Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Hawa walisitisha huu mradi wafunguke zaidi walichokuta huko ndani ni kitu gani?
Hadi kufikia uamuzi huu?
Hujasikia mzee wa msoga alikua ikulu jana? Ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe.. Cha muhimu huo upuuzi imepigwa chini
 
Hawa walisitisha huu mradi wafunguke zaidi walichokuta huko ndani ni kitu gani?
Hadi kufikia uamuzi huu?
Ni waarabu wa Oman, baada ya kuona wanatukwana na CCM Zanzibar na kina Lukuvi eti wanataka kuitawala Zanzibar, wameamuwa kujitowa kusaidia mradi huu!
 
H................
Na hili la kuachiana madaraka kwa kweli kama si Mwalimu ambaye akiwa hai alilisimamia sana sijui kama hata hapa kwetu waongeza muda wasingekuwepo. Hapa hoja ya msingi ni kuwa na Jamii inayoweza kuwalazimisha watawala kutii Katiba. Tatizo Afrika ni rahisi watu kuwagawa Kidini, kikabila, kiukoo na mwisho wa siku anayevunja Katiba hujifanya kulinda Kabila, dini, Ukoo, chama, au jinsia yake dhidi ya wale wanaomhimiza kulinda Katiba!

Ningependa nikubaliane na wewe 100%. Ukiona jinsi wanasiasa wetu wanavyosaka nafasi za uongozi na hata kutishiana kuuana kweli kama tusingekuwa tumewekewa msingi ule wa zege - wa kupishana, kungatuka alioweka Nyerere TANZANIA tusingekuwa tofauti na nchi nyingine. Tena hatuna budi kushukuru vyombo vyetu vya habari kwa kutafuta hotuba zile kali za Nyerere zenye kukemea uovu wa kung'angania madaraka na hasa ile inayoisemea Ikulu ni mahali patakatifu na ile ya umuhimu wa muungano (dhambi ya Ubaguzi). Hotuba hizi zimekuwa zikitukumbusha bila shaka kwamba tunaweza kutumbukia pabaya na wengine wameogopa.

Pamoja na hayo hatuna sababu ya kufikiri sisi ni tofauti na wenzetu barani Afrika. Ni kweli watu binafsi wameogopa, wameogofiwa na kauli kali za Mwalimu, lakini CCM pekee imebaki bila kujali, ikitumia kila mbinu kubaki madarakani, na tena bila aibu kupiga kampeni chafu ikidai wengine ni wanaukanda, wadini nk. Badala ya mtu binafsi kama Nkurizinza Tanzania tunaona Genge lisilokuwa na jina na sura bali nyuma ya kivuli cha chama- namna ya ukoo mpya, dini mpya, jinsia mpya. Fikra za Mwalimu na Kauli Zake Kali bado kuzingatiwa!
 
..wakati wa kampeni Dr.Magufuli alisema fedha za ujenzi wa bagamoyo, tanga, mtwara, zipo.

..pia wananchi wameshahamishwa kwenye ardhi zao ili kupisha ujenzi wa bandari.

..na Raisi Kikwete aliamuru wote ambao ardhi yao imechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wajengewe nyumba.

..pia Raisi alimfukuza kazi afisa mtathmini wa ardhi kwa madai kwamba anazungusha na kuwanyima wananchi haki zao.

..msikilizeni Dr.Magufuli hapa:

cc MTAZAMO, Magurudumu, Bukyanagandi, Nguruvi3, Ngongo



Coz bagamoyo ni kwao ndo wajengewe nyumba ila sehemu nyingine wananyanyasika hata baada ya kutoa maeneo yao.
Kumbuka ishu ya wakazi wa kipawa kupisha ujenzi wa terminal III JNIA
 
kama hela zinatoka china kama unavyo dai sasa kwanini Tanzania wasitishe ujenzi huo na badala yake hela ziende kuboresha bandari zilizopo mie sipingi sana swala la kujenda hiyo bandari bagamoyo lakini je kina cha bahari upande wa bagamoyo kinatosha au ndo tena kazi ya kuchimbw inaanza.
kwanini wasijenge mtwara kama mapendekezo ya mwanzo yalivyo tolewa? y bagamoyo
Kama fedha ziliishapatikana kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, wakisitisha ujenzi huo, fedha hizo haziwezi kuhamishwa kufanya kitu kingine chochote!. Bandari hiyo ya Bagamoyo ingekuwa ndio bandari kubwa kuliko zote kwa bahari ya Hindi upande wa Bara la Afrika.

