Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kishoka bwana....maneno miiingi, halafu unaongea kama upo kwenye mars!! mzee tunaongelea bongo, ambako unemployment ipo kwenye roof!! hizo McD zipo ngapi? kuwa utingo unafikiri ni virahisi?
kuna points nzuri umetoa, lakini kiujumla una simplify hii issue kupita kiasi.....hivi unajua bei ya scientific calculator pale bongo? je katika boom na mikopo mingine wanaweka na mahesabu ya calculator?.....wewe unaongelea vitu ideal wakati sie tunaongelea vitu real! baadhi ya proposals zako ni totally impossible ktk tanzania ya leo.
vijisenti vya Chenge pale Jersey ni nuff, kununua calculators na kufix elevators zote pale UDSM......hivi ni chepi hasa ambacho ni kigumu?
acha kuwajaza wafunzi ujinga, wewe ndio unachangia wale wanafunzi kufukuzwa chuo, ungewapa ushauri mzuri wenye kujenga. Na watakukumbuka maisha yao yote kama ikitokea wakakutwa na hatua kwa kusoma uliyokuwa unayaandika hapa kuwasisitiza waendelee kugoma.
nina haraka si unajua hapa internet cafe na muda unaenda. Je unajua kuwa asilimia zaidi ya 50 ya watanzania hawana access ya umeme, na asilimia zaidi ya hiyo haina maji unayoyaita tape water? kitu gani maalum kwa hao wanafunzi walichonacho hadi kusema kuwa wenyewe ndio wana haki zaidi ya kuwa na maji ya bomba kuliko wantanzania wengine wowote?
hao wanfunzi wana kila sababu ya kupigania kwa haki za wazazi wao ambao wengi wao hawajasoma. Ninachouliza kama kweli hao wanafunzi wanauchungu na ufisadi kwa nini wanakuwa selfish na kupigania hayo wanayoyaona ni shida hapo chuo (ambapo hawatakuwa hapo kwa zaidi ya miaka minne) na kwamba watakutana nayo kwa kipindi kilichobaki cha maisha yao huko mitaani. Kwa nini wasigome kwa kuishinikiza serikali kuboresha miundo mbinu yote vijijini badala ya kulipa kampuni hewa mabilioni ya pesa?
Soma vizuri utaiona.
Wewe unaonekana unapuuzia yote waliyofanya viongozi wa wanafunzi pale walipomshinikiza Kikwete kuwashughulikia mafisadi na vile walivyoshiriki kwenye kongamano la siku ya vijana na wakatoa matamko mbalimbali kuitaka serikali kushughulikia maswala ya watanzania.
Take time kuona kazi nzuri waliyofanya hawa ambao muuaji, dikiteta na fisadi Mukandala anawaita wavuta bangi.
ninakupinga kwa sababu tatu;
1. kusema kuwa amekulia mlimani ni sentensi tata ambayo wewe kama mchangiaji ulipaswa kuona kama likuwa mtoto wa mkazi ya maeneo hayo, whether ni mfanyakazi or the opposite, na alikuwa anaenda kusoma shule za nje kama mlimani primary school, hata shule za secondary kama makongo ila mienendo mizima ya wanachuo alikuwa anaiona.
2. pili inawezekana amesoma hata mlimani, UDSM, na kipimo cha elimu sio Lugha kama wewe unavyotaka tuamini
3. hata hivyo, inawezekana ni typing error, maana sijaona tatizo kama vile grammar n.k.
kwa hiyo hukupaswa kutoka kwenye mada kama kweli wewe ni makini na kuanza kudeal na vitu irrelevant ambavyo havina uhusiano na hili.
ningekuwa wewe ningemuomba radhi, ila ninajua huwezi maana sio mara yako ya kwanza kutumia alibacrum.
pole.
wako pale UDSM kulitumikia taifa,the same way JWTZ wanavyolitumikia TAIFA.hao wanafunzi wa UDSM na vyuo vingine ndio future ya tanzania if u realy know what i mean.sorry but thats the real truth.they not only deserve attention but they deserve care.
and since they aren't getting any..,look where our country is heading.
Wala usifanye mimi kuwa part ya ufisadi na udikiteta aliofanya Mukandala. Kumbuka kuwa mimi nilikuwa kimya nikipambana na kina Chenge kabla huyo muuaji mukandala hajaingilia uchaguzi huru wa wanafunzi.
Sihusiki na suala la kufukuzwa wanafunzi na wala usitafute mtu kwa kulaumu kwa vitendo vya uonevu na ujangili ambavyo Mukandala amefanya dhidi ya mama mjamzito na wanafunzi wengine wasio na hatia
Mwafrika wa kike sio mwananchi?Falsafa za CCM kuwa wananchi ni wana CCM peke yao?Shivji nafikiri pia alikuwa akimaanisha "jambo forums"Taifa ni la wote..we all have high stakes in the well being of our country's educational institutions..for its the core point of democracy,hope leadership and progressive minds that if propely utilized(instead of always opposing)..can yield to a more prosperous Nation.UTASUBIRI NINI WAKATI WATU TAYARI WAMEFUNGIWA KWENYE LIBRARY, MADARASANI NA HATA KUPIGWA ETI KWA SABABU HAWAKUBALIANI NAO?
