Serikali yaziunganisha Benki za TPB na TIB Corporate na kuwa Benki moja ya Biashara

Serikali yaziunganisha Benki za TPB na TIB Corporate na kuwa Benki moja ya Biashara

Huoni ni kutaka ua mabenki mengine.
Mana mmelazimisha taasisi na mashirika yote yawe na account na malipo yote yafanyike kupitia TCB
Bwashee mbona Vodacom na Tigo hawajafa?

Soko la benki ni kubwa sana!
 
Huoni ni kutaka ua mabenki mengine.
Mana mmelazimisha taasisi na mashirika yote yawe na account na malipo yote yafanyike kupitia TCB
Kila kitu anataka jiwe chini Yake, na Doto Wa hazina ndio mastermind, ajira nyingi zitapotea but he doesn't care
 
Wafanyakazi inakuwaje?Wa TIB wanakuja posta au?
 
Tulizoea miaka ya nyuma Benki kuzaa Mtoto mfano NBC ilivyozaa NMB lakini leo tunaona watoto wakiungana na siyo kuzaa tena.
Uendeshaji wa Benki zetu unapaswa kuangaliwa kwa namna nyingine
 
Ngoja tupitie hili libarua kidogo


EYhL22TWoAABFnx.jpeg


EYhL22jWAAE7_nK.jpeg



EYhL22lWsAAMyr3.jpeg
 
Fuatilia historian ya China(mfumo Huawei) na urusi(Gazprom) then urusi hapa
 
Serikali imeamua kuziunganisha Benki ya TPB na TIB Corprate kuanzia Juni Mosi, 2020 kwa lengo la kuboresha utendaji wa benki inazomiliki ili kuwa na Benki moja ya biashara ambayo ni imara.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

Bw. Mbuttuka alisema kuwa muungano wa Benki hizo unalenga kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na taswira ili benki hiyo iweze kuhimili ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.

“Serikali inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kuhakikisha utendaji wa benki zake unaimarika na maslahi ya wenye amana na wateja wote yanalindwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa Benki na taasisi za fedha”, alieleza Bw. Mbuttuka

Bw. Mbuttuka alisema kuwa kwa hatua ya awali, Benki ya TPB itachukua mali na madeni ya Benki ya TIB Corprate na Wateja wote wa Benki ya TPB na Benki ya TIB Corporate wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.

Aidha alisema kuwa Serikali inawahakikishia wateja wa benki hizo mbili pamoja na umma kuwa huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote vile kutokana na mabadiliko hayo

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana, ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.
 
Bado Benki ya Kilimo (TADB ) na TIB Investment Bank...Hizi zilitakiwa zitangulie na mchakato uliushakaa vyema sijui nini kinachelewesha manake nazo hazijitambui... Benki ya Kilimo inakopesha walima kwenye lami na vyama vya ushirika vilivyovilisika tu..Aisee
 
Huo muunganiko utakua na tija sana iwapo utaendana na upunguzwaji wa riba kwa wateja kwa kiwango cha chini zaidi kuliko benki nyingine yoyote ile nchini, na pia kupunguza masharti ya ukopaji hasa kwa wananchi wasio na dhamana kama nyumba, gari, kiwanja, nk.
 
Mkuu Paskali,
TFDA (Tanzania Food and Drug Authority) majukumu ya chakula yamehamia TBS

Kwa sasa kuna TMDA Tanzania Medicine and Medical Devices Authority.

Hawa Bankers wana haja ya kuwa wabunifu ili kuongeza ufanisi kwenye biashara hasa kwenye ulimwengu wa ushindani.

TIC, EPZA, TRA, BRELA hawa wanatakiwa kuwa na mfumo mmoja ambapo ukisajili kampuni, same system ya usajili imsaidie mteja kuondoka na all the necessary docs za kumfanya kuanza biashara.

Hii ni hatua nzuri kupunguza duplication na kuunda vyombo giant's.

Bado kuunganisha TIC na EPZA.

TFDA na TBS
P
 
Ndio utaishuhudia hii ikifanikiwa bwashee!
Kwenye upande wa banking. Serikal haijawahi kufanya vizuri.
TIB was a sign of failure according to last data.
This time tuone. But if hawana creative person wa kuongoza hizi taasis ..bado tu lazima itabuma tena.
 
Bwashee usiwe mbumbumbu na mjinga, kwani huko kwenye benk zingine Magufuli akitaka kupiga hela kinashindikana kitu gani?
Mijitu ya Chadema imejaa ukungu kwenye akili zao.u
 
Back
Top Bottom