Huu usitishaji wa mipango iliyoshapata funding hauna tija kabisa kama hiyo mipango mbadala ndio kwanza mchakato wa kuitafutia funding ndio inaanza!.

Pasco
 
"The project has been suspended and not cancelled" ... Sijui mmeelewa ama mnakurupuka kuchangia kwa mihemko?!

Jiongeze ndugu hiyo ni Lugha ya Dipromasia kutuliza mihemko ya mkwere na Genge lake....unadhani ikikaa miaka zaidi ya 50 bila kujengwa utasema haijawa Cancelled au Wameandika na muda
 
Kama fedha ziliishapatikana kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, wakisitisha ujenzi huo, fedha hizo haziwezi kuhamishwa kufanya kitu kingine chochote!. Bandari hiyo ya Bagamoyo ingekuwa ndio bandari kubwa kuliko zote kwa bahari ya Hindi upande wa Bara la Afrika.

Huu usitishaji wa mipango iliyoshapata funding hauna tija kabisa kama hiyo mipango mbadala ndio kwanza mchakato wa kuitafutia funding ndio inaanza!.

Pasco


Ulikuwa mkopo ule hakuna hela hapo kaka icho kilikuwa kitanzi icho bora wakiepuka
 
Bandari Ya Bagamoyo Haina Ubaya Wowote.
Hivi Nchi Ikipata Rais Kama KUNA Eneo Anakotoka Linafaa Kwa MRADI Basi Aogope Sababu Tu Watu Kwa HISIA Kuliko MANTIKI Watasema Anapendelea Kwao???
Wanaiangalia Kila Jambo Kwa Ukabila BADALA ya Merits Ndio WAKABILA NO 1.
Mbona MIRADI Mikubwa Wakati Wake ya Barabara, UDOM, Madaraja KIGOMA, MORO,KIGAMBONI nk Nk Alijenga Kwa Kupendelea???
Mtwara, DAR Sawa , Bagamoyo Dhambi Kuwa Na Bandari??
Sio Sehemu Ya Tanzania???
Rais Wetu Mpendwa JPM Alitoa Ahadi ya Kujenga Daraja Katika Kivuko Cha Busisi Mwanza-Sengerema Juzi Nimeona Zimetengwa 400m Ajili ya Feasibility Studies Kuna Ubaya Gani Mfano As Long as MRADI Unafaa????
Wakati Tunashangaa Bagamoyo Kujengwa.
Kenya Wanaboresha Mombasa Kwa Mabilioni ya Dola, Kujenga Bomba La Mafuta Kenya -Uganda- Kigali.
Wanajenga Standard Gauge Railway Hivyo Hivyo.
Wana MRADI Mpya Mkubwa Wa LAPPSETT wa Bilioni 7 Usd Na Wanausukuma Kwa Nguvu Uende.
Bandari Mpya Kabisa Pembeniii ya Mombasa LAMU NA RELI NA BOMBA LA MAFUTA KWENDA ETHIOPIA.
Sisi Hapa Tumekalia SIASA ZA FITNA, UMBEA NA MAJUNGU.
Eti MRADI wa Bagamoyo Haukuwa Na Manufaa.
MRADI wa DAR Wafadhili Ni Benki ya Dunia.
Bagamoyo Port Ni CHINA NA OMAN FUND Havihusiani Unasimamishwa Kwa Vigezo Gani Kama Sio CHUKI NA FITNA TUUU.
 
kumbe ndo maana akawahi ikulu kuomba isisitishwe.....ukitaka kumuua nyani....
 
