Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Serikali yasitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kuimarisha Bandari za Mtwara, Dar

Status
Not open for further replies.
Ikiwa uyasemayo ni kweli,kwanini sasa watake kuimiliki bandari kwa muda huo tajwa?wanapata nini hapo bandarini in return?
Kuna Mdau mmoja hapa nimemuuliza hayo mapato yote ni mapato yapi lakini hajanijibu labda nisaidie wewe kunipa darasa!!

Can I tell you something?! I am afraid ikiwa kweli unalifahamu vizuri hili suala kwa jinsi issue ya kodi ulivyoita vikodi!!

Guys, pesa nyingi bandarini inachukuliwa na TRA na sio TPA!! Na mapato ya TRA yanaongezeka kadri mzigo unaopitia bandarini unavyoongezeka; keeping other factors constant! Pesa inayoingia bandari ni ndogo sana ukilinganisha na inayoenda TRA! Na kv bandari ya Dar hawana eneo kubwa kimapato ndo wanaathirika zaidi na ndio maana sehemu kubwa ya mzigo unahifadhiwa na Privately owned ICDs!

Kule Bagamoyo, hata kama bandari itakuwa funded na Wachina kwa 100%; mapato/kodi za TRA through imports and export Mchina hazigusi kwahiyo ndo maana umenishangaza unaposema vikodi unless kama unamaanisha kodi zitazolipwa na Wachina wenyewe! Ikiwa bandari itakuwa na uwezo wa kupitisha mzigo mara 3 ya sasa, maana ake ni kwamba hata mapato ya TRA yatapanda kwa similar proportionality!

Halafu nitarudia tena kwako!! Bandari 3 au 4 sio nyingi kama mnavyodhani.... kwa sasa zinaweza kuonekana nyingi kv we don't produce so we don't export! Likewise, our purchasing power ni ndogo so we don't import much! Kwahiyo mnaweza kudhani bandari ni nyingi kumbe msingi wake ni bandari kutumiwa na nchi maskini! Leo hii uki-import smart tv milioni moja zitakudodea but assume nchi zinazutumia bandari ya Dar zinakuwa kiuchumi angalau mara tu na hivyo kuongea exports na purchasing power ya imported goods.... hivi bado hapo unaamini Dar port itakuwa abandoned kwa kukosa mzigo?!
 
Ningekuwa mimi ndio mwenye majukumu ya ile awamu iliyopita.,...nisingesaini mkataba October wakati Rais mpya anaingia November. Ni kukosea katika kupima uzito wa mambo.
 
Daaa jpm unamfanya yule mkwere achanganyikiwe aise yaani nahis adi sasa hivi anataman kukimbia nje na price mamaaaaaaaaa anataman kufa walifanya nchi kama ya kwao vile wanataka bagamoyo igeuke kama ulaya ee
 
Mawazo yako ni mazuri na ndy lengo la serikali lkn huna kitu unamadeni unaanza kukidisha kila kitu kwa wenzio utaibuka lini. Imesimamishwa kupisha uimalishaji wa miundo mbinu kwanza hakuna reli yaani unawaza kuwa na benzi hata baiskeli huna. UTUMWA WA MAWAZO
Kupisha miundombinu ipi wakati according to the Citizen, wanataka kuonesha gati 1-7; 13 & 14 za bandari ya Dar na kisha kuboresha Mtwara!

Lakini vilevile hakuna anayepinga kuboresha bandari ya Dar lakini huwezi kusitisha mradi mkubwa kama wa Bagamoyo kwa ajili ya Dar ambayo nishasema hapo awali kwamba hata maeneo ya kujenga container depots hamna unless kama wanakusudia kuimaliza Temeke yote na kuibadilisha kuwa eneo la maghala!
 
The Construction of the 10 billion (about Sh22 trillion) Bagamoyo Port has been suspended, The Citizen has learnt. The government wants to focus instead, on improving the capacity, performance and efficiency of the Mtwara and Dar es Salaam ports.

The Minister for Works, Transport and Communications, Prof. Makame Mbarawa, confirmed yesterday that the construction of what would be the largest port in Africa has been suspended, not shelved to pave way for upgrading berths 13 and 14 as well as developing the Mtwara Port depending on the availability of Funds. The activities would take years to complete, the minister said because the process has to start from finding funding.


