Serikali yatangaza Amri ya Bei Elekezi za Sukari Tanzania Bara

hao walala hio wanaojifanya kuwatetea hawanywi chai wala kutumia sukari...wangeaca ipande tu...jk aliacha sukari 1600/kg akaichezea jpm sukari lethos retai price haizidi 500tsh/kg watu walikuwa wanaifikisha tunduma kwa tsh 900 akapiga marufukukuingizwa...
 
Ukitaka kujua Tanzania ni rotten shithole country njoo hapa boda ya Mutukula, sukari ya Uganda [emoji1254] [emoji58] best quality inauzwa Tsh 1700 mpaka 2000 wakati low quality ya Kagera sugar tunanunua 4000 mpaka 5000 kwa KG
 
Hii issue mfumo serikali iliotumia kupanga bei elekezi una walakini kwanini wasifuatilie bei kutoka kiwandani wao wameanza na dealer kwanza dealers wenyewe wameachwa tu ila wanaenda kudeal na wafanyabiashara wadogo wasio hata na kosa lolote
 
Hapa serikali inanichekesha Sasa kama sukari ya nje ilikuwa imeshaagizwa tayari na inakuja kulikuwa na haja gan ya kujidai kwamba wanajali wananchi na kufatilia bei ya sukari na kukamata wafanyabiashara Kwa show off kwenye TV sukari ya nje ikishakuja na bei ndogo yenyewe tu itasababisha stability of price ni simple economy sukari ilipanda Kwa sababu ya scarce kwenye market...
Wameingiza wafanyabiashara wengi kwenye hasara Kwasababu umenunua sukari Kwa bei juu Leo hii uuze bei chini Kwa agizo la serikali...wamesahau hao ndo walipa Kodi wao Kwa kiwango kikubwa
 
Kuweka bei elekezi ni kama danganya toto. Factor kubwa hapa ni supply and demand.
Tena ni simple economics tu serikali ina maana Haina wataalamu wa uchumi kujua Hili suala linaenda naturally tu..
 
Tunawapongeza kwa hili la sukari wamelichukulia hatua za haraka hebu waulize hawawezi kutuagizia na umeme huko?
 
tunaweza kutofautiana Kwa mawazo ila tukabaki na ukwel halisi kuwa mtu pekee alieweza kudhibiti mfumko wa Bei ni JPM tu, na hakuwa na mchezo na alikuwa na Nia, pamoja na malengo,

wengine huku wanatuchezesha Ngoma ya mdundiko tu, tuendelee kula mtori nyama tutazikuta chini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutoa amri ya bei elekezi ya sukari ilihali sukari haipatikani sio solution Cha msingi serikali ihakikishe sukari inapatikana ya kutosha
 
Nilipo bei ni 4000+

Tofauti na hapo kakoroge chumvi itumike kama mbadala wa sukari
 
Nimetoka kununua muda, huu mitaa, ya Ukonga Dsm, kilo Moja ya sukari ni 4500/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…