nchi ipanukee
Yaani ningekuwa mods, ningesema the mada is closed. Jibu lako ni tosha kabisa. Watu lazima wajue dar na bagamoyo si zaidi ya miaka kumi itakuwa imeungana, hivyo msongamano utakuwa pale pale. Nchi itanuliwe kwa kujenga bandari mbali kabisa na dar, na hilo litapunguza watu kuhamia dar kwa kasi kama ilivyo sasa.
 
Wengine tulijiuliza huyu Rais wetu ni mikataba gani 17aliyoingia kwa siku moja?

Ni vyema sasa mikataba yote iwekwe wazi na iwe inajadiliwa bungeni.
 
Hii nchi tutasubiri sana, ni chi ambayo haina dira, kila raisi ana dira zake za miaka 10, 10 au 5, mradi kama huu nlifikiri ulipewa baraka kubwa na baraza la mawaziri wote waliopita, ok tusirudi nyuma, lakini hapa inaonyesha ni jinsi gani kila kiongozi anaamuka na kufanya analojisikia. Kuna vitu nadhani hasa vya maendeleo viwe either tuna debate bungeni, kwenye vyombo ya habari, mitandaoni au njia yeyote itumike kuhalalisha sera na dira za maendeleo ya Tanzania. Haiwezekani unaamuka na kufuta project ya bandari ya 10B usd ambayo ingeli serve the whole africa , hivyo kuiongezea mapato na ajira kwa vija bila sababu. Kwani uwezo wa kupanua bandari ya zingine upo na wakati ujenzi wa bandari hii ukiendelea.
 
Ikiwa uyasemayo ni kweli,kwanini sasa watake kuimiliki bandari kwa muda huo tajwa?wanapata nini hapo bandarini in return?
Nilichosema ndo kweli yenyewe kwani wewe hukufahamu kwamba bandari iwe ya Mchina au Mwarabu lakini kodi iko pale pale basing na mzigo unaopita? Labda jambo moja ckusema-- China, wanataka independent port badala ya sehemu kama Dar coz' lengo lao ni ku-establish langu lao la kibiashara kati ya China na East & Central Africa! Kama ujuavyo, China ndo largest exporter to Africa... sasa walichotaka wao ni kutumia bandari ya Bagamoyo kwa ajili ya kusambazia bidhaa zao East & Central Africa na vile vile wana similar project Djibouti kwa ajili ya nchi za horn of Africa!! Sasa kwa mtu anayetaka kuushika u kanda mzima huwezi kumpeleka Bandari ya Dar yenye uhaba wa maeneo ya kuweza ku-handle millions of containers.

Tukija wao watapata nini; cjasema hawatapata kitu bali nilichosema TRA itaongeza mapato maradufu kutokana na kuongezeka kwa mzigo maradufu! Aidha nimesema mapato watakayoingiza TRA ni makubwa zaidi kuliko watakayoingiza Wachina!

Why 40 years?! Hii ni grand project.... $10 Billion sio pesa ndogo kui-refund na wala tusione ajabu! Fuatilia contracts za NHC na private real estate developer uone ni mikataba ya miaka mingapi wakati ile ni mikataba of just some billions Tanzania Shillings... wewe unashangaa mradi wa trillion 20 kuendeshwa for 40 years wakati hata sheria yenu ya kumiliki ardhi tu ni miaka 99 na wala hakuna serikali inachopata cha maana ingawaje nackia hivi sasa ni miaka 33!!! Sasa nyinyi mnaona hatari kwenye active project worth $10 billion kuwa operated kwa miaka 40 huku mkiendelea kukamua kodi kama kawaida?!

Lakini vilevile ikiwa shida ni hiyo miaka 40; solution ni kurudi kwenye negotiation table co kuachana na mradi....

Hapa narudia tena, kama hizi taarifa ni kweli basi Kenya lazima wachangamkie hii fursa na yale mashindano yetu na Kenya yatakuwa yamekufa rasmi na kutuacha na uboya wetu huku wenyewe tukifurahia! I bet atachofanya Mchina ni kitu kimoja tu... kuboresha TAZARA kisha anatuacha na uzuzu wetu!
 


Big Port Afrika itasafirisha bidhaa gani? hakuna Uchumi Tanzania wala nchi zinazotuzunguka za kuweza kuitumia Bandari kama hiyo, hiyo ingekuwa ni white elephant project!
 
Asante ndugu yangu kuzidi kuwafafanulia. Haiingii akilini kwa ghafla tuache kupata mapato ya bandari ili tusubiri miaka hamsini ya mapato tusiyokua na uhakika nayo. Mchina wa leo si yule wa enzi ya Nyerere. Anajua Sifa kubwa ya Tanzania yetu ni shamba la bibi. Masharti ya kwanza atakayoweka ni kwamba kwa miaka 40 hiyo meli zote lazima ziweke nanga bagamoyo. Hivyo bandari ya dar ingekufa kifo cha mende. Kwa kweli sijui kwa nini imekua shida kwetu kuona hilo. Kuna mtu katoa mfano mzuri sana hapa wa migodi ya dhahabu. Awali Mwalimu alikataa yasichimbwe kwa hoja watanzania hawatafaidika nayo. Sasa kuna migodi imemaliza madini na imefungwa hali wananchi wa maeneo hayo bado wako hoi. Kwa hili nampongeza sana Mhe Magufuli ila aende polepole na la walala hoi wa mabondeni. Kwa maana awaondoe lakini yeye kama baba wa Watanzania awasaidie wapate makazi hata kama ya muda.
 



Hata wewe tatizo la uelewa pia! Unawezaje kujenga Bandari TanZania ikahudumia Afrika nzima? Kivipi unaweza kuniambia? Kwa taarifa yako tu wateja wanaotumia hata Bandari ya Mombasa Kenya huwezi kuwaleta kutumia Bandari yetu ni ngumu sana na hai make economic sense kwao kijiografia sasa iweje Bandari ijengwe Bagamoyo ihudumua Afrika nzima? Unawezaje kumfanya Muethiopia au Msufdani aje kutumia Bandari ya Bagamoyo badala ya Mombasa unaweza kuniambia hilo?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…