Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Ule mkataba ulikuwa unaleta Dron hapo sokon ingefanyaje kazi? Lakini ata hivo huwezi kufanya mipango ya kusaini mkono wa takriban Trilion 1 huku baraza la waziri halijui chochote
Kwamba hiyo Trilion 1 ilikua ya kuleta drone tu hakuna vifaa vingine?
 
Hivi ile migari miingi ya washa washa waliyonunua wakati wa uchaguzi mkuu 2015 yanafanya kazi gani? Mengi naona yanaoza kwenye vituo vya polisi bora yangegeuzwa mabasi au zimamoto
 
Miaka yote hii hakuna mikakati ya kukabiliana na majanga? Kama kujaza maji kwenye magari kumeshindikana ndiyo wataweza kutengeneza mkakati?
Inshu ya zimamoto inahitaji preparation kubwa unaweza kwenda na maji yamejaa kumbe Moto unahitaji dry chemical Powder , au sand au carbon , Moto hauzimwi tu unazimwa kutokana na chanzo cha Moto , zaidi ukijua fire classes itakusaidia kwamba sio kila kitu ni zima Moto Bali watoa taarifa kuhusu chanzo cha moto
 
Kamishna Mkuu wa Zimamoto aliwahi kutumbuliwa enzi za JPM kwa tuhuma za kusaini mkataba aghali wa vifaa vya Zimamoto
Yule ni haki kabisa kutumbuliwa.
Unakwenda kununua drone hata nchi tajiri za Europe bado awajaweza kununua.
Magari ya kuzima moto tunayo lakini maji tu yametushinda.
Kwa nini asingewekeza kwenye water supplies kwenye sehemu kama hizi ambazo ni very risk!! Mambo madogo tu yanatushinda tunakimbikilia makubwa!!
 
Ule mkataba ulikuwa unaleta Dron hapo sokon ingefanyaje kazi? Lakini ata hivo huwezi kufanya mipango ya kusaini mkono wa takriban Trilion 1 huku baraza la waziri halijui chochote
Yule aliyetaka kununu drone ambazo ni bei kubwa ni mpuuzi sana!!
Hata water supplies ilimshinda ndio aliona drone ndio solution!
Angalia hata majengo yaliyojengwa sasa hivi kama yalijengwa kukabikiana na matatizo ya moto kama yakitokea. Mfano milango, window materials na hata kama ya hydrant karibu!!
Yeye badala ya kuboresha fire safety regulations alikimbilia mambo makubwa…bure kabisa!
 
Serikali pia inunue magari ya Zimamoto yenye maji.

Inasikitisha sana Waziri Mkuu anakuja na kauli kama ile eti kama Kuna mkono wa mtu.

Unasemaje namna hiyo, how do you lead a country ufikiri Kuna hujuma??

How long this administration itakua inalilia hujuma tu,

Hujuma ni kuficha madhaifu.

Lazima tupambane na madhaifu yetu na sio kulia lia kuhujumiwa.
 
Msitupotezee muda na wala Kamati hiyo haina haja ya Kutumia Siku nyingi. Kamateni upesi sana Watu wote waliokuwa wakiunda Bodi ya Soko hilo la Kariakoo iliyovunjwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwani kwa Taarifa za ndani kutoka kwa waafanyabiashara wakubwa hapo ambazo GENTAMYCINE nimezipata wamesema waliokuwa wakiunda Bodi ya Soko hilo Kubwa la Kariakoo ndiyo wamesababisha Kilichotokea kama sehemu yao ya Kulipiza Kisasi, Kukomoa na Kuuchafua Utawala qa Rais Samia na Kumjengea Chuki na Wafanyabiashara na Wamachinga Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Acha ramli. Na maeneo mengine ambako kila mara kunatokea ajali za moto, wanaosababisha ni iliyokuwa board ya soko la Kariakoo?

Nchi hii mambo mengi ni ovyo karibia kila sehemu. Hatuna uwezo wa kupambana na matukio ya dharula na ajali kwa sababu watawala hawajui vipaumbele.

Fikiria watu walivyokufa kwenye ajali ya meli pale Mwanza, ndipo utajua kuwa nchi hii hatuna serikali kwaajili ya watu bali ipo serikali dhidi ya watu.
 
Serikali pia inunue magari ya Zimamoto yenye maji.

Inasikitisha sana Waziri Mkuu anakuja na kauli kama ile eti kama Kuna mkono wa mtu.

Unasemaje namna hiyo, how do you lead a country ufikiri Kuna hujuma??

How long this administration itakua inalilia hujuma tu,

Hujuma ni kuficha madhaifu.

Lazima tupambane na madhaifu yetu na sio kulia lia kuhujumiwa.
Mombasa soko pia limeungua ... na kuna shule ya imeungua we unaonaje
 
Mombasa soko pia limeungua ... na kuna shule ya imeungua we unaonaje
Kule Arusha Kuna wakati shule ziliungua mfululizo walikua wanamhujumu Magufuli au??

Mimi nadhani serikali inapaswa kutathmini uwezo wake wa kukabiliana na majanga ya aina mbali mbali na sio kukimbilia tu kusema Kuna mkono wa mtu.

Tunapaswa kuwa na uwezo na utayari wa kukabiliana na dharura za aina mbali mbali.
 
