Serikali yaziunganisha Benki za TPB na TIB Corporate na kuwa Benki moja ya Biashara

Serikali yaziunganisha Benki za TPB na TIB Corporate na kuwa Benki moja ya Biashara

Ndio utaishuhudia hii ikifanikiwa bwashee!
Haya yanayotokea ni uthibitisho wa jinsi ambavyo wameshashindwa, watazivuruga kila aina ya muundo, ukweli unabaki kuwa, serikali haifanyi biashara.
Atcl nayo inapumua kwa pesa za walipa kodi, wenzao duniani kote wameshatangaza hasara, hasa kutokana na janga la korona, sisi tunadanganywa mambo ni mazuri, uchumi haujatetereka wakati ni dhahiri, pesa za walipa kodi ndio zitaelekezwa kuyanusuru makapuni yaliyo chini ya serikali.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Tulikuwa tunajua toka zamani. Ni mpango w Magu kuiba pesa ndefu. Na tender nyingi zitakuwa zinapitia hapo.

Crooks are leading the country what do you expect?

Hata NMB hawatalipa salary tena. Hii bank ndio italipa . mtegemee vipigo kwa lend mbele. Doto ndio master mind akipoke maelekezo from Chato regime
Hata ivo NMB kupewa hio kazi naona alianza kujisahau kabisa sasa balaa lake Akipokonywa mbona itakuwa balaa mana ma bank mengi yanapulia mashine
 
Miaka ya nyuma yupo waziri aliwahi unganisha masomo Maths plus history ikawa somo moja, physics plus chemistry ikawa somo moja etc eti wanafunzi wasiwe na vipindi vingi.

Naona sasa ndiyo yameingia benki.

Okay we will see.
 


SERIKALI imziunganisha benki za TPB Bank Plc pamoja na TIB Corporate ili kuimarisha utendajikazi wa benki hizo na kuhimiri ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Athuman Mbutuka alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari.

Aidha Mbutuka amesema kuwa Kufuatia uamuzi huo leo Juni Mosi mwaka huu, benki ya TPB itachukua mali na madeni ya benki ya TIB huku serikali ikisisitiza kulinda maslahi ya wafanyakazi wote kwenye benki hizo.

Mbutuka amesisitiza kuwa maslahi ya wenye amana na wateja wote yatalindwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa benki na taasisi za fedha.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji,” ameeleza Mbutuka.

Mbutuka ameongeza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na kitaswira ili benki iweze kuhimili ushindani kwenye sekta ya fedha nchini

Mbutuka amehitimisha kwa kuwatoa hofu wateja wa benki wa TPB na TIB wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo na huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote kutokana na mabadiliko hayo.

Kigogo alisema haya Week Mbili zilizopita MATAGA wakambishia!!! Akatuambia Subirini mtaona na kweli zimeunganishwa halafu anatokea mtu anasema taarifa za kigogo ni uongo huku sirikali ikihaa kumtafuta.
 
Watapona tu, mtanao wao ni mpana mno, they are too big to fail.
Too big to fail ni misemo tu hio mkuu,hata Lehman brothers walikua kwny category hio hio ya 'too big to fail 'lkn mtikisiko ule uliondoa ile dhana.
 
Too big to fail ni misemo tu hio mkuu,hata Lehman brothers walikua kwny category hio hio ya 'too big to fail 'lkn mtikisiko ule uliondoa ile dhana.
Ni kweli lakini kumbuka Lehamn brothers ilikuwa investment bank, hizi zetu ni retail, they are more resilient kuliko investment banks
 
Aisee hapo NMB,CRDB,NBC ndio mwendo wa kifo cha mende,wanapelekwa kibra kwa style ya mwendo wa bata.
Shida benki zote zinataka kufanya biashara na serikali hata visaccos wanataka kufanya biashara na serikali ili uwe stable kibiashara lazima uwe huru kufanya biashara na kila mtu na sio kutegemea upande mmoja mana huo upande ukibadili upepo n lazima wewe upotee kama sio kufa kabisa n muda muafaka kwa hizi benki maarufu Tanzania kuanza kufanya biashara na mwananchi wa kawaida kwa mazingira nafuu zaidi ya kumnyonya huyu mtanzania mdogo kwa kunufaisha kukopesha bank kupitia DEPOSIT na kulipia monthly na transaction charges hope bank hizi zikibadili upepo maisha yatakuwa rahisi sana
 
