Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu Tanzania kupanga kununua umeme nchini Ethiopia

Yaani kusafirisha kutoka dar kwenda arusha ni gharama kuliko kutoka ethiopia kwenda arusha via Kenya.
Akili yangu haifanyi kazi sawasawa jamani
 
Hawa Serikali wasitufanye wote hatuujui umeme, unasingiziaje umbali na upotevu wa umeme au gharama, why gharama zetu siwe kubwa
 
Sasa hivi wanasema wanautolea Kenya badala ya kupitia Kenya
Hoja ni kwamba, unakozalishwa ni Ethiopia ina maana humo njiani haupotei?

Kama tunahesabia umbali kutoka Kenya, basi pia hata huu wa rufiji tutahesabia umbali pale mkoa jirani uliounganishwa na grid ya taifa.

Kwa namna nyingie, humu bongo, kila mkoa huwa unapokea umeme grid ya taifa na mkoa mwingine unachukulia pale kama ambavyo wao watachukulia Kenya.

Wakija na hoja ya umbali kunakozalishwa umeme, Ethiopia ni mbali kuliko rufiji.
 
Sasa hivi wanasema wanautolea Kenya badala ya kupitia Kenya
Kenya ....40% wanasambaza walionunua Ethiopia uko 200km from boarder yetu....cost zao kuleta boarder....beiaoiko cheap zaidii yetu......kufikisha huko ftom rufiji sio chini miaka 6...plus cost zoote fidia etc....bado kupeleka Mwanza Ngara...bado Mveya Rukwa ( wanatumia zambia).....hii sio siasa we need pesa na kipaumbelee ....kumbuka bado maji tu rahisi hatuwezi kufikisha......weeee sikia tuuu.......hapo hakuna siasaa
 
Hivi ufafanuzi maana yake huwa nini. Yani yawezekana waskilizaji hawakulewa lugha ilyotumika, walikuwa wamelewa, au mzungumzaji hakuwa sawa kiakili na kiafya wakati anaongea. Msaada tafadhali maana mimi huwa napata shida sana.

Huu msamiati wa ufafanuzo mbona miaka ya nyuma haukuwepo au ndo kukua kwa lugha.
 
huu ndo ufafanuzi? au kuna mwngine unakuja?...😳😳🙌🚮❗
 
Sasa hivi wanasema wanautolea Kenya badala ya kupitia Kenya
Kwamba wao huko wanavyousafirisha hauvuji kutoka ethiopia to kenya ila kutoka rufiji to tanga ndio unamwagika kama sio kuvuja...
Aisee ccm ni janga, Mungu tuepushe nalo.
images (2).jpeg
 
Iko hivi umeme kutoka vyanzo vikuu vya umeme wa uhakika Rufiji na mikoa mingine ukitaka kuusafirisha kwenda mikoa ya kaskazini unakuwa unazungumzia mradi wa wastani wa 800km ~900Km
Je, hakuna miradi ya umbali huo katika nchi zingine za Afrika? Vipi, imefeli au bado inaendelea?
 
Ni kweli nchi ina umeme wa kutosha lakini haina maana kwasababu umeme upo wa kutosha basi unaweza kuupeleka popote pasipo kufanya tathmini!

Gharama za kusafirisha umeme kwa umbali huo ni kubwa mno ukilinganisha na kuuchukulia hapo kenya .
Wanaposema umeme wa Ethiopia haina maana uko huko Ethiopia! Ni uko hapo jilani kenya wastani wa km 250km~300km tu

Hivyo ukichukulia gharama za kuusafirisha umeme kwa wastani 50mil kwa kila span moja ( nguzo moja hadi nyingine) hapa tutazungumzia wastani wa span elf 8000 hadi 9000 endapo utaamua kuutoa mikoa ya rufiji!

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mbali na gharama hizo mradi mkubwa kama huo unahitaji kulipa watu fidia na kuchepusha miundombinu itayoingiliana hapo katikati ya mradi!

Miradi ya mabomba ya mafuta yaliyopita ardhini yatalazimisha kubadilisha span badala ya kupitisha umeme juu ya bomba ushushwe chini (underground) ili kuepusha muingiliano wa frequency za umeme na zile za bomba la mafuta! Yote hayo yanapaisha gharama za mradi!

