Serikalini watu tunaishi kwa kuiba; huu ndo ukweli

Serikalini watu tunaishi kwa kuiba; huu ndo ukweli

Bila wizi hii mishahara tusingeweza kufanya jambo lolote

Ndo maana walimu wanalia Sana ni kwa sababu hawana sehemu ya kuokota .

Hakuna MTU ambaye haibi wala kupiga dili .
Yaani umeongea ukweli. Wafanyakazi wengi ambao siyo waalimu ni mafisadi 100%. Waalimu wote kuanzia shule ya msingi mpaka chuo hawana vya kuiba.
 
Ukiona MTU analalamika ni kwakuwa Asali haijamfikia
Hiyo attitude yako inashida...Kuna watu asali zinawabubujikia lakini bado wanaona kuwa ni short lived kwakua hawezi kuwa kama kisiwa na pia unawaumiza wengi wakiwa hawana hiyo asali wakati wewe inakumwagikia tena bila kulazimisha
 
Ngoja niwambie ukweli .Serikali haina shukrani itakutumia kama kondomu ukuisha muda inakudampo. Tena unaweza kufanya mazuri mia moja ila kosa moja tu itakuadabisha. Kwahiyo jamani wewe ukijifanya mzalendo itafika muda wako wa kustafu utatoka na uzalendo wako.

Muhimu ni kwamba ukipata upenyo wa kupiga we piga tumia amri ya kumi na sita ya shetani inayosema "Usihurumie kiumbe ambacho haukukiumba".
Makanisani viongozi wanapiga sembuse serikalini.
Wewe jifanye mzalendo utakufa masikini na uzalendo wako.
Unataka serikali ikushukuru vipi? Wewe sio ndugu au mjomba wa serikali, unachotakiwa ni kutimiza majukumu yako kwa weledi na uaminifu ambapo mwisho wa mwezi unalipwa mshahara kwa kodi za Watanzania.
 
Sio wote waizi lakini
Ni hulka ya mtu na ukaribu wa watu ulionao
Kama utakuwa na majizi nawe utaiba
Malezi mabaya yanachangia na society yetu pia
Wala sio mishahara, mbona wenye vipato vikubwa ndio vinara wa kuiba? Wana shida gani hao?
Ni tabia zenu tu
 
Back
Top Bottom