Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Wakuu pesa tuliyotumia kama taifa kusomesha wasomi imeleta laana kwa taifa. Umbali wa kutoa umeme maeneo ya kusini imeonekena ni kazi Bure kwani katika hatua ya kusafirisha umeme kutoka Mtera ama Bwawa na la Nyerere kuupeleka mikoa ya kasikazini umeme unapotea sana. Sasa sijajua labda kwa sababu ya friction ama heating effects ama drift velocity ama kitu Gani kinafanya voltages zipotee hapo njiani. Nakubali Kuna factors zinapelekea umeme unaozalishwa na unaofika site Huwa unatofautiana lakini si kwa kiwango Cha kuamua kununua umeme kutoka Ethiopia kilomita zaidi ya Elfu 2 na kuacha kuchukua umeme uliopo kilometa 600. Haya ni maajabu. Lazima tuelewe watanzania tuna maisha magumu Sana na haya mambo yanatuumiza sana.
Taarifa yenyewe hii hapa ni ndefu kinyama...
Serikali imetolea ufafanuzi kauli iliyotolewa na Rais Samia leo kwamba Serikali itanunua umeme maalum kwa ajili ya Mikoa ya Kanda Kaskazini ili umeme usikatikekatike ambapo imesema umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unazalishwa kutoka ukanda wa Kusini Mashariki na hivyo kulazimika kusafirishwa umbali mrefu kwenda maeneo mbalimbali nchini hali inayosababisha upotevu mkubwa wa umeme.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali leo March 09,2025 imesema “Kwa Kanda ya Kaskazini upotevu wa umeme unaosafirishwa umekuwa ukisababisha hasara ya zaidi ya Tsh. bilioni 32 kwa mwaka, kutokana na upotevu huo na usafirishaji mrefu wa umeme, Kanda ya Kaskazini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali ambayo inawaathiri Wananchi”
“Ununuzi wa umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya utasaidia kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuokoa upotevu mkubwa wa umeme unaokwenda katika kanda hiyo, gharama za umeme unaonunuliwa kutoka Ethiopia ni nafuu kutokana na Tanzania kuwa mwanachama wa Gridi ya Umeme ya Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika ambapo nchi zina makubaliano ya kuuziana umeme kwa gharama nafuu ambayo inalingana ama ni chini ya gharama za uzalishaji umeme zilizopo sasa hapa Tanzania kwa baadhi ya vyanzo vyetu”
“Utaratibu wa Tanzania kununua umeme kutoka nchi jirani umekuwa ukifanyika tangu miaka mingi hususani Mikoa ya pembezoni ambayo ni Rukwa (kutoka Zambia) Kagera (kutoka Uganda) na
Tanga (kutoka Kenya), lengo kuu la kununua umeme kwa ajili ya maeneo ya pembezoni mwa nchi ni kuimarisha Gridi ya Taifa na kuiwezesha nchi kuwa na njia mbadala ya kupata nishati ya umeme pale kunapotokea changamoto katika Gridi ya Taifa.