Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu Tanzania kupanga kununua umeme nchini Ethiopia

Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu Tanzania kupanga kununua umeme nchini Ethiopia

Ufafanuzi
Kwanini Tanzania inapanga kununua umeme
kutoka nje ya nchi kwa ajili ya Kanda ya
Kaskazini.

1. Umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unazalishwa kutoka ukanda wa
Kusini Mashariki na hivyo kulazimika kusafirishwa umbali mrefu
kwenda maeneo mbalimbali nchini hali inayosababisha upotevu
mkubwa wa umeme.
Hivi kutoka Morogoro hadi Kilimanjaro na kutoka Ethiopia hadi Kilimanjaro wapi mbali?
2. Kwa Kanda ya Kaskazini upotevu wa umeme unaosafirishwa ume-
kuwa ukisababisha hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 kwa mwaka.
Kwani tunaponunua umeme kutoka nje ya nchi hatuingii gharama kubwa? Na je suala hili na hilo hapo juu si kitu kimoja tu =UPOTEVU WA UMEME/GHARAMA KUBWA?
3. Kutokana na upotevu huo na usafirishaji mrefu wa umeme, Kanda
ya Kaskazini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya kukatika
kwa umeme mara kwa mara hali ambayo inawaathiri wananchi.
Umeme kukatika hovyo ni tatizo hata Dar es Salaam pale Ubungo na Kinyerezi unapozaliswa umeme wa gesi. Ni tatizo hata kule Morogoro Kidatu na Mtera Dodoma.
4. Ununuzi wa umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya utasaidia kuon-
doa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuokoa
upotevu mkubwa wa umeme unaokwenda katika kanda hiyo.
Si hayo hayo tayari mmeyazungumzia number 3, 2 na 1 hapo juu???
Idara ya Habari - MAELEZO na
Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali
Maelezo
www.maelezo.go.tz

Share

Export

Rewrite
 
OOctober 2025
Kuwanyima Kura Hawa Wapuuzi
umeme Wetu Nchini Kwetu Wataalam Tunao Wanashindwaje Kuthibiti Huo Upotevu
Kutoka Pwani Yaañi Liliko Bwawa Mpaka Tanga Ambako Ndiyo Mikoa Ya Kaskazini Iwe Mbali Namna Gani ?

Halafu Ethiopia via Kenya Iwe Ndiyo Karibu

Upuuzi Mtupu

watu wanakabidhi bandari kwa foreigners ambapo kwa nchi nyingi bandari ni national security, lkn tanzagiza wameshindwa kuendesha ije kuwa umeme ?
 
Hii inaitwa hiishi mpaka iishe tena! Ufafanuzi bado unahitaji ufafanuzi, sasa sijui ufafanuzi wa awamu ya pili utakuwaje huu ulikuwa wa maandishi! Labda ujao uwe kwa mahojiano. Aidha, tunayo-pool of Electrical Engineers hapa nchini tena wengine ni PhD holders wabobevu kwenye tafiti. Si kungefanyika project ya uvumbuzi kukabiliana na upotevu mkubwa huo wa umeme angalau upotevu ufikie asilimia 0.0005 ya upotevu wa sasa?
Nimejaribu kuwaza tuu! Au kama vipi tuwaite marafiki zetu wa damu wachina tuwape mchongo huo. Tuone show itakavyokuwa hapo!
Usiku mwema aisee nipo kwenye majonzi, nimepatwa msiba bado hatujazika ila hili nalo linanifanya nigawanye majonzi kidogo ya msiba nilionao.
 
HII NCHI INASIKITISHA SANA, WANAOUNGA MKONO CCM LAZIMA
FB_IMG_1733095840848.jpg
 
Hii inaitwa hiishi mpaka iishe tena! Ufafanuzi bado unahitaji ufafanuzi, sasa sijui ufafanuzi wa awamu ya pili utakuwaje huu ulikuwa wa maandishi! Labda ujao uwe kwa mahojiano.
Wataukana huu UFAFANUZI watakuja na Ufafanuzi mwingine ambao hatutatakiwa kuuhoji
 
hapo!
Usiku mwema aisee nipo kwenye majonzi, nimepatwa msiba bado hatujazika ila hili nalo linanifanya nigawanye majonzi kidogo ya msiba nilionao.
Pole sana Ndugu yangu, tuombeane Tu uzima , hilo Tu ndio muhimu sana
 
Dah nimesikitika sana na uongo wa Greyson....

kwamba kusafirisha 100MW, almost 80MW zinapotea njiani unaofika ni 20MW.

Duh hiv hii ni power system ya namna gani hapa nchini, kwa umbali gani huo?...Aise Hii inchi inatuona mazuzu sana.
 
Vijana wa UVCCM Kesho watatoa tamko kumuunga Mkono Mwenyekiti wao kuamua KUNUNUA UMEME kutoka Ethiopia ambako ni Karibu Sana ukilinganisha na Kidatu, Nyumba ya Mungu au Pangani hydro powers
 
Vijana wa UVCCM Kesho watatoa tamko kumuunga Mkono Mwenyekiti wao kuamua KUNUNUA UMEME kutoka Ethiopia ambako ni Karibu Sana ukilinganisha na Kidatu, Nyumba ya Mungu au Pangani hydro powers
MKuu aise yan kwa hili serikali imejivua nguo ni heri wangetuliza kichwa waje na ufafanuzi ulioshiba, technicaly na sio politicaly....Hakuna kitu cha namna hiyo NEVER.
 