Habari wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa soko kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

Makalla amesema kamati itakuja na mapendekezo ya namna bora ya kufanya ili kuendelea kukabiliana na majanga ya aina hiyo.

Mkuu wa Mkoa amewaomba waathirika kuwa watulivu wakati Serikali inachukua hatua za kubaini chanzo na athari. Pia amewakaribisha Bima kuja kuona wateja wao(Ambao walikuwa wamekata bima).

=========

Amos Makalla: Mheshimiwa Waziri mkuu, sisi tuko hapa toka jana, tumelala hapa baada ya janga hili la moto.

Athari ya janga hili ni kubwa na tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa watu isitkee vifo au ajali za watu lakini mali nyingi zimeharibika.

Waziri Mkuu: Ndugu wafanyabiashara, nimekuja kuleta salam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu. Kuja kwangu leo asubuhi ilikuwa ni moja ya maelekezo yake bna kuja kuona hali halisi ya kuungua kwa bidhaa mbalimbali ambazo ndizo zilizokuwa zinaipa hadhi ya eneo hili la Kariakoo.

Nimeona hali halisi na kwa namna ninavyojua soko la Kariakoo, hasara kubwa inatarajiwa kupatikana, kama ambavyo nimetangulia kuwapa pole, nirudie tena kuwapa pole kwa kupoteza mali, fedha lakini pia hata muelekeo wa kufanya shughuli zenu za kibiashara hapo baadae.

Eneo hilo kwa sasa ni hatarishi kwasababu bado moto unafuka mwingi, hatujajua bado kuna maeneo yana milipuko kama vile mitungi ya gesi ambao wanatumia gesi lakini kuna nyaya nyingi sana za umeme, kuna mitambo mingi iliyokuwa inauzwa lakini pia ilikuwa inatumika ndio maana eneo hili sio salama.

Tumeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi viendelee kuwa hapa kwa ajili ya kulinda usalama eneo zima lakini pia kuhakikisha moto huo hauendelei tena na watakuwa hapa mpaka utakapotulia kabisa.

Nawasihi sana wafanyabiashara wote muwe watulivu, kwasasa Serikali ipo na itaendelea kuwepo hapa mpaka tutakapojua nini chanzo cha moto huu, nani kisababishi cha moto huo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa

Mkuu wa mkoa ameunda timu ya uchunguzi lakini bado haitoshi, hili soko ni la kimataifa. Itakuja timu ya kitaifa ambayo itaungana na timu ya mkuu wa mkoa.

Timu ya mkuu wa mkoa ni wale ambao walikuwa hapa kuanzia jana wakafanya kazi ya uokoaji na kusikia hiki na kile na kupata taarifa

Timu hii ya kitaifa kuchunguza moto itajumuisha wafuatao
  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka
Kama nilivyosema awali, tubaini chanzo cha moto. Nini kimesababisha au nani kasababisha moto huu. Pili tunataka tujue angalau kutabiri tu kiwango cha mali zilizopotea.

Tatu tunataka tujue usalama wa jengo lenyewe baada ya moto, Je jengo bado linaweza kutumika?

Endapo itagundulika kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, ndio maana huko ndani kuna Mwanasheria Mkuu, mkurugenzi wa mashtaka, Polisi. Hatua zitachukuliwa moja kwa moja.

Ndugu wafanyabiashara, tunatambua mheshimiwa Rais alipotembelea hapa aliunda tume ya kufanya mapitia ya tuhuma mbalimbali ziliibuliwa, inawezekana pia sijui, labda tume hiyo ilianza kuwagusa. Kama kulikuwa na njama zozote zilizowahusu tume ile na hao waliokuwa wanaguswaguswa na wakigundulika, hatua kali zitachukuliwa
je kama ni hitilafu ya umeme,
 
Kule Arusha Kuna wakati shule ziliungua mfululizo walikua wanamhujumu Magufuli au??

Mimi nadhani serikali inapaswa kutathmini uwezo wake wa kukabiliana na majanga ya aina mbali mbali na sio kukimbilia tu kusema Kuna mkono wa mtu.

Tunapaswa kuwa na uwezo na utayari wa kukabiliana na dharura za aina mbali mbali.
Shule zote za mlengo flani wa dini? Hakuna kitu kama hicho kwenye intelligensia labda tu useme sababu na motives behind hazikuwekwa public
 
Tunapowaambia nchi inahitaji mabadiliko mnaanza kusema chokochoko tunahitaji fikira pevu sio hizi za kinyerere pumzikeni hata hao munaowaita wapinzani ni watanzania wote mmetuletea mpaka wahutu na wametuongoza pumzikeni mmechoka nyie ma Ccm
 
Inshu ya zimamoto inahitaji preparation kubwa unaweza kwenda na maji yamejaa kumbe Moto unahitaji dry chemical Powder , au sand au carbon , Moto hauzimwi tu unazimwa kutokana na chanzo cha Moto , zaidi ukijua fire classes itakusaidia kwamba sio kila kitu ni zima Moto Bali watoa taarifa kuhusu chanzo cha moto
Siku zote tunaambiwa na vyombo vya usalama chanzo cha moto hakijulikani, sasa wananchi wa kawaida watajuaje kama wataalamu hawajui
 
Back
Top Bottom