Serikali yatangaza Amri ya Bei Elekezi za Sukari Tanzania Bara

Serikali yatangaza Amri ya Bei Elekezi za Sukari Tanzania Bara

Watu wameshanunua sukari zao kwa jumla huko wameshapigwa bei, wanazisukuma rejareja hela irudi halafu waambiwe wauze bei ambayo hata walivyonunua jumla hawakuuziwa bei hiyo? Lazima wazifiche ni mwendo wa kuuziwa kwa kujificha kama bangi.
 
Waende kiwandani wawaambie wauze sukari kwa bei elekezi na iwe toshelezi, kwann sukari inapanda bei, mawakala wameweka oda kiwandani lkn bidhaa hakuna, ikipatikana anapigiwa cm wakala mmoja sukali ipo lkn kwa shilingi kadhaa bei sio ile halisi anaongezewa kidogo hata hivyo anapata pungufu ya idadi aliotaka mfano amehitaji tani 60 analetewa tani 40 wakati huo huyu wakala ana wateja zaid ya 20 wanataka sukali, ikifika anaiweka ndani anawapigia wateja sukari imefika lkn kwa bei fulania wale wanaenda kununua hapo inauzwa kwa jumla mtu anachukua mifuko 100 nk huyu nae anakwenda kuwauzi wale wa mfuko moja mwenye kuitaji mifuko kumi kwa kuongoza zaid mpka ikufikie ww , kaa kwa kutulia waende kiwandani wakatatue tatizo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes, hk ndo walitakiwa kufanya kama kweli wako serious, sio kuja na matamko tamko ambayo hakuna utekelezaji,,, yaan wameacha mzizi wanapapatika na matawi
 
Serikali imefikaje JUNE na sisi bado tupo JANUARY???😳😳😳

Au wametumia time machine ndio maana hata signature hawakuweka...?
Screenshot_20240124_090639_Chrome.jpg
 
Ikiadimika serikali inatakiwa iwachukulie hatua wanaoficha sukari.
Hawa watu sio wakuwachekea hata kidogo. Ukiona hadi awamu hii inafikia hatua hii ujue uhuni umezidi.
Haisaidii kitu, serikali iruhusu sukari nyingi kutoka nje kufidia pengo.
 
View attachment 2881106
View attachment 2881107
Kufuatia malalamiko ya Wananchi juu ya kupanda kwa gharama za Sukari, Serikali imetangaza Amri ya Bei Elekezi iliyoanza kutumika Januari 23, 2024 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara kwa lengo la kudhibiti Bei holela za Bidhaa hiyo

Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali, Amri hiyo imesema Mtu yeyote anayeuza Sukari kinyume na Bei Elekezi zilizoainishwa atakuwa ametenda Kosa na akitiwa hatiani atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa katika masharti ya Sheria ya Tasnia ya Sukari

Bei Elekezi za Rejareja kwa Kilo 1 Sukari ziko kama ifuatavyo: Dar, Morogoro, Pwani Tsh. 2,700 - 3,000, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe Tsh. 2,700 -3000, Dodoma, Singida, Tabora Tsh. 2,800 - 3,000, Lindi Mtwara, Ruvuma Tsh. 2,900 - 3,200

Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara Tsh. 2,800 - 3,000, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara Tsh. 2,700 - 3,000 na Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa Tsh. 2,800 - 3,200
Mbona tumeyazoea haya na serikali haikuwahi kushinda, bei ndiyo kwanza zikaendelea kupanda.
 
Back
Top Bottom