SGR Dodoma -Dar yaanza rasmi leo 25 July 2024 usiku huu

Glenn

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
69,329
Reaction score
164,730
Hatimaye SGR imeanza kazi rasmi kwa safari za Dodoma -Dar.

Watu wa viunga vya Dodoma wamechangamkia fursa cha kuvutia zaidi ni jengo la station kuu Dodoma, jengo lake limejenjwa mithili ya terminals za airport na lenye nakshi za taa nzuri za kuvutia.

Watu wa Dodoma nao wamechangamkia fursa kwa kukata tiketi kwa ajili ya kutumia usafiri huu ambapo usiku huu wamepanga foleni kwa ajili ya kupata huduma ya usafiri.

Sio vibaya tukampa shukrani mbeba maono na mwanzilishi wa huduma hii muhimu Mwenda zake Magufuli.

Rai yangu kwa viongozi wengine wajifunze katika hili nao wawe na moyo wa uthubutu.

Rais Samia unalo la kujifunza hapa.



Pia soma:
Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kagua SGR, Treni kuanza kufanya kazi Juni 14 (Dar-Moro), Julai 25 (Dar-Dom)
 
Mbeba maono Gani hamalizi kazi?
Issue ni utekelezaji bwana
Kwangu mimi Magufuli ndo nampongeza wengine waliishia kuongea tu
Mambo ya upembuzi yakinifu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…