Ni kweli lakini kumbuka Lehamn brothers ilikuwa investment bank, hizi zetu ni retail, they are more resilient kuliko investment banks
Let's assume mishahara yote ya wafanyakazi wa serikalini ihamishiwe TPB,mikopo ya wafanyakazi iwe inatolewa TPB,Taasisi za umma zote as per above document wahamishie a/c zao TPB,Govt internal borrowings zifanyikie TPB(ingawa so far nadhani hio mikopo ya ndani inakaribia kuleta clouds out effects au possibly imeshaleta tayari), unadhani banks zote zilizobaki zitaweza ku survive kwa kutegemea private sector only?

BTW sector yetu ya bank bado ni changa tu hatujafikia uwezo wa kujitegemea kiasi hicho,ninaweza kukupa mfano mrahisi:Ukwasi wa bank ya FNB ya south Africa ni mkubwa kuliko ukwasi wa banks zote zilizoko Tz combined.
 
Miaka ya nyuma yupo waziri aliwahi unganisha masomo Maths plus history ikawa somo moja, physics plus chemistry ikawa somo moja etc eti wanafunzi wasiwe na vipindi vingi.

Naona sasa ndiyo yameingia benki.

Okay we will see.

Haaa, Joseph Mungai RIP, nchi hii imepitia maajabu mengi, imagine Maths + History, hell no, unthinkable.
 
Let's assume mishahara yote ya wafanyakazi wa serikalini ihamishiwe TPB,mikopo ya wafanyakazi iwe inatolewa TPB,Taasisi za umma zote as per above document wahamishie a/c zao TPB,Govt internal borrowings zifanyikie TPB(ingawa so far nadhani hio mikopo ya ndani inakaribia kuleta clouds out effects au possibly imeshaleta tayari), unadhani banks zote zilizobaki zitaweza ku survive kwa kutegemea private sector only?

BTW sector yetu ya bank bado ni changa tu hatujafikia uwezo wa kujitegemea kiasi hicho,ninaweza kukupa mfano mrahisi:Ukwasi wa bank ya FNB ya south Africa ni mkubwa kuliko ukwasi wa banks zote zilizoko Tz combined.


Yaani ukwasi wa TPB + TIB zikiungana ni Tshs 1 tril tu, kidogo sana sana hizo aisee.
 
Shida benki zote zinataka kufanya biashara na serikali hata visaccos wanataka kufanya biashara na serikali ili uwe stable kibiashara lazima uwe huru kufanya biashara na kila mtu na sio kutegemea upande mmoja mana huo upande ukibadili upepo n lazima wewe upotee kama sio kufa kabisa n muda muafaka kwa hizi benki maarufu Tanzania kuanza kufanya biashara na mwananchi wa kawaida kwa mazingira nafuu zaidi ya kumnyonya huyu mtanzania mdogo kwa kunufaisha kukopesha bank kupitia DEPOSIT na kulipia monthly na transaction charges hope bank hizi zikibadili upepo maisha yatakuwa rahisi sana
Naunga mkono hoja boss kwa 100% na hata Magu alivyoingia madarakani alisema hilo jambo sana lkn sector ya bank bado ni changa sana tu bado inahitaji kupelekwa mdogo mdogo kiaina.

Hivi serikali tangu lini imefanikiwa kufanya biashara?Angalia POSTA,TTCL,TANESCO,ATCL(ambayo mnaweza ku delay kuondoka kwa masaa 2 zaidi wakiulizwa mnajibiwa tunamsubiria Dr. Tulia bado hajaingia kwny ndege), yaani inshort ili serikali ifanikiwe kufanya biashara ipasavyo lazima itengeneze mazingira ya kua MONOPOLY na hapo lazima kuna wahanga,je kwny hii sector ya ki bank nani ataenda kua mhanga?

Let's wait n see boss.
 
Back
Top Bottom