Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,577
Nawapa Pole sana ,Hivi hao walinzi wa hizo balozi walikuwa wanafanya nini wakati vijana wanashambuliwa?Kwani tuliwahi kuelezwa hapa kwamba vijana wapo kwenye hali ya usalama hasa ukizingatia ulipo Ubalozi wa UK vile upo Ubalozi wa USA.Sasa nini kimejiri tena?Ninahabari za kusikitisha zaidi kutoka Ukraine...!Ubalozi wa UK leo umefunga kazi mapema kutokana na mapumziko ya siku nne. Kutokana na jibu walilopewa na serikali jana, Ubalozi huo umejitolea kuwalipia tiketi za kurudi hadi vyuoni ili kusubiri hatima yao kwani wao (ubalozi) unashindwa kufanya lolote zaidi kwa wakati huu. Vijana walitaka kuendelea kukaa hapo nje lakini kwa Ubalozi umewasihi warudi vyuoni na watawaombea wasifukuziwe mitaani kwani hali ya usalama wao pale siyo nzuri. Kabla vijana hawajaondoka na mara baada ya ubalozi kufungwa, vijana wawili wameshambuliwa na kujeruhiwa na "skinheads" (vijana weupe wanaopinga watu wa rangi nyingine) ambao walikuwa wameanza kuwasumbua na kuwanyanyasa siku mbili zilizopita nusu saa iliyopita vijana hao wawili wamekimbizwa hospitali wakiwa wamepoteza fahamu. Kijana mmoja ameporwa kamera yake, na wengine waliobakia sasa wamechanganyikiwa na hawajui kama waondoke na kurudi vyuoni au wasubiri hatima ya wenzao. Hawajui waombe msaada wapi.
Kati ya mambo yote niliyoyahofia kutokea ni jambo kama hili. Ndugu zangu msije kusikia habari mbaya sana kutoka Ukraine, leo au mwishoni mwa juma hili.
Ni wapi kati ya vijana hao waliopo kwenye Picha wamepatwa na mkasa huo?Ninahabari za kusikitisha zaidi kutoka Ukraine...!Ubalozi wa UK leo umefunga kazi mapema kutokana na mapumziko ya siku nne. Kutokana na jibu walilopewa na serikali jana, Ubalozi huo umejitolea kuwalipia tiketi za kurudi hadi vyuoni ili kusubiri hatima yao kwani wao (ubalozi) unashindwa kufanya lolote zaidi kwa wakati huu. Vijana walitaka kuendelea kukaa hapo nje lakini kwa Ubalozi umewasihi warudi vyuoni na watawaombea wasifukuziwe mitaani kwani hali ya usalama wao pale siyo nzuri. Kabla vijana hawajaondoka na mara baada ya ubalozi kufungwa, vijana wawili wameshambuliwa na kujeruhiwa na "skinheads" (vijana weupe wanaopinga watu wa rangi nyingine) ambao walikuwa wameanza kuwasumbua na kuwanyanyasa siku mbili zilizopita nusu saa iliyopita vijana hao wawili wamekimbizwa hospitali wakiwa wamepoteza fahamu. Kijana mmoja ameporwa kamera yake, na wengine waliobakia sasa wamechanganyikiwa na hawajui kama waondoke na kurudi vyuoni au wasubiri hatima ya wenzao. Hawajui waombe msaada wapi.
Kati ya mambo yote niliyoyahofia kutokea ni jambo kama hili. Ndugu zangu msije kusikia habari mbaya sana kutoka Ukraine, leo au mwishoni mwa juma hili.
yah msisahau kuwa hayo yote yanawakuta WAKIMBIZI kama hao vijana
ni kawaida hiyo kwa wakimbizi kukuta na majanga kama hayo.
HIVI HAO SKY NEWS bado hawajaipata tuu?
...and yet Tanzania inaambiwa ni nchi yenye amani na utulivu, nchi inayoheshimu haki za binadamu na utawala bora..nilidhani hata hao wanaozunguka nchi kukusanya maoni/malalamiko ya wananchi kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu wangelionahili..as a result WATANZANIA wanapigwa na skinheads wakati wakijaribu kutafuta haki zao...OOOh Lord!