JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Uchumi hauendi hivyo, Mambo ya bei elekezi ni Mambo ya Kijima ya miaka 1947!View attachment 2881106
View attachment 2881107
Kufuatia malalamiko ya Wananchi juu ya kupanda kwa gharama za Sukari, Serikali imetangaza Amri ya Bei Elekezi iliyoanza kutumika Januari 23, 2024 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara kwa lengo la kudhibiti Bei holela za Bidhaa hiyo
Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali, Amri hiyo imesema Mtu yeyote anayeuza Sukari kinyume na Bei Elekezi zilizoainishwa atakuwa ametenda Kosa na akitiwa hatiani atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa katika masharti ya Sheria ya Tasnia ya Sukari
Bei Elekezi za Rejareja kwa Kilo 1 Sukari ziko kama ifuatavyo: Dar, Morogoro, Pwani Tsh. 2,700 - 3,000, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe Tsh. 2,700 -3000, Dodoma, Singida, Tabora Tsh. 2,800 - 3,000, Lindi Mtwara, Ruvuma Tsh. 2,900 - 3,200
Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara Tsh. 2,800 - 3,000, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara Tsh. 2,700 - 3,000 na Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa Tsh. 2,800 - 3,200
Bidhaa zinatakiwa ziende kwa nguvu ya soko,demand and supply,
Low demand, high supply, bei zitaporomoka!
High demand, low supply, bei Zita panda tu, high demand, high supply, bei zinakuwa stabble, sio huu upuuzi unaoendelea,
Inawezekana vipi, watu wakaficha bidhaa, ili bei zipande, na serikali IPO, Waziri, katibu mkuu, maofisa ndani ya mkoa, wilaya, watu wa usalama, nk