Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Lake Oil kila kona ya nchi hii, yaani ni tishio
 
Ukija pale jkt mlalakuwa kuelekea kawe kuna kituo,na pale paliwa makazi,ukija maringo njia panda kawe kna kituo...
Kino studio kituo ....
Ila hawa wafanyabiashara wana nguvu lazima watakuja na plan B [emoji1]

Ova
Halafu vyote vipo kwenye hatua ya ukamilishaji ,bado Mikocheni near Heinken house.
 
Wamemaliza kutakatisha ndio wanazuia, kwa wale waliokuwa wanadunduliza siku watimize ndoto zao ndio imetoka iyo
 
Serikali imesitisha kutoa vibali vipya kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta pia imezuia kubadilisha matumizi ya ardhi ili kujenga vituo vya mafuta kwa miezi mitatu ili wizara iweze kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini.

Siku za karibuni kulikuwa na angalizo kutoka kwa wadau juu ya kasi kubwa inayoendelea ya ujenzi wa vituo vipya vya mafuta.
 
Attachments

  • 315302010_1212194896379435_46566828266003287_n.mp4
    7.2 MB
Mama shughulikia hati za viwanja...watu wapate hati hayo mengine huyawezi...kwenye sekta ya mafuta kuna fitna kali sana..watakutoa hapo
 
Vimejengwa kwa kasi sana, sasa kila hatua mia mbili unakutana na kituo cha kuuza mafuta na vingi vipo karibu na makazi ya watu, sidhani kama wahusika waliangalia usalama wa majirani wakati wa huo ujenzi, sababu ni kujuana tu, tunasubiri litokee janga ndio tuanze kuulizana kulikoni kama kawaida yetu.
 
Mama Mh Waziri naona ametakata sana na tranformation kubwa from villager to township
 
Serikali imesitisha kutoa vibali vipya kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta pia imezuia kubadilisha matumizi ya ardhi ili kujenga vituo vya mafuta kwa miezi mitatu ili wizara iweze kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini.

Siku za karibuni kulikuwa na angalizo kutoka kwa wadau juu ya kasi kubwa inayoendelea ya ujenzi wa vituo vipya vya mafuta.
expand...
Hawa watu wana nguvu ya kufanya watakavyo. Fikiria kuna mtu anajenga katikati hifadhi ya barabara ya njia nane pale Kimara Stopover hakuna anayemuuliza.
 
By Sharon Sauwa

Mwandishi wa Habari
Mwananchi

Muktasari:​

Kufuatia ongezeko la ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchini, Serikali imesitisha ujenzi huo ili kutoa nafasi ya kufanya tathimini ya ujenzi wa vituo hivyo.

Dodoma. Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.
Ametoa mfano wa eneo lililopangwa kuendeleza ujenzi wa maghorofa vibali vifuate mpango
 
Mh Waziri unarudisha nyuma maendeleo
Acha vituo vijengwe viturahisisshie upatkanaj wa Mafuta
 
Acheni roho mbaya, yaani mnataka wahindi na waarabu tu ndio wawe matajiri?
Twende kazi rizi
 
jambo la msingi wafanye tathimini haraka, kisha watoe maelekezo waendelee na ujenzi.

Angalizo.
Wizara iwe makini sana katika kukisimamia jambo hili kwani inaweza kuwa chanzo cha RUSHWA.
uadilifu na uwazi unahitajika sana kwenye jambo hili.
 
Hawa watu wana nguvu ya kufanya watakavyo. Fikiria kuna mtu anajenga katikati hifadhi ya barabara ya njia nane pale Kimara Stopover hakuna anayemuuliza.
Hahaha! Ni TANROADS wame lease eneo itakuwa.
 
Back
Top Bottom