Serikali yazuia vifaranga 62,730 vilivyoingizwa nchini kutoka Ubelgiji

No Rais Samia alisema ilikuwa makosa kuchoma vifaranga vya kenya, je vya hawa wazungu atavichoma??? Au vitarejeshwa??? Kwa ufupi nchi yetu imekosa dira na muelekeo. Tukiwaambia ni mtu asiyekuwa na info ndiye atakuja kuwekeza Tanzania, nwenye uelewa atachagua na kujiuliza sana kabla ya kuwekeza
Kuchom.wale vifaranga ilikuwa sahihi hakuna cha kosa pale, hata hawa walipaswa kutiwa kiberiti sema muagizaji ni mzembe mno mno mno
 
Ndiyo maana tunasema Rais Samia kazungukwa na minafiki, ile issue ya vifaranga vya kenya ilikuwa sahihi ila wao wakamdanganya
 
Ngoja tushuhudie vifaranga viivyotoka kwa beberu vikitiwa moto...
 
Urasimu umerudi... Kwani Si tunanunua mchele kilo 3000 sababu mchele mwingi umeuzaaa nje?? Mahindi kama yote yameenda kenyaaa... Leo wananchi wanapambana na kupanda na bei za mazao ila kuna viongozi wakubwa aana maghala ya vyakulaaa wanatuuzia bei juuu.. Urasimuu urasimuuuu...
Mimi ni mkenya lakini maandishi Yako haya yanakeraaaaaa
 
Ni.mzembe sana huwezi ingiza mzigo huo mkubwa hivyo Bila vibali aisee
Kwani yeye ni mgeni katika biashara hii?

Hata kama angekuwa mgeni, mfanya biashara yeyote hawezi kuchukua 'risk' kiasi alichochukua huyu. Kuna sababu zisizoelezwa.
Huyu ni mzoefu wa uhalifu, ndiyo maana hakuwa na wasiwasi na analofanya.
 
Inaonekana huyo mtu kaingiza hivo vifaranga Kwa ajili ya kampuni yake ...Kwa jambo sensitive kama Hilo kweli hakuwa na vibali? Au wanamfanyia figisu?
Why vifaranga vitoke mbali namna hiyo Kwa gharama kubwa ...vina uspecial gani? Je mbegu ya hao kuku ni hatari au?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wapewe masaa 12 kuviondosha na kuvirudisha walikovitoa la sivyo vipigwe moto. Nchi yetu siyo shamba la bibi. Tuna sheria, lazima zifuatwe. Tusikubali kujigeuza kuwa a lawless country.
Take a deep breath and reflect on what your leaders are doing.

This is just one example of the confused state of affairs in this government.
This country now is a de facto "banana republic".
 
Imagine kifaranga kinapanda ndege wakati kuna member mwenzangu humu jambo kubwa alilofanya kuhusu ndege ni airplane mode
 
Tarehe 22/12/2022 saa nne usiku Wakaguzi wa Mifugo na Mazao yake walio katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA
Walijua macho yote yameelekezwa kwenye kubonyeza kitufe
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, Desemba 24, 2022

KUZUILIWA KUINGIA NCHINI KWA VIFARANGA 62,730 VYA KAMPUNI YA PHOENIX FARMS LIMITED VILIVYOFIKISHWA AIRPORT KUTOKA NCHI YA UBELIGIJI
Ndugu wanahabari,

Tarehe 22/12/2022 saa nne usiku Wakaguzi wa Mifugo na Mazao yake walio katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) walikamata vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited ya Mkuranga, Pwani vilivyofikishwa uwanjani hapo vikitokea nchini Ubeligiji bila ya kuwa na vibali vya kuingiza nchini vifaranga (Import permit) pamoja na cheti cha afya (animal health certificate). Vifaranga hivyo viko kwenye makasha (crates) 697 na stakabadhi ya mauziano (Invoice) ya mzigo inaonesha vina gharama ya shilingi 200,262,706 ambayo ni sawa na Euro 80,828.80 (Cost Insurance and Freight – CIF). Mkurugenzi wa Kampuni pamoja na Wakala wa Mmiliki wa vifaranga (clearing agent) hivyo walikiri kutokuwa na kibali hivyo kuwa amevunja Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 156 na Kanuni za Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN. Na. 28/2007.

Ndugu wanahabari,

Kulingana na kifungu cha 54(2) cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 156 kinakataza kuingiza nchini mifugo na mazao yake bila kuwa na kibali nanukuu; “No person shall bring or cause or permit allow to be brought into the country any animal product, contrary to any order or regulation prescribing the introduction of animal products into the country or without animal products inspected and certified in the prescribed manner.” Hivyo kwa kitendo cha Kampuni ya Phoenix Farms kutaka kuingiza nchini vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 ni kukiuka Sheria hii.
Ndugu wanahabari,

Aidha, Kanuni ya 26 ya Kanuni za Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN. Na. 28/2007 inabainisha kuwa, “Ikiwa wanyama au mazao ya wanyama yatafika nchini bila kibali na cheti cha afya ya wanyama au mazao ya wanyama, Mkaguzi aliyeko kwenye kituo cha ukaguzi azuie uingizaji wa wanyama au mazao ya wanyama husika nchini. In the event, of any animal or animal products intended for importation arriving without the certificate required as aforesaid, an Inspector shall refuse to allow such animal or animal products to enter Tanzania ….”.

Ndugu wanahabari,

Hivyo, kutokana na tafsiri ya vifungu hivyo viwili hapo juu, vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 walioletwa na Kampuni ya Phoenix Farms Limited waliopo katika Uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) upande wa mizigo (cargo) wamezuiliwa kuingizwa nchini kwa kuwa ni mzigo hatarishi. Aidha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeutaka uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Tawi la Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuielekeza Kampuni ya Phoenix Farms Limited kuvirudisha vifaranga hivyo nchini Ubeligiji kwa sababu wanaweza kuhatarisha usalama wa kuku nchini. Vilevile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited ameelekezwa kuviondosha vifaranga hivyo katika maeneo ya uwanja wa ndege na kuvirudisha alikovitoa.

Ndugu wanahabari,
  • Kama mtakumbuka, Mwaka 2006 Tanzania iliweka zuio (karantini) la uingizaji wa kuku na mazao yake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege duniani (HPAI). Kutokana na zuio hilo (karantini), nchi yetu imeendelea kuwa salama dhidi ya ugonjwa huo ambao umeathiri nchi nyingi duniani. Ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege huambukiza wanyama na binadamu na hutokea kwa njia ya mlipuko na kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifo vingi vya kuku na ndege wa porini. Njia za kudhibiti ugonjwa huu ni pamoja na kuzingatia usafi kwenye mabanda ya kuku (biosecurity measures) na karantini ya kuzuia kuingiza kuku, ndege wengine na mazao yao. Nitoe wito kwa watanzania wote hususan wadau wa kuku kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo ya kudhibiti kuingia na kuenea kwa magonjwa ya kuku nchini hususan Ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege ili kulinda usalama wa kuku, na ndege wengine pamoja na afya ya jamii ya watanzania kwa ujumla.
Asanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na
Profesa Hezron E. Nonga
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI
24 DESEMBA 2022
Huyu ndiye Waziri

…. Asanteni kwa kunisikiliza

Vichomwe moto. Wangejua wazungu wanavyochukia bidhaa zetu wala wasingepoteza muda zaidi ya kuwasha kibiriti.
 
Sheria ifuate mkondo wake viteketezwe kwa moto ....vinginevyo vitakufa ndani ya saa 24...siasa zimeingilia sheria.peleka kifaranga marekani uone kama hakitachomwa.kuna uhujumu mkubwa wa uchumi wetu...hapa nchini viwanda vinakosa soko na kuchoma bidhaa zake maana yake viwanda vitakufa na watu kukosa ajira na kodi.kwanini watu waruhusiwe kuagiza vifaranga nje ya nchi kiholela?kama ni vifaranga special basi walete mbegu au mayai yatotolweshwe kwa kutumia viwanda vya ndani.
 
Viongozi wetu kuwaelewa ni kazi sawa kampuni imevunja sheria lakini kwanini wasivipime hivyo vifaranga then kodi ikatwe na viruhusiwe kama vipo salama
Na wengine wakiwa wanaingiza kwa mtindo huo kutakuwa na haja gani ya kuwepo sheria?

Na kama wana vimelea huoni tayari ni hatari kwa mazingira waliyohifadhiwa?
 
Mkuu naomba unisaidie. Yule mama alivichoma vifaranga vyake kwa sabb gani haswa?
Ni kufikisha ujumbe kwa serikali kwa sababu ya mambo kama haya. Inaonekana umekuwa mchezo unaondelea na yule mama anajua mengi.
Ni wazi tumeshaingiza ndege wengu hadi sasa bila kufuata taratibu. Ukiangalia kwa sasa kuna mlipuko sana wa magonjwa ya mafua na vifua.
 
No Rais Samia alisema ilikuwa makosa kuchoma vifaranga vya kenya, je vya hawa wazungu atavichoma??? Au vitarejeshwa??? Kwa ufupi nchi yetu imekosa dira na muelekeo. Tukiwaambia ni mtu asiyekuwa na info ndiye atakuja kuwekeza Tanzania, nwenye uelewa atachagua na kujiuliza sana kabla ya kuwekeza
You are very right
Kuwekeza hii nchi inataka ujitoe fahamu.
Si nchi sahihi kwa mwekezaji makini.
Pana uovyoovyo mwingi.
 
Sheria inaweza kurekebishwa, yule bwana nilisoma habari yake, ni wazi hana connection/hajui biashara ya Tz, Mkuu unadhani biashara ya kuku imekuwa kwenye hali ile kweli ? Kila siku Bar kuku zinaliwa,Moshi pale mishikaki ya kuku wanauza mpaka buku

Ndio maana unaona huyu kaingiza kuku wote hawa anajua biashara ni nzuri , yule aliyechoma atakua hakuwa na pesa ya kuvilisha vile vifaranga labda, lakini angevifuga ilikuwa pesa ipo
Basi ukiona hivyo ujue kuna mmoja anabanwa kufuata taratibu zote ikiwemo kodi na mwingine anafanya atakavyo. Hapo kuna mkono wa wakubwa fulani. Hutosikua tena hiyo habari.
 
Back
Top Bottom