Humu mna mada zinazozungumza hili japo kila mmoja kaelezea kwa namna anavyojua yeye ila hizi mada zimenijenga sana juu ya kuheshimu mahusiano yangu.
Hili jambo nilili-experience mwenyewe miaka 16 nyuma kipindi bado nafanya fanya ujana,kuna demu mmoja nilikuwa na mahusiano nae na nilikuwa nimeshakaa nae faragha mara mbili lakini mara zote nikitoka pale lazima nipatwe na tatizo,either nitapoteza cash kiasi kikubwa,nitapoteza mali ya mtu au nitampa mtu pesa mwisho ananiruka fut mia kwamba hatujawahi kuonana yaani alimradi vurugu.
Siku hiyo funga kazi nimemuita gheto jumapili nakazana kupiga show mara simu inaita,mara ya kwanza mara ya pili mara ya tatu nikaona nikapokee kupokea anapiga simu jamaa yangu jana yake tulipiga deal kumbe kimewaka ikaonekana tuliuza mali ya wizi so tunatafutwa jamaa ananiambia jifiche utakavyojificha ukikamwatwa usitutaje hamu ikaisha nikamruhusu aondoke baadae nikajisemea nimpigie jamaa yangu tuende beach (Coco) kipindi hicho naishi Sinza Mori akaniambia tukutane pale Bamaga kufika akaniambia bwana endesha chuma sijisikii vizuri ile tumebadilishana upande tu kwamba huyu ahamie huku huyu ahamie kule ile namalizia kufunga mkanda niweke D mara pembeni inapaki road patrol imejaa traffic kosa nimepita taa nyekundu.
Nikawaambia wazee mbona ndiyo kwanza nimekabidhiwa usukani na mwenzangu pia upande mnaosema tumetenda kosa siyo upande gari ilikotokea wakasema nabishana na mamlaka wakanipiga mabanzi kama mtoto kisha huyoo mpaka Mabatini police station pale wakasema huyu panapomfaa ni Oysterbay kilichoniokoa pale nilikuwa na mtu but still nililala nikatoka kesho yake mchana,haya mambo yapo aisee,au kuna Ile mtu anaoa anaanza kupoteza mali mwisho anapoteza na kazi yenyewe.