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu kauli ya Rais Samia kwamba itanunua umeme maalum kwa ajili ya Mikoa ya Kanda Kaskazini ili kupunguza changamoto ya umeme kukatikakatika. Taarifa zinaeleza kuwa umeme wa sasa katika Gridi ya Taifa unatoka Kusini Mashariki mwa nchi, lakini kwa sababu ya umbali wa kusafirishwa, kuna upotevu mkubwa unaofikia hasara ya Tsh. bilioni 32 kwa mwaka.
20250309_220513.jpg

Kupitia mpango huu, Tanzania itanunua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya kwa gharama nafuu. Serikali inasema kuwa hii ni njia mbadala na salama kwa kuimarisha upatikanaji wa umeme, kama ilivyofanyika kwenye mikoa ya Rukwa, Kagera, na Tanga kwa miaka mingi.

Wadau, mnaonaje uamuzi huu wa kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya? Je, ni suluhisho la kudumu au tunapaswa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa ndani?
 
Ufafanuzi

Kwanini Tanzania inapanga kununua umeme kutoka nje ya nchi kwa ajili ya Kanda ya Kaskazini.

1. Umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unazalishwa kutoka ukanda wa Kusini Mashariki na hivyo kulazimika kusafirishwa umbali mrefu kwenda maeneo mbalimbali nchini hali inayosababisha upotevu mkubwa wa umeme.

2. Kwa Kanda ya Kaskazini upotevu wa umeme unaosafirishwa umekuwa ukisababisha hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 kwa mwaka.

3. Kutokana na upotevu huo na usafirishaji mrefu wa umeme, Kanda ya Kaskazini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali ambayo inawaathiri wananchi.

4. Ununuzi wa umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya utasaidia kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuokoa upotevu mkubwa wa umeme unaoelekezwa katika kanda hiyo.

5. Aidha, gharama za umeme unaonunuliwa kutoka Ethiopia ni nafuu kutokana na Tanzania kuwa mwanachama wa Gridi ya Umeme ya Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika ambapo nchi zina makubaliano ya kuuziana umeme kwa gharama nafuu ambayo ina lingana ama ni chini ya gharama za uzalishaji umeme zilizopo sasa hapa Tanzania kwa baadhi ya vyanzo vyetu.

6. Utaratibu wa Tanzania kununua umeme kutoka nchi jirani umekuwa ukifanyika tangu miaka mingi hususani Mikoa ya pembezoni ambayo ni Rukwa (kutoka Zambia), Kagera (kutoka Uganda), na Tanga (kutoka Kenya).

Lengo kuu la kununua umeme kwa ajili ya maeneo ya pembezoni mwa nchi ni kuimarisha Gridi ya Taifa na kuiwezesha nchi kuwa na njia mbadala ya kupata nishati ya umeme pale kunapotokea changamoto katika Gridi ya Taifa. Halikadhalika Tanzania inao mpango wa kuuza umeme katika nchi majirani zetu kupitia mpango wa soko la pamoja la umeme ama kupitia gridi ambazo ni wanachama.

Mojawapo ya makubaliano ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano wa Nishati uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam ni kuuziana umeme kati ya nchi na nchi kupitia kuunganisha kwa gridi za nchi hizo.

Cc: Nipashe
1741547264853.jpg
1741547267312.jpg
 
Ethiopia to Arusha is easy...ni karibu na gharama ni nafuu kuliko kusafirisha kutoka sehemu yoyote ile Tz. Umeme wetu unapotea mno unapoelekea Kaskazini
Pale Singida upo upepo mkali sana. Kule ulaya Kuna nchi wanatumia umeme wao waliozalisha kwa upepo
 
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu kauli ya Rais Samia kwamba itanunua umeme maalum kwa ajili ya Mikoa ya Kanda Kaskazini ili kupunguza changamoto ya umeme kukatikakatika. Taarifa zinaeleza kuwa umeme wa sasa katika Gridi ya Taifa unatoka Kusini Mashariki mwa nchi, lakini kwa sababu ya umbali wa kusafirishwa, kuna upotevu mkubwa unaofikia hasara ya Tsh. bilioni 32 kwa mwaka.
View attachment 3265012
Kupitia mpango huu, Tanzania itanunua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya kwa gharama nafuu. Serikali inasema kuwa hii ni njia mbadala na salama kwa kuimarisha upatikanaji wa umeme, kama ilivyofanyika kwenye mikoa ya Rukwa, Kagera, na Tanga kwa miaka mingi.

Wadau, mnaonaje uamuzi huu wa kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya? Je, ni suluhisho la kudumu au tunapaswa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa ndani?
Mngesema umeme taysri uko Kenya km 200 kutoka mpakani na Tanzania ...guarama kujenga hizo njia umeme mkubwa rahisi kulingana kujenga na fidia kutoka rufiji to kaskazini 700km hivi.....miaka 5 inatakiwa...plus cost kusafirishaaaa.......tofauti Kenya watajenga wao wakuletee mpakani....
 
Sii walisema tutajitosheleza kwa umeme, na ata kuuza huo umeme..! Acha wanunue uenda alijakamilka bado!
Screenshot_20250304-172445.png
 
Back
Top Bottom