Ninahabari za kusikitisha zaidi kutoka Ukraine...!Ubalozi wa UK leo umefunga kazi mapema kutokana na mapumziko ya siku nne. Kutokana na jibu walilopewa na serikali jana, Ubalozi huo umejitolea kuwalipia tiketi za kurudi hadi vyuoni ili kusubiri hatima yao kwani wao (ubalozi) unashindwa kufanya lolote zaidi kwa wakati huu. Vijana walitaka kuendelea kukaa hapo nje lakini kwa Ubalozi umewasihi warudi vyuoni na watawaombea wasifukuziwe mitaani kwani hali ya usalama wao pale siyo nzuri. Kabla vijana hawajaondoka na mara baada ya ubalozi kufungwa, vijana wawili wameshambuliwa na kujeruhiwa na "skinheads" (vijana weupe wanaopinga watu wa rangi nyingine) ambao walikuwa wameanza kuwasumbua na kuwanyanyasa siku mbili zilizopita nusu saa iliyopita vijana hao wawili wamekimbizwa hospitali wakiwa wamepoteza fahamu. Kijana mmoja ameporwa kamera yake, na wengine waliobakia sasa wamechanganyikiwa na hawajui kama waondoke na kurudi vyuoni au wasubiri hatima ya wenzao. Hawajui waombe msaada wapi.
Kati ya mambo yote niliyoyahofia kutokea ni jambo kama hili. Ndugu zangu msije kusikia habari mbaya sana kutoka Ukraine, leo au mwishoni mwa juma hili.