Kuna Mtu anaongelea mambo ya 3G na 4G ambazo bandari za wenzetu zinalenga kuanzisha na hivyo kama nimemuelewa vizuri anasema tutashindwa kuingia katika ushindani na bandari za wenzetu. Swali langu ni Je, bandari za Dar, Tanga na Mtwara haziwezi kuboreshwa na kuingizwa hiyo mifumo ya 3G na 4G? (kama ni mifumo/technolojia anyway). Au hili lingewezekana tu kwa kujenga bandari ya Bagamoyo. Ni maoni yangu kuwa serikali imefanya tathimini ya kutosha juu ya hasara na faida za ujenzi wa bandari mpya kwa sasa kabla ya kufikia hatua iliyochukuliwa ya kusitisha ujenzi huo. Hivyo binafsi napongeza uamuzi uliochukuliwa na serikali wa kusitisha mradi huo.
3G na 4G ni bandari zenye kina kiefu cha maji kuweza kupokea ile mimeli mi kubwa, mi giant ya mafuta!, ambapo kwa Bandari zilizopo huwezi kuziboresha!, hii itamaanisha kubomoa kila kitu kilichopo na kujenga upya!. Kama ni kuboresha zilizopo ili ziwe na uwezo huo, huko hakutakuwa kuboesha, bali kujenga upya adjecent na zilizopo!.

Kama ni bandari ya DSM, then eneo lote la Kurasini hadi Mtoni Kijichi litahusika na daraja la NSSF itatubidi tuling'oe!.
upload_2016-1-8_19-46-46.jpeg
upload_2016-1-8_19-46-46.jpeg
Search Results
upload_2016-1-8_19-47-38.jpeg
upload_2016-1-8_19-47-38.jpeg
upload_2016-1-8_19-47-38.jpeg
upload_2016-1-8_19-47-38.jpeg
 
Sasa hauoni kama tungejenga Terminal III ya kuchukuwa abiria milioni 6 /mwaka, mwaka 1980 ingekuwa ni white elephant project? Ambapo leo hii ni lazima tungeuvunja tu kwa maana kwanza ungekuwa umechakaa na usingekuwa wa kisasa kulingana na teknolojia iliyopo? Halafu kama wakati huwo watu waliokuwa wanatumia uwanja wetu walikuwa chini ya Milioni huoni kwamba jengo la kuchukuwa milioni 6 lingekuwa ni hasara kubwa?
Haya ndiyo mambo yanayotushinda Afrika, ni wapi tutumie fedha na miradi ya aina gani tuanzishe!

Ndiyo maana kwenye uchumi kuna projections hiyo project ni white elephant ni feasible zaidi kama tukiwekeza kwenye Bandari ya Tanga, Mtwara, kwenye maziwa yetu Kigoma, Mwanza, Musoma, Bukoba Ziwa Nyasa kote huko kunahitaji Bandari na hii ina make economic sense klk kutumia mabilioni kujenga Bandari Bagamoyo wakati 100 km kuna Bandari tayari ya Dar!

Hakuna mtu anayeelewa uchumi ambaye anaweza kuukubali mradi kama huu, hauna tija kabisa!
Hoja hapa ni kwamba project kubwa kama bandari huangalii miaka 10-20 ijayo bali unaangalia over 50 years!! Ikiwa unaona Uwanja wa abiria 6M ingekuwa ni white elephant; ni nani kati yetu na Kenya anafaidika kwa kuwa ni gateway? Ule Uwanja wa Jomo Kenyatta umejengwa miaka ya 70... leo hii, Kenya wanaona Jomo Kenyatta haitoshi na wanataka kujenga terminal itakayo-accomodate 20 million passengers annually wakati kwa sasa wanapokea roughly 6 millions!!! Na bila shaka nadhani unafahamu kwamba pamoja na Mombasa kuwa ni bandari kubwa kuliko Dar lakini kv wenzetu wanaangalia 50 years to come; nao wana mega project sawa na ya Bagamoyo ambayo wanataka kujenga Lamb! Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani ule mradi walitaka ku-team up na China lakini China wakaamu kuja Bagamoyo probably kv tayari wana another mega project Djibouti!!