TANZANIA DAIMA YA LEO IMEMKWOTI SHIVJI AKIWASHAURI WANAFUNZI KUWA INABIDI KUJIFUNZA KUGOMA KWA MAMBO AMBAYO WATAPATA SUPPORT KUTOKA KWA WANANCHI.( nadhani alitaka kusema sio kupata support kutoka kwa akina Mwafrika wa kike maana watawapoteza. emphasis is mine)
acha kuwawajaza jazba vijana wa chuo, waelekeza, watu kama nyie ni hatari sana kwa jamii kama mkiendelea na mwelekeo huu. Nilikusifu sana katika kuupigia kelele ufisadi na sio siri katika watu walionivutia nikajiunga na huu ukumbi ni wewe. Lakini nimesikitishwa na kauli zako katika hili.
Najua hapa lazima utanitukana au kunipiga kibao lakini habari ndio hiyo. Umeandika ushauri ambao wanafunzi waliouchukua na kuufanyia kazi watajuta katika maisha yao kama ikitokea wafukuzwa chuo, au wakatakiwa kudahiliwa upya.
BTW mie sio mtetezi wa mafisadi kwani najua mwenyewe ni jinsi gani mafisadi wameniathiri na hali yangu ya maisha naijua mwenyewe. Siwapendi na siwataki mafisadi.
Kwa nini hao vijana wa chuo huwa hawagomi bunge lisipofanyia kazi matatizo yao?
lakini ninasikia wameresume masomoni.
je wamefuata ushauri wa nani?
Idealism? si tunamlaumu Nyerere kwa kushindwa kufanya vitu viwe practical? sasa nafasi tunayo tunatoa sababu eti "hali halisi"!
We need to be creative bwana to become successful. We have been a dependent nation, kiasi kuwa tumekuwa wavivu wa kuwa wabunifu.
Tayari unalalamika kuwa Utingo si kazi rahisi, sasa iweje iwe kazi rahisi ya Utingo imshinde msomi? Hivi hawa jamaa wasomi wakienda na kuanza kuthamini Ubamedi na Utingo si watajifunza mambo mengi tuu kama hawatapata kazi za maofisini au viwandani?
Lets say siku yako darasani ni saa 1 asubuhi mpaka saa 8 mchana, halafu huna lolote zaidi ya kubukua na homework. Ukienda kuwa konda/utingo pale Mwenge kwa masaa manne, si pumziko tosha huku ukijifunza hata hiyo kazi na kujua biashara ya vipanya inafanywaje na mapato yake yanaweza kuwa makubwa kiasi gani (mind you kuanzia saa 9 mchana mpaka saa 1 usiku ni rush hour Dar)?
Au kama hilo halitoshi, si kuna tenda kila siku za kusafisha maofisi, mazingira na vitu vingine ambavyo vinahitaji mtaji mdogo wa pesa na zaidi ni nguvu kazi? Sasa kama RevYNIM wakianzisha kakamppuni kao ka kusafisha ofisi na madarasa na kuwasilisha tenda kwa UDSM au ESRF na maofisi mengine, si hapo tunajifunza biashara na kupata pesa za kukidhi mahitaji?
Labda mwisho niseme hivi, niko Uhandisi, darasa limekweisha nakwenda pale zamani palikuwa panaitwa IPI, naanza kuchora mashine yangu ya kusukuma maji kwa kubanjua mashine mbovu na kutumia vipuri. Sasa kama nimeweka mawazo chanya na nguvu za ubunifu si nitapata kuelimika kwa kujua ninachosoma kwa nadharia na kukifanya kwa vitendo an si kusubiri chuo kikifungwa niende field work?
"Akili tunazo, tunazikalia"!
JAMANI TUWE WAKWELI KATIKA HILI JAMBO, TUSIWE WACHOCHEZI WA MIGOMO BALI TUWAELEKEZE HAO WANAFUNZI NJIA MUAFAKA YA KUTATUA HILI TATIZO, JAZBA HAIJENGI MARA NYINGI HUBOMOA.
IDUMU VITA DHIDI YA MAFISADI (pia mafisadi wa kifikra)
kishoka bwana....maneno miiingi, halafu unaongea kama upo kwenye mars!! mzee tunaongelea bongo, ambako unemployment ipo kwenye roof!! hizo McD zipo ngapi? kuwa utingo unafikiri ni virahisi?
kuna points nzuri umetoa, lakini kiujumla una simplify hii issue kupita kiasi.....hivi unajua bei ya scientific calculator pale bongo? je katika boom na mikopo mingine wanaweka na mahesabu ya calculator?.....wewe unaongelea vitu ideal wakati sie tunaongelea vitu real! baadhi ya proposals zako ni totally impossible ktk tanzania ya leo.
vijisenti vya Chenge pale Jersey ni nuff, kununua calculators na kufix elevators zote pale UDSM......hivi ni chepi hasa ambacho ni kigumu?
na pia wewe unapuuzia yote waliofanya viongozi wa wanafunzi pale waliposhnikiza wanafunzi wenzao kupinga mgomo kwa kutamka kuwa ni mgomo batili. si ndio hao hao unaowageuka?
So far naona aliyeleta FFU kupiga mama mjamzito na wanafunzi wengine wasio na hatia baada ya kuwa amengilia uhuru wao wa kuchagua viongozi wao ndio ameleta jazba.
kama wenyewe tu ndio wanataka care, wananchi wengine wenye maisha duni zaidi ya hao wanafunzi hao chuo inakuwaje. Hao wanafunzi wamepandishiwa kiwango cha posho kwa siku, watakuwa wanalipwa 10,000 kwa siku kwa wiki 17 za semista. Je ana hali gani mwananchi wa kijijini ambaye pato lake la mwaka mzima halizi 400,000. Kumbukeni watanzania walio wengi wana kipato cha chini ya dola moja kwa siku.