Serikali yatangaza bei ya kikomo ya Sukari; ipo kati ya Tsh. 2,600 na Tsh. 3,200 kwa kilo kutegemea na Mkoa

Serikali yatangaza bei ya kikomo ya Sukari; ipo kati ya Tsh. 2,600 na Tsh. 3,200 kwa kilo kutegemea na Mkoa

Serikali imetangaza bei ya ukomo ya Sukari kwa rejareja katika Mikoa yote nchini, ambapo kwa Dar es Salaam itauzwa kwa Shilingi 2,600 kwa Kg 1, Mbeya 3,000, Mwanza, Dodoma na Shinyanga 2,900, Kigoma 3,200, Arusha na Kilimanjaro ni 2,700, Kagera na Mara ni 3,000.

Aidha kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara, Sukari itauzwa kwa Sh.2,800, Rukwa, Katavi, Ruvuma itauzwa kwa Sh 3,200. Njombe, Geita, Tabora, Singida, Iringa na Simiyu itauzwa kwa Sh.2900 na kwa Manyara, Tanga, Pwani na Morogoro itauzwa kwa Sh 2,700 na Songwe ni Sh.3,000.

Mbona hawakutaja Chato watanunua kwa shilingi ngapi?
 
Nikikutukana nawe utanirudishia wakati sijasema baya,mwisho nijiumize roho.Bora ninyamaze!!
Hii ndiyo serikali ya wanyonge, inayowajali wanyonge na kufanya kazi kwa ajili ya wanyonge kama wewe sio mnyonge kamwe huwezi kuelewa namna gani serikali yetu sikivu inavyotujali wanyonge.

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
Kuna mambo yamezingatiwa katika upangaji bei. Ikiwemo umbali na eneo sukari inapozalishwa,maana gharama za usafiri zinatofautiana toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Mkuu kwani viwanda vikizalisha bei zinatofautiana mkoa hadi mloa?
 
Huku niliko (kusini), bei iko vilevile au imeongezeka. ilikuwa 3,600/= kabla ya agizo lakini sasa ni 3,800-4,000/=. huko uliko hali ikoje?

Nani yuko karibu huko afikishe ujumbe kuhusu kiburi hiki cha hawa watu?!! mi niko mbali huku sitowahi kwa wakati!
 
Huku kilo ni 3400/=

Agizo lilielekeza kilo iuzwe kwa 2700/=

Tuendelee kuchukua tahadhari Corona ni hatari sana
 
Hivi ni kwa nini Wafanyabiashara wa sukari wanaichezea Serikali?. Wamepewa bei elekezi lakini hawataki kufuata.
 
nawashauri hiyo bodi ya sukari watoe namba za simu kwa wananchi ili wakiuziwa bei tofauti wapige simu.... 😎 😎
 
Back
Top Bottom