Kwa staili hii Wakenya wana kila sababu ya kutuona maboya....
 
Kama fedha ziliishapatikana kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, wakisitisha ujenzi huo, fedha hizo haziwezi kuhamishwa kufanya kitu kingine chochote!. Bandari hiyo ya Bagamoyo ingekuwa ndio bandari kubwa kuliko zote kwa bahari ya Hindi upande wa Bara la Afrika.

Huu usitishaji wa mipango iliyoshapata funding hauna tija kabisa kama hiyo mipango mbadala ndio kwanza mchakato wa kuitafutia funding ndio inaanza!.

Pasco
Ndio maana kila siku tunasema hakuna 'vision wala mission' kuhusu uelekeo wa Taifa
Kama mradi huo ulipitishwa na Cabinet na miezi 3 Cabinet nyingine inausitisha, maana yake ni kuwa waliokuwa katika Cabinet ya JK ambao ni Mh Rais na Mawaziri waliopo sasa hawakukubalina na mradi huo wakati huo. Sasa wanatoa hisia zao.

Katika hali hiyo, tunacheza mdumange maana kesho ataibuka mwingine na kuzua lingine tena

Mambo kama haya yanatakiwa yapitie katika taasisi kama bunge ili kujadiliwa kwa kina na kuwa na kumbu kumbu
Sikumbuki kama hilo lilifanyika zaidi ya kusikia mradi huo umeanza

Hata usitishwaji wake unatia shaka maana hakuna sababu za kitaalamu zilizotolewa. Kama pesa imepatikana nini tatizo?

Mjadala wote unajikita katika hoja moja, hatuna mfumo unaohakikisha vision na mission kwa Taifa

Na 'factor' muhimu hapa ni CCM ambayo inaunda serikali miaka 50 na bado hatuonekani kujua tunakwenda wapi

Hii ni felia na ndicho tunachosema, bila kukaa chini na kujiwekea utaratibu (mifumo) tutasikia mauza uza kama haya kila uchao

Watu wanalala wakiamka wanabadili njia na gia, sisi tupo nyuma tukishangilia !

Tumevaa njuga na manyanga tunaserebuka na hapaNdima tu. Hatujui kazi gani lakini tunaimba tu. Hakuna cha ajabu mbona tunaimba nyimbo za kikongo bila kujua maana yake!

Judi wa Kishua (mpwa)
 
Leo ndo nimekiri kuwa tanzania hatuwezi kuanzisha na kusimamia miradi mikubwa , ni wazuri sana kwa kubuni, likija swala la implementation tunakimbia. Leo tumeanza issue za kusema mara ohhh we need standard gauge reason behind kenya wanajenga standard gauge, huu mradi wa reli upo, na juzi kati tulisikia mzee six anasema wameweka jiwe na msingi, kwa hiyo ni wawekezaji wawili tofauti. Inabidi tuondokane na tabia hii ya kuogopa ogopa, we can have all simultaneously, uchumi wa kati hauji kwa maneno tu na kukumbatia miradi kama ya upanuzi, sijui upgrade, kujenga mabanda /containers za kufanyia clearance Tanga/Mtwara. Tunaridhika kabisa na tunakaa hapa tunahesabu ohh tuna bandari tatu, ziko wapi hizo bandari tatu tanzania? its jokes.

Mkuu unaambiwa kupanga nikuchagua Kwa mujibu wa Mkataba inasemekana baada ya ujenzi kukamilika..mchina ataHold hiyo Bandari kwa 40yrs arudishe Gharama zake...naujue ..kwa kipindi hicho hiyo bandari itachukua mizigo mingi kuliko ya DAR..MTWARA na TANGA ziko chini ya Serikali...kwahiyo unaona nivyema mchina anufaike kuliko sisi...Inasemakana itajengwa ila kwanza tuboreshe hizi tunazomiliki kwa % 100 then wachina wataruhusiwa
 
Hapana itaendelea kupaa.

Hizi pwani zimebarikiwa huwezi kushindana nazo hata chembe. Ukiiua bandari utakuta kuna mafuta na mi gas ya kufa mtu.

Hapo sasa.




