Hatimaye SGR imeanza kazi rasmi kwa safari za Dodoma -Dar.
Watu wa viunga vya Dodoma wamechangamkia fursa cha kuvutia zaidi ni jengo la station kuu Dodoma, jengo lake limejenjwa mithili ya terminals za airport na lenye nakshi za taa nzuri za kuvutia.
Watu wa Dodoma nao wamechangamkia fursa kwa kukata tiketi kwa ajili ya kutumia usafiri huu ambapo usiku huu wamepanga foleni kwa ajili ya kupata huduma ya usafiri.
Sio vibaya tukampa shukrani mbeba maono na mwanzilishi wa huduma hii muhimu Mwenda zake Magufuli.
Rai yangu kwa viongozi wengine wajifunze katika hili nao wawe na moyo wa uthubutu.
Rais Samia unalo la kujifunza hapa.
View attachment 3051256View attachment 3051257View attachment 3051258View attachment 3051259
Pia soma:
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kagua SGR, Treni kuanza kufanya kazi Juni 14 (Dar-Moro), Julai 25 (Dar-Dom)