Muda wa kuujenga mradi mkubwa kama huo unaweza kuchukua miaka siyo chini ya mitano!

Upotevu wa umeme hapo katikati (power losses) kwa umbali huo ni Mkubwa ukilinganisha na faida utayovuna ukiuufikisha mikoa husika ya kaskazini!

Yote tisa hata kama umeme upo lakini kama jilani ana bei rahisi kuliko za nchi yetu kwanini kujichosha ilihali kwa jilani anao umeme karibu na ni bei nafuu zaidi?

Ambao hawajaelewa naomba kutoa mfano huu!
Mkuu ni vyema tu kukaa kimya ulinde heshima yako.
 
Nipe umeme nikupe umeme. Nipe nikupe. Niuzie na ninunue.
 
Mbali ni Stiglers. Ethiopia ni karibu kabisa. Kwani hamjui kuwa kutoka Dodoma mpaka Arusha ni mbali kuliko Addis Ababa mpaka Arusha?
Tulia basi uelewe umeme mzalishaji ni ethiopia kenya ni transit sisi tunaupokea kutokea kenya kwenye gridi yao ya kenya tunalipa transit fee shirika la kenya na tunawalipa ethiopia kununua umeme wao ambapo mikoa ya kaskazini inapakana na kenya gharama inakuwa ndugu ya kusafirisha umeme kuliko ule tunasambaza sisi
 
Ni kweli nchi ina umeme wa kutosha lakini haina maana kwasababu umeme upo wa kutosha basi unaweza kuupeleka popote pasipo kufanya tathmini!

Iko hivi umeme kutoka vyanzo vikuu vya umeme wa uhakika Rufiji na mikoa mingine ukitaka kuusafirisha kwenda mikoa ya kaskazini unakuwa unazungumzia mradi wa wastani wa 800km ~900Km

Gharama za kusafirisha umeme kwa umbali huo ni kubwa mno ukilinganisha na kuuchukulia hapo kenya .
Wanaposema umeme wa Ethiopia haina maana uko huko Ethiopia! Ni uko hapo jilani kenya wastani wa km 250km~300km tu

Hivyo ukichukulia gharama za kuusafirisha umeme kwa wastani 50mil kwa kila span moja ( nguzo moja hadi nyingine) hapa tutazungumzia wastani wa span elf 8000 hadi 9000 endapo utaamua kuutoa mikoa ya rufiji!

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mbali na gharama hizo mradi mkubwa kama huo unahitaji kulipa watu fidia na kuchepusha miundombinu itayoingiliana hapo katikati ya mradi!

Miradi ya mabomba ya mafuta yaliyopita ardhini yatalazimisha kubadilisha span badala ya kupitisha umeme juu ya bomba ushushwe chini (underground) ili kuepusha muingiliano wa frequency za umeme na zile za bomba la mafuta! Yote hayo yanapaisha gharama za mradi!

Muda wa kuujenga mradi mkubwa kama huo unaweza kuchukua miaka siyo chini ya mitano!

Upotevu wa umeme hapo katikati (power losses) kwa umbali huo ni Mkubwa ukilinganisha na faida utayovuna ukiuufikisha mikoa husika ya kaskazini!

Yote tisa hata kama umeme upo lakini kama jilani ana bei rahisi kuliko za nchi yetu kwanini kujichosha ilihali kwa jilani anao umeme karibu na ni bei nafuu zaidi?

Ambao hawajaelewa naomba kutoa mfano huu!
Mkuu, umejaribu kufafanua kiunaga ubaga, lakini umejazia nyama sanaa!
 
Je, hakuna miradi ya umbali huo katika nchi zingine za Afrika? Vipi, imefeli au bado inaendelea?
Kumbuka tuna vipaumvele vingi mkuu miradi ipo fund hakuna......ingia website Tanesco angalia procurement za kila mwaka za expansion grid taifa utaona.....mkuu fund...na vipaumbele mambo mengi pesa....nehiii....
 
Back
Top Bottom