Source: THE CITIZEN
View attachment 315504
 
Sawa mkuu ila tunauhitaji mkubwa sana wa bandari mtwara kwa sasa kuliko bagamoyo.pia kama tutaboresha kwanza bandari ya dar na ika perfom to the maximum itatupa tija sana wakati wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo.

gudbye mkwere
Bandari ya Dar ina changamoto chungu nzima ni nifinyu sana, itatugharimu an arm and leg tukitaka kuipanua, kwa nini hatuendi kupanua Bandari ambazo zina a kina kirefu
Bandari ya Bagamoyo serikali inatoa kiasi gani cha pesa? tusifuate mambo ya wanasiasa, Tanzania hata nchi baadhi ya africa haina uwezo wa kujenga bandari Ilikuwa ni jukumu la serikali kuwashawishi hao wawekezaji kuwa inafaa hii bandari ijengwe sehemu zile ambako wao wanaona sio kukataa dmradi, na ikiwa muwekezaji anaona bado option nzuri ni bagamoyo basi aendelee na plan hiyo. Hapa tunasema kuna halafuNashangaa tunasema huu mradi uligubikwa na usiri ,sijui wizi, mara ohhh sio priority yetu, sasa unataka tuwaambie wahisani acheni kujenga bagamoyo kwani sio pririoty yetu? au ajenge na sisi tuendelee na plan zetu? mimi sioni logic hapo, serikali ya iendelee na upanuzi na wawekezaji wandelee na mradi huo.
Well said mkuu, mimi sidhani Serikali ina mpango wa kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, kama kuna mpango wa kujaribu kuweka spana kwenye Project hii nzuri basi Dunia itatushangaa, I hope hakuna external forces ambazo zina excert pressure kwa viongozi wetu ili wasitishe mpango huu mzima.

Wakati mwingine magazeti ya Citizen na Mwananchi yana kawaida ya exaggerate nambo madogo - wanakuza out of proportion 4 some reasons ambazo wanazijua wao, haingii akilini kwamba Serikali inaweza ku abandon Project kubwa ya ujenzi wa bandari ya kisasa na yenye manafaa makubwa kwa Taifa letu kwa kuendekeza ushauri ambao hauitakii mema Taifa letu - tukifanya mchezo washindani wetu watatuzidi kete,tutabaki tunajilahumu kwa ujinga wetu - si China wala Oman wataendelea ku entertain ujinga wetu, watakwenda kuwekeza kwingine.
 
Kama itakuwa habari hizi ni za Uhakika, basi nitaamini kuwa sasa Tanzania tumepata Rais bora na siyo BORA Rais kama aliyepita.

Asisahau na kimeo chake cha MV DAR ES SALAAM. nacho ni kijipu uchungu japo sijui atakitumbuaje
 
Hapo safi sana, ilikuwa na ulazima gani wa bandari pale😱 ingeboreshwa bandari ya tanga ingekuwa imeshakamilika na kutoa ajira zaidi na serikali ingepata mapato ya kutosha, hongera kwa hilo..!!
 
Bandari ya mwaa kivyake na ile kivyake.

Habari imekaaa kiudaku zaidi na siwezi kuishadidia mpaka nione tamko rasmi la serikali.

Strategically Bagamoyo Port ni better kuliko Dar.
Yeah strategically kwa nyie silent bahari
 
Hapo wawekezaji walioingia mikataba watakula fedha ya bure kama hii habari ni ya ukweli.

Huo mradi wa Bagamoyo unajengwa kwa ubia kati ya nchi moja tajiri ya kiarabu na nchi ya china kwa makubaliano ya kuuendesha kwa miaka 50 ndipo waiachie Tanzania bandari yake.Waliofaidika ni watanzania wenzetu walioukaribisha mradi na asilimia zao walishachukua iwe kwa manufaa ya nchi au kinyume chake mmeshaisoma na mwiha ashalipwa ujira wake. Bandari hiyo itakuwa na kituo cha jeshi la china kupokelea manowari zake na vifaa vingine vya kijeshi na kuvisambaza kokote wanakotaka na hiyo inaipa marekani hofu. Kwa ushauri wa wataalam wa bandari wa kimataifa wamesema kwa miaka 25 ijayo ndipo matumizi sahihi na yenye manufaa kwa taifa yataanza kuonekana. Ushauri wao kwa sasa wanasema ni bora kuimarisha bandari zilizopo za Dar,Tanga na Mtwara pamoja na reli zetu. Naona hili ndilo lililomuingia raisi Magufuli na kuagiza hiyo bandari ya kisiasa kusimama kwanza nami na walio wengi tunamuunga mkono kwa hilo.
 
Kwa sababu Bagamoyo ndio karibu zaidi na kitovu cha biashara cha Afrika Mashariki, Dar Es Salaam.

Na hizo nyingine zote si vibaya kuwepo zenye ubora.
Sasa huu ndo umasikini wa mawazo. Kwanini kitovu cha biashara kiwe Dar pekee?? Lazima tufike mahali tuwe na diversifications. Kuhudumia Kaskazini iwe ya Tanga, Kusini iwe ya Mtwara na hii itasaidia kuipunguzia kazi ile ya Dar. Watu tunawaza ni namna gani tutaondoa foleni ya kila kitu Dar, bado wengine mnawaza kuiongeza. Tupanue wigo na kila zone iwe economically strategic.
 
Mimi binafsi sijafurahishwa na kitendo cha serikali cha kusimamisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo kwa sababu ingepunguza foleni ya malori yanayokuja huku dar. Na ninaamini kwa hili mzee wa msoga alikuwa na sababu za msingi na ambazo kama Magufuli akienda msoga ataelezwa sababu zote kiundani. Kwa hili wakuu, nafikiri mzee wa msoga hakukosea sana hata kama ni nyumbani kwao
 
Ndugu yangu faizaFoxy, kwanza nashukuru sana kwa mawazo yako, walau tunaelekea sehemu nzuri, maana hoja zilizokuwa zinatoka sikuzielewa, maana investment ya 10 B usd sio ya kukataa hivi hivi, Tanzania inahitaji investment za maana sio mchezo mchezo maana tuko kwenye dunia ya ushindani. Lakini swala kama hili magufuli alitakiwa awaambie hii bandari haina uhusiano na issue za kijeshi, na ni opportunity pekee kwa taifa letu. Nakumbuka ujenzi wa TAZARA , Mwl aliwaomba wamarekani waje wasaidie kujenga reli Tanzania wakakataa, ndipo mwl akaenda kuomba wachinese, walipokulbali wamarekani walimpiga vita sana mwl, lakini bahati nzuri mwl na mao ze dong walikuwa ni watu wenye msimamo ,hatimaye reli ile kujengwa. Hapa kuna watu wanabeza investment of 10 B USD, lakini hawajui impacts zake katika uchumi wa tanzania, na hapa kuna nchi nyingi sana zinahofia competitions kati ya tanzania na nchi hizo baada ya Bandari hii kukamilika. My take, ilikuwa ni bora Tanzania, china, Oman na USA wajadili hii issue kabla hajaifuta. Maana tunaoathirika ni sisi.
 
Lakini kwenye Kampeni watu wa Bagamoyo walielezwa nini kuhusu hiyo Bandari ambayo ujenzi wake sasa umesitishwa?
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kama nchi tunakabiliana na ushindani wa kibiashara ktk ukanda wetu tunahitaji bandari mpya na ya kisasa ili tuweze kushindana kibiashara na nchi jirani. Swali je bandari mpya itajengwa wapi kwa maoni yangu sijali itajengwa wapi kama ni Mtwara Tanga Bagamoyo yote ni Tanzania je kama ni kweli ujenzi wa bandari ya Bagamoyo imesitishwa ni kwasababi ipi? Gharama au sisi kama nchi tulikuwa hatupati faida kwa miaka hamsini serikali ikaona huo mradi hauna tija kwa masirahi ya Taifa? Tunataka maelezo ambayo wananchi yatatupa mwanga kwanino serikali imesimamisha ujenzi huo na plab B ni ipi? sio kwenda kukarabati bandari ya mtwara na tanga bora liende huku tunapigwa bao na wakenya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom