Serikali yazuia vifaranga 62,730 vilivyoingizwa nchini kutoka Ubelgiji

Sasa huyu aliyeingiza hivyo vifaranga si wangemuacha tu ili apate hasara? Maana soko la vifaranga hakuna kwa mujibu wa yule mzungu wa Arusha
Labda hukumuelewa yule Mama !! Kuhusu hili la sasa; sheria ifuate mkondo wake.
 
Mkuu naomba unisaidie. Yule mama alivichoma vifaranga vyake kwa sabb gani haswa?
Sababu kubwa ni gharama kutoendana na bei ya soko ikiwa ni pamoja na uingizwaji wa vifaranga kutoka nje. Na sio ajabu uingizaji huu wenye ukwepaji kodi ni sababu mojawapo ya wafugaji wa ndani kushindwa kuendana na biashara hii na hivyo baadhi yao kuamua kuachana nayo.
 
Hahahah rais Samia walindanganya afungue nchi, na kumdhihaki Dkt Magufuli, naona hivyo vifaranga ni moja ya big failure ya sera ya kufungua nchi ya rais Samia. Sisi wana CCM tunampenda sana, uzuri kila jambo tunamtonya kuwa anahujumiwa na wabaya wake. Swali hivyo vifaranga vitachomwa moto???
 
Serikali ya awamu ya sita inafungua nchi
 
Labda hukumuelewa yule Mama !! Kuhusu hili la sasa; sheria ifuate mkondo wake.
No Rais Samia alisema ilikuwa makosa kuchoma vifaranga vya kenya, je vya hawa wazungu atavichoma??? Au vitarejeshwa??? Kwa ufupi nchi yetu imekosa dira na muelekeo. Tukiwaambia ni mtu asiyekuwa na info ndiye atakuja kuwekeza Tanzania, nwenye uelewa atachagua na kujiuliza sana kabla ya kuwekeza
 
Madam President akisema anaifungua nchi maana yake ni nini? Maana yake si ni kuwa na soko huria!?

Unampata wapi mwekezaji gani wa nje bila ya kumhakikishia ushindani huru na wenye haki sokoni!?
Hivi uwekezaji huwa unachagua soko la ushindani!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Let's wait and see for a proper action to be taken.
 
Sheria inaweza kurekebishwa, yule bwana nilisoma habari yake, ni wazi hana connection/hajui biashara ya Tz, Mkuu unadhani biashara ya kuku imekuwa kwenye hali ile kweli ? Kila siku Bar kuku zinaliwa,Moshi pale mishikaki ya kuku wanauza mpaka buku

Ndio maana unaona huyu kaingiza kuku wote hawa anajua biashara ni nzuri , yule aliyechoma atakua hakuwa na pesa ya kuvilisha vile vifaranga labda, lakini angevifuga ilikuwa pesa ipo
 
Hahahaha wale viherehere wa kufungua nchi waje haraka sana hapa. Maana wengi comments zao eti aliyeingiza vifaranga aadhibiwe. Unajiuliza swali, je Rais si walimdanganya kuwa eti nchi ilikuwa imefungwa, na wakamuandalia safari na alivyorudi akaitisha vyombo vya habari akijisifia kusema eti nchi ilikuwa imefungwa enzi za Dkt Magufuli wakati yeye huyo huyo rais Samia alitumwa kwenda nje kumuwakilisha na mabalozi duniani kote walitumwa, then eti unakuja kusimama kuutamkia umma eti nchi ilikuwa imefungwa??? Hakika kazi iko kubwa mbeleni. Maana akija rais Mwingine atamwaga kejeli kibao kwa rais Samia. Rais Samia bado anaomuda, amuombe radhi Dkt Magufuli huko aliko amsamehe kwa dhambi ya kumdhihaki na kumdharau otherwise utawala wa rais Samia utaendelea kuonekana ni maigizo
 
Hebu kwanza:

Huyu Professa Hezron E Nonga ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, na wakati huo huo ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi?

Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza hapa:

Hii Kampuni ya Phoenix hawajui sheria zilizopo zilizotajwa hapo, kiasi kwamba hawakufikiri kabisa kuwa wanaweza kuingia hasara kubwa, au walishajua namna ya kuzunguka hizo sheria, na kwa bahati mbaya sana safari hii ikawa tofauti?

Lakini ukweli ni kwamba, hivyo vifaranga vimekwishaingia Tanzania, hayo mengine yanayosemwa kuvirudisha UBelgiji ni stori tu za vijiweni.
Inawezekana kabisa mwekezaji mwenyewe alijua hivyo na hana mashaka yoyote juu ya vifaranga vyake. Hizo kelele ni kulaza tu akili za wajinga.

Ni hivi karibuni tu pametolewa taarifa za kuzuia uagiza wa vifaranga na mayai ya kutotolesha toka nje na wizara hiyo hiyo kwa sababu za kuwalinda tu wazalishaji wa ndani, ambao sasa bei zao zipo juu sana. Kuna umuhimu wa kuangalia upya zuio hilo lisilokuwa na manufaa kwa sekta hiyo.
 
Tukisema Nchi hii imeshakuwa shamba la Bibi watu wengine wanakataa.
Hivyo vimeshikwa, je, vingapi havijashikwa?
Hata hivi kushikwa kutakuwa na sababu zake ambazo hazielezwi.

Habari ilivyokaa ni kama alikuwa anajua analofanya toka mwanzo.

Hakuna mtu mwenye akili timamu achukue risk yote hiyo (hiyo ni hela ndefu hata kwa wenye ukwasi kupoteza tu hivi hivi).
Anajua vifaranga havirudi ubelgiji, na mambo yatakwisha kimya kimya.
 
Hivi wale wa kibaha walochoma vifaranga kukosa soko ndo Hawa hawa au wengine[emoji848]
 
Vifaranga wanatolew Belgium kuja Tanzania, duh!
 
Hawa ni Parents stock, nashangaa sana kwa nini anaingiza Parents stock bila kibali, ni uzembe wa kiwango cha mwisho kabisa, yaani wa kulaumu ni mwagizaji wa hao vifaranga
 
Sasa huyu aliyeingiza hivyo vifaranga si wangemuacha tu ili apate hasara? Maana soko la vifaranga hakuna kwa mujibu wa yule mzungu wa Arusha
Ni.mzembe sana huwezi ingiza mzigo huo mkubwa hivyo Bila vibali aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…