Bibianna
JF-Expert Member
- Jun 6, 2025
- 474
- 163
Katika kipindi cha 2020 hadi 2025, Mkoa wa Tanga umeongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 325 hadi 417 (ongezeko la vituo 92), ambapo zahanati zimeongezeka kwa 74 (kutoka 287 hadi 361), vituo vya afya kwa 15 (kutoka 31 hadi 46), na hospitali kwa 3 (kutoka 7 hadi 10). Kwa upande wa rasilimali, mkoa umepokea shilingi 19,751,050,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba muhimu kama CT Scan, X-ray, vitanda na ambulance.
Aidha, mkoa umepokea shilingi 3,600,000,000.00 kwa ajili ya magari 12 ya wagonjwa, shilingi 17,575,497,902.00 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa hospitali 10 katika halmashauri mbalimbali, na shilingi 1,000,000,000.00 kwa ajili ya majengo 3 ya dharura (EMD). Pia, shilingi 1,137,000,000.00 zilitumika kujenga nyumba 19 za watumishi wa afya, shilingi 250,000,000.00 kwa ajili ya ICU ya Hospitali ya Pangani, na shilingi 4,463,960,376.00 kwa miundombinu ya maji, vyoo, kunawa mikono, na vichomea taka katika vituo 71.
Kwa ujumla, mkoa wa Tanga umetumia shilingi 47,777,508,278.00 katika kuboresha huduma za afya. Vilevile, kumekuwa na ongezeko la watumishi kutoka 3,185 hadi 4,380 kufikia Mei 2025, ambapo watumishi wapya 926 wameajiriwa na ongezeko la jumla limefikia watumishi 1,195.