Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Mwanakijiji!No problem KT, tangu niamke nimekuwa nikijitahidi kuwasiliana na Balozi Chokala bila ya mafanikio. Nimetuma email na pindi nikipata majibu nitawajulisha.
Kama wataweza kuomba Assylum na kufanikiwa sioni ubaya wake ila itakapotokea wakakataliwa na kurudishwa Nyumbani huoni hapo watakuwa wamejiweka ktk kufunguliwa mashitaka kwani ndivyo wafanyavyo.Kama hao ubalozi walikubali waende Kiev Halafu walipofika wamewaacha nje huoni hilo nalo ni tatizo ,nilitegemea watawapokea na kuwapatia mahitaji ya muhimu ya kijamii wakati wanasubiri hatima au uamuzi kutoka serikali yetu Lakini kitendo cha kuwawacha Nje ya Balozi sioni Kama kinaleta picha nzuri ya kupata msaada hasa kwa maana ya msaada au cha hao ubalozi kutoa msaada kwa maana ya msada uliokamilika kwa watu wenye shida kama hao vijana wetu.KNKCU, nimeshazungumza na wanafunzi wa Urusi ambao kesi yao ni tofauti kidogo lakini na wenyewe wanamatatizo hasa miezi hii inayokuja.. nimezungumza na wanafunzi wa Cuba ambao matatizo yao yalikuwa yanakaribiana na wa Ukraine. Ni kweli mengi yametetatuliwa, ila kama nilivyoeleza kwenye mada nyingine kesi ya Ukraine ni tofauti kidogo. Hata hivyo kumbuka pia kuwa kwa vijana hawa kuja hadharani na kusema hadharani na kutaja majina hadharani.. wamejijengea uadui mkubwa, hata kama wakirudi wanaweza kushindwa kabisa kusoma tena Tanzania!! na wakaoenekana ni maadui wa serikali!! mwisho tutaanza kuwashauri waombe political asylum kwani serikali haiwezi kuwatendea lolote jema baada ya haya yote.. I might be wrong.. lakini that option should be on the table now!
we'll take a notch higher next week..
Sasa huyo Mh. Chokala anafanya nini Kama hawezi kukubali ktk mambo ya shule kwavile hana mamlaka nayo kwanini asikubali tu kusaidiwa na huo ubalozi wa uingereza kwa kukubali wakatiwe angalau tiketi warudi nyumbani.Nafikiri tunamatatizo ya decision making Kama ni mimi ningekubali msaada wa hao vijana kukatiwa tiketi warudi nyumbani ,Halafu nione kama hao mabosi huko nyumbani ktk hali kama hiyo wangenifukuza kazi kwani ushahidi wa fedha zilivyotumika ungekuwepo tena kuna Organization inaitwa IMO(INTERNATIONAL MIGRATION ORGANIZATION) Ni kiasi tu cha balozi kuwaandikia tu nina wananchi wenzagu ninaomba wasafirishwe kurudishwa Tanzania kwani hatuna uwezo kwasasa.Hao jamaa wakipata hiyo barua wanawaandalia walengwa usafiri na fedha za matumizi hadi kwao.Wana ofisi pale moscow inayoshughulikia Nchi zote zilizokuwa chini ya Jamhuri ya Kisoviet ya Urusi ikiwemo hiyo Ukraine.kwa vile sasa hivi hawajaomba Asylum ndio maana ubalozi unafungwa mikono kidogo. Na ubalozi huo uko tayari kuwasaidia endapo tu serikali ya Tanzania itakuwa tayari kurudisha hizo fedha kwa ubalozi. Nina uhakika endapo wataamua kujilipua basi ubalozi utaanza kushughulikia kama wakimbizi au asylum seekers..!
Unajua kadiri unavyotafuta habari kupitia vyanzo mbali mbali ndiyo unavyoelewa zaidi na unapopata majibu ya uhakika kutokana na kile unachokifuatilia,Baada ya kutafuta habari na kuona kuna wanafunzi wanalipiwa tena Nchi nyingi tu na bodi ya mikopo na maelezo yako amabayo umeyapata moja kwa moja kutoka kwa hao vijana nimeona tatizo ni hilo,Inanisikitisha sana na ninatamani kuona ufumbuzi wa haraka unafanyika ili kuwatoa hawa vijana kwenye hiyo adha wanayopambana nayo.Unajua nimewahi kutembelea Ukraine mara kadhaa ninaelewa nini kinachowakabili hao vijana ktk mazingira ya NCHI ILE.Kinachonisikitisha ni kwamba pamoja na majukumu yetu tuliyonayo sisi kama wanadaamu tunawezaje kutafuta habari na kujaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo lakini wale wenye Jukumu hilo ambao ni watumishi wa umma na wanalipwa kwa kazi hiyo washindwe?Kazi, naona umeona tatizo lilipo sasa..
Kiev: Vijana bado wapo. Wamewaruhusu dada zao (3) kurudi vyuoni kwani hali ya hewa si nzuri. Usiku wa kuamkia leo wamenyeshewa na mvua lakini bado wapo nje ya Ubalozi wakisubiri majibu labda kesho asubuhi.
Moskow: Ubalozi bado haujasema lolote na jitihada za kuwapata hazikuzaa matunda.
Dar: Msimamo wa serikali wa kutowatambua na kushindwa kutafuta utatuzi wa suala hili bado ni ule ule. Hakuna kiongozi anayejisikia haja ya kulizungumzia jambo hilo. Vyombo vya habari vya nyumbani licha ya kujua kuhusu suala hili bado wako kimya na hawajaanza kulifanyia kazi.
Michango:
Hadi hivi sasa ni watu wanne tu wamechanga karibu dola 300 hivi ambazo zimetumwa na zimepokelewa leo. Nashukuru wote mliojitokeza kusaidia na kwa niaba yao Mnyezi Mungu awabariki na kuwazidishia.