Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
na Nasra Abdallah (Tanzania Daima)
UMOJA wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na TLP, umeitaka serikali kueleza wazi juu ya hatima ya wanafunzi wa Kitanzania wapatao 29, ambao walikuwa wanasoma nchini Ukraine na kufukuzwa kwa kushindwa kulipa ada.
Viongozi wa vyama hivyo, walitoa kauli ya pamoja mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki iliyopita, zilikuwa zinaeleza kuwa, kutokana na hali mbaya kifedha inayowakabili, wanafunzi hao waliamua kujisalimisha katika ubalozi wa Uingereza uliopo nchini humo.
Ubalozi huo, nao ulikubali kuchukua mzigo wa kuwahudumia wanafunzi hao wakati matatizo yao yanatafutiwa ufumbuzi.
Vyama hivyo vimetaka kujua msimamo wa serikali, baada ya wanafunzi hao kutelekezwa na kuamua kuomba hifadhi kwenye ubalozi wa Uingereza jijini Kiev, huku serikali ikiwa imeendelea kukaa kimya bila ya kusema lolote.
Wakizungumza kwa masikitiko, viongozi wa vyama hivyo walisema tukio hilo ni la aibu kwa taifa, kwani kwa kushindwa kuwalipia ada, serikali imewafanya raia wake waishi nchi za ugenini kama watu wasiokuwa na nchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema ameshamuandikia Rais Jakaya Kikwete barua kuhusu suala hilo zaidi ya mara tatu, lakini hadi leo hajajibiwa hata barua moja.
Mrema alisema wazazi wa wanafunzi hao wamekuwa wakienda ofisini kwake mara kwa mara, kumuomba awasaidie ili watoto hao waweze kuendelea na masomo.
"Hata jana (juzi) wazazi hao walifika ofisini kwangu huku wakiwa wanalia, ikabidi nitume barua nyingine kwa rais kama kumkumbushia, lakini mpaka ninavyoongea na nyie hivi sasa, sijajibiwa chochote, sasa sijui ni kudharauliwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani au wanaona kama tunajitafutia umaarufu kupitia wananchi wanyonge, ambao wamekuwa wakiumizwa kupitia kodi zao," alisema.
Alisema serikali ina wajibu wa kuwalipia wanafunzi hao ada ili waweze kuendelea na shule.
Mrema alidai kuwa ana vielelezo vyote alivyopatiwa na wazazi wa wanafunzi hao vinavyoonyesha kuwa serikali iliahidi kuwalipia ada.
Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James mbatia, alisema kukaa kimya kwa serikali ni kuwadharau wananchi ambao ndio wamewaweka madarakani, kwani fedha zinazodaiwa si nyingi kiasi cha serikali kushindwa kulipa.
"Fedha zinazotakiwa ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo ni sh bilioni 6, lakini tunashangaa serikali imeendelea kuwapuuza wananchi wake ambao kodi zao ndizo zinazotumika kununulia mashangingi wanayotembelea," alisema Mbatia.