Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
806
Reaction score
2,049
Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

"Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya
mafuta nchini," amesema.


=====

Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.

Ametoa mfano wa eneo lililopangwa kuendeleza ujenzi wa maghorofa vibali vifuate mpango.

Source: Mwananchi.
 
Huu ni usanii, nani asiyejua kuwa ridhiwani alipelekwa ardhi kufanikisha upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya vituo vya lake oil ambavyo vimechipuka kama uyoga baada ya pesa fulani kupigwa.
 
Dk Angeline Kusimamisha ujenzi wa vituo vya mafuta inaonyesha umeichoka wizara ya ardhi.

Sasa unatafuta kushika simba masharibu au ndevu na dawa utaipata.

Sasa wengi wataanza na kufuatilia hiyo Phd yako ulivyoipata iwapo wengi walikuwa wamepiga kimya.

Visima vya mafuta vingi na vinavyojengwa ni vya naibu wako na mtoto wa mtu mkubwa.

Baraza la mawaziri linasukwa upya utajikuta kukipigwa chini kama Mulamula
 
Huu ni usanii, nani asiyejua kuwa ridhiwani alipelekwa ardhi kufanikisha upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya vituo vya lake oil ambavyo vimechipuka kama uyoga baada ya pesa fulani kupigwa...
Jamaa wana vituo aisee
 
Acha bangi, Ridhiwani na lakeoil wapi na wapi, acheni kuwaongopea watu
Watanzania wengine wana roho ya kichawi

Mimi sioni shida hata hiyo kampuni ikimilikiwa na mtanzania ngozi nyeusi mwenzetu yeyote awe Ridhiwani au yeyote

Watanzania ngozi nyeusi baadhi hawataki kuona wenzao ngozi nyeusi wanamiliki kampuni kubwa za mafuta wanataka ngozi nyeupe tu hivi shida nini?
 
Back
Top Bottom