Kwahiyo unataka kutuambia bagamoyo kuna gesi...wewe kama ulikosa ata uje wa nyumba kumi kipindi cha mzee msoga sahau kabisa
 
Home

Pitia hiyo link hapo juu
Mikataba ya aina hii iko mingapi? Magufuli ana kazi kweli! Mungu akuzidishie courage na hekima Magufuli ya kupambana na haya manyang'au (for want of a better word).

Nimekumbuka wimbo wa wamerekani weusi: hii ni sehemu tu

The more you refuse to hear my voice
The louder I will sing
You hide behind Walls of Jericho
Your lies will come tumbling
Deny my place and time
You squander wealth that's mine
My light will shine
So brightly it will blind you
Because there's,

Something inside so strong
I know that I can make it
Though you're doing me wrong so wrong
You thought that my pride was gone, oh no
There's something inside so strong
Something inside so strong.

Magufuli you are standing tall for all of us. Thank you
 
Mnajaribu kila njia ku attack character lakini ikija kwenye issues za ukweli hamumuwezi.

Kikwete anadunda na ana rikodi ambayo mpaka sasa hakuna wa kabla yake aliyeifikia. Na ikitokea wa sasa akiifikia basi hilo pia ni chaguo lake, au mmesahau?


Mzee wa msoga amekutuma kuja kumtetea humu aiseee....kamsaidie kulima unasema anarekodi labda za kufikisha nchi tulipofika
 
hapa ndipo utajua bongo wajuaji ni wengi sana...🙁
 
Halafu nikisoma comments za watu humu nina mashaka ikiwa wanaifahamu vizuri bandari ya Dar es salaam na adjacent areas!!

Waungwana msioifahamu vizuri Bandari ya Dar na maeneo ya jirani--- leo hii ukitaka kuipanua bandari ya Dar na iweze ku-meet changamoto za miaka 50 ijayo basi karibu nusu au hata 3/4 ya Wilaya ya Temeke itabidi ivunjwe! Changamoto ya kwanza ni container terminals.. sie tuliokulia maeneo ya karibu na bandari ya Dar tumepata akili tukikuta bandari haina maeneo! Kule Kurasini zamani baadhi ya nyumba ilikuwa ukifagia; takataka unasukumia baharini...
maeneo ambayo kimsingi yalitakiwa yawe eneo la Bandari! Leo hii bandari wakitaka hata kujitanua kidogo tu, lazima wavunje nyumba za watu! Mbaya zaidi nyumba karibu zote za kiraia wameshavunja na soon wataanza kuvunja nyumba zao wenyewe ambazo waliwauzia wafanyakazi na baada ya hapo wakimaliza maeneo machache ya kiraia yaliyobaki labda wageukie police line!!!

So, nyie mnaosema wapanue Dar, hiyo itakuwa ni short term solution lakini kama tunataka long term solution Dar hapafai! Hii inastahili kuchukua crown ya second largest port in the country lakini sio first!

Halafu JF inakutanisha vijana lakini wanavyoongea utafikiri wameaminishwa Tanzania itakuwa maskini forever!! Per capita GDP ni chini ya $1000 lakini tayari bandari ya Dar imeelemewa na umaskini wetu huu huu! Hapa purchasing power yetu iongezeke japo kwa 50% tu (still tutakuwa nchi maskini) kiasi cha ku-attract more and more imported goods; hapo hapo bandari ya Dar inaenda ICU halafu bado watu eti mnaona mradi wa Bagamoyo ni libandari likubwa ambalo hatulihitaji??!! Halafu kanchi kadogo na maskini kama Djibouti ambao kuna mradi kama huu nao wasemaje?!
 
Wana JF hivi mna maelezo yanayoleta tija nzuri ya kupinga kwa ujengwaji wa Bandari mpya ya Bagamoyo?

Tuleteeni points za maana, acheni siasa mambo mengine muwaachie wataalamu, kazi yetu ni kuhoji kwa nini wamesitisha na kama hajutapata majibu ya kuleta tija basi tuzame kufanya utafiti sio kulopoka humu mitandaoni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom