Mkuu majibu ykuhusu ushiriki wa Magufuli, kuelewa mradi na kuutumia katika kampeni yanapatika bandiko 410 la mkuu
JokaKuu au unaweza kusikiliza kupitia link hii
magufuli akemea uchochezi - YouTube
Mkuu Cabinet ndicho kikao kiuu cha ushauri cha Rais na serikali.
Mawaziri wakila kiapo wanaapa kutunza siri za vikao... Hakuna excuse fulani alikuwa wizara hii na yule ile, uamuzi wao ni wa pamoja 'collective responsibility''
Kama unanisoma vema na mabandiko yapo wazi kwa reference, kiongzi anyefanya vema Nampa big up, akiboronga Nampa failure. No more no less
Nafanya hivyo kwasababu naamini katika Taifa si mtu au vyama
Unapouliza Magufuli na Lowassa nani alifaa kuwa Rais, kwanini usiulize Dovutwa na Kuga Mziray wa TPP Maendeleo?
Unajaribu kuhamisha mjadala u-fit theory zako na si ukweli ulivyo.
Hapa nitakupa ukweli kwasababu nimeandika sana na rekodi zipo
Nimesema, nchi haiondoki ilipo ichini ya CCM. CCM si chama imegeuka genge. Nikaendelea, kama Dovutwa au Kuga Mzira wataiondoa CCM hilo ni heri.
Nilisema, haina maana ni viongozi wazuri, bali kuondoa CCM ni jambo muhimu kuliko jingine. lolote . Genge lililotufikisha hapa linageukaje kutuongoza tena?
Ushahidi wa miaka 10 ni haya tunayoyaona. Waliosadia kutufikisha hapa ndio hao waliounda serikali. Kamati kuu ya CCM na NEC ni ile ile iliyopitia mradi wa Bagamoyo kama chama tawala
Mh Nape Nnauye katibu mwenezi wa CCM, na waziri wa habari na maelezo amethibitisha maneno yangu. Ametamka nchi ilifikia mahali pa baya, hadharani
Ni huyu aliyetuambia nchi inaendelea vema chini ya CCM miaka 10, leo anaona alichokuwa hakijui akiwa ngazi za juu, iweje wengine muendelee na'' mgomo ''
Hoja hapa si Magufuli, ni jinsi nchi isivyo na mifumo ya kuweka maendeleo endelevu. Miradi ni kazi za kitaalamu si kisiasa.
Tuliwaambia Bagamoyo ni white elephant. Hawakutusikiliza , leo wanasemwa ni ''mashujaa'' baada ya kuona felia! eti tusiseme.
Wengine hatukuwepo katika siasa tulisimama na Taifa wao walishiriki vikao
Wana dhima ya kutueleza nini kimetokea. Kwanini mradi walioamini
magufuli akemea uchochezi - YouTube umefeli.
HaTutataki habari za gizani kama ulivyoletwa bali maelezio, si ''cheap politics''
Miradi ya Kitaifa lazima iwe mbali na siasa. Tuweke mfumo miradi hiyo iendeshwe kwa utaalamu na uwazi.
Tujue nini kinaendelea si kujificha nyuma ya miogongo,waombe radhi.
Kwa mfano ningalikuwa hakimu mka wa mahakama na kesi ya namna hii ikaja , ningeweka makundi mawili 'wahalifu' na accomplices
Tushirikiane kuwauliza, walishiriki kutupeleka 'porini' wameona nini mbele na wanataka twende wapi
Nchi haitabadilika kama hatubadli mind set za ndiyoo bila ku reason.
Mind set za kudhani criticism ni dhambi, uzalendo ni kuvaa njuga na manyanga.
Mindset zisizoweza kuangalia mbali bali kila jambo kwa mtizamo wa siasa.