Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Serikali yasitisha ujenzi wa vituo vya mafuta

Punde tu baada ya kufariki kwa JPM, vituo vikaanza kujengwa mpaka kwenye makazi ya watu.

NA KWA UTENDAJI WETU HUU HUU, SITAKI KUWA MTABIRI KUNA SIKU WENGI WATAZIKWA KWA MAFUNGU MAFUNGU BAADA YA KITUO KULIPUKA.

EBU NENDA PALE NJIA YA KWENDA WAZO KULIA KUNA KANISA KKKT WAZO, KUSHOTO KUNA KITUO.
 
Wakati duniani kote Sekta binafsi inawekewa mazingira rafiki , Nchini Tanzania hali ni Tofauti .

Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Ardhi , Anjelina Mabula , imetangaza kuzuia ujenzi wa vituo vipya vya mafuta kuanzia leo , kutokana na kinachoitwa kufanya kwanza Tathmini , Zuio hilo ni la muda wa miezi mitatu

Chanzo : Mwananchi
 
Makamba ndo aliyetangazia watu wajenge vituo na serikali itawakopesha mitaji. Kujisahihisha si ujinga.
 
Kwahio unataka vituo vya mafuta viwepo kila kona kama vile duka la peremende ?

Na siku ikutokea moto ndio tutajikaanga, haya mambo inabidi yafuate sheria kuna minimum distance baina ya kituo na kituo for safety reasons as well...

Ila hii itakuwa ni kujikosha tu kutokana na backlash wa Naibu wake kuhusisishwa kutumia hii fursa kugeuza kila open space kuwa kituo cha mafuta
 
Acha bangi, Ridhiwani na lakeoil wapi na wapi, acheni kuwaongopea watu
Siku hivi huku Mitaani yamerudi yale ya Awamu ya nne kila Gari nzuri kila Nyumba nzuri ni ya Riziwani😁😂
 
Lake ndio anaongoza kwa vituo vya wese kwa TZ.
Ukija pale jkt mlalakuwa kuelekea kawe kuna kituo,na pale paliwa makazi,ukija maringo njia panda kawe kna kituo...
Kino studio kituo ....
Ila hawa wafanyabiashara wana nguvu lazima watakuja na plan B [emoji1]

Ova
 
Maana vituo vya mafuta zilikuwa zinajengwa mpaka maeneo ya makazi ya watu

Ova
Yaan ilikuwa hadi kero hadi unashangaa
Mfan Ukianza kwa tumbo tandare mpk darajani sinza kuna vituo vya mafuta 7 vinne vishakamilika vitatu vipo ongoing kwa maana vibari vishatoka au vinasikiliziwa maana maeneo yapo wazi kwa ujenz
Yaan hapo kutoka kwa Tumbo mpaka darajani ni ndani ya kilomitaa kama 1.5 au 1.7
Lkn pana utitili wa vituo vya mafuta
Ambavyo vinaibuka kama UYOGA
 
Kituo kinajengwa kimebanana na makazi ya mtu kabisa...mpk jirani
Anaona htr,je kituo kikilipuka

Ova
 
Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

"Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya
mafuta nchini," amesema.

=====

Serikali imesitisha utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi Novemba 10, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula.

“Lengo ni kutoa nafasi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta nchini,” amesema.

Aidha, Dk Angeline ameagiza kusitishwa kutolewa kwa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe ya majiji, manispaa, miji na kusitisha ugawaji wa viwanja kiholela unaosababisha taswira za miji kuharibika.

Ametoa mfano wa eneo lililopangwa kuendeleza ujenzi wa maghorofa vibali vifuate mpango.

Source: Mwananchi.
Thread 'Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa' Vituo vya mafuta katikati ya mji na makazi ya watu Dar: Bomu linalosubiri maafa makubwa
 
Lake Oil kila kona ya nchi hii, yaani ni tishio
 
Yaan ilikuwa hadi kero hadi unashangaa
Mfan Ukianza kwa tumbo tandare mpk darajani sinza kuna vituo vya mafuta 7 vinne vishakamilika vitatu vipo ongoing kwa maana vibari vishatoka au vinasikiliziwa maana maeneo yapo wazi kwa ujenz
Yaan hapo kutoka kwa Tumbo mpaka darajani ni ndani ya kilomitaa kama 1.5 au 1.7
Lkn pana utitili wa vituo vya mafuta
Ambavyo vinaibuka kama UYOGA
Njia ya Tandare kuelekea Sinza unaweza waza hao wafanya biashara wana wazimu yaani sehemu hata haistahili unaona kabisa huyu ana teketeza pesa zake hapa hamna biashara yaani kila hatua tatu kituo cha mafuta🤷🏼‍♀️
 
Back
Top Bottom