Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Wee akili huna hivi nchi hii kupata vibali vya ardhi kujenga shell mpaka ridhiwani awe naibu waziri wa ardhi?naibu waziri kwaza Hana uwezo wa kutoa kibali
Akili yako imeoza
 
Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

"Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya
mafuta nchini," amesema.


=====

Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.

Ametoa mfano wa eneo lililopangwa kuendeleza ujenzi wa maghorofa vibali vifuate mpango.

Source: Mwananchi.

Yaani vituo vya mafuta mijini vinajengwa hata maeneo ya kufanya huduma nyingine yanakosekana
Kwa mtazamo wangu anayesababisha hii chnagamoto ni EWURA
wanawezaje kuachia biashara ifanywe bila Ushindani?
Natamani EWURA iendeshwe na wafanya biashara na sio kuendeshwa na wasomi ambao hawana uelewa wa biashara. Hivi unawezaje kuweka bei ya juu na bei ya chini halafu uite bashara? hapo ni kukaribisha Huduma mbovu kwani mtu anajua kwa vyovyote vile atauza tu kwani bei ni moja hivyo hata hana haja ya maboresho...
1. Kibiashara nafikiri wangeweka bei elekezi ya juu tu huku chini watu washindane
 
Wafanyabiashara wakubwa hawataki upinzani wakiona watu wengine wanaingia wanatumia nyundo ya Serikali kukataza kwani Serikali si ndio wanatoa vibali kwa nini wasiendelee kusimamia vibali kwa usahihi ni kama wanaojenga hivyo vituo wanajenga bila usimamizi wowote ndio wameamua kutoa hilo Tamko...
 
Back
Top Bottom