SGR hodi hodi Dodoma, masaa matatu unusu umefika

Huduma nzuri kama hii badala ya kuendelea kuboreshwa utashangaa baada ya miaka 2 inaanza kufa taratibu yale yale tu kama mwendokasi, kuna majitu huko wakiwemo wafanyakazi wanatafuta namna ya kuipiga sgr, ngozi nyeusi sijui imelaaniwa dah!
Miaka 2 mingi sana sema uchaguzi ukiisha, utaambiwa SGR inaenda service Korea
 
ivi kama unasafari ya dumila unashuka kituobgani uwai unapoenda au reli ipo mbali sa na eneo ilo
 
Saa kumi na mbili ratiba hapo juu,kama unataka lala lodge kaliakoo, hapo unasogea na bolt station ya SGR asubuhi, pia utafidia hiyo cost incentive kwa kuwahi kufika na kuepuka kula pale msamvu
 
Dar-Mwz saa 8Β½ litatoboa kabla halijaanza kugonga mifugo au na uzio tayari?
 
Ila hawa watu. Mwanzo ya Morogoro ilikuwa hivyo hivyo watu wakalalamika wakaweka saa tatu. Sasa kweli napand express kuna sababu gani ya kuamka saa 10? Basi hata waweke ingine saa tatu,nne au saa sita mchana.
Nadhani kwenye ratiba ndio tunachangomoto sana sijui huwa tuna fail wapi, saa 11 train inaondoka sasa inategemea unaishi wapi unatakiwa ufike saa moja kabla maana uwepo saa 10 Alfajir station sasa uamke labda saa 9 au saa 8 inategemea unaishi wapi, hapo utaingia gharama zingine usafiri wa usiku kwenda kituo na tunajuwa bei itakuwa juu sababu huna option nyingi za kukufikisha kituo.

Kuna haja ya hizi ratiba zilenge kufanya wepesi kwa wateja na kupunguza stress za mtu kuwaza niamke saa ngapi, usafiri alfajir nitapata kweli? je nikipata shida barabarani nitapata usafiri mbadala... Naomba TRC waje na ratiba ilyoenda shule na yenye ushawishi.
 
Watakua wamewalenga wafanyq biashara, wazee wa go & return
 
Saa kumi na mbili ratiba hapo juu,kama unataka lala lodge kaliakoo, hapo unasogea na bolt station ya SGR asubuhi, pia utafidia hiyo cost incentive kwa kuwahi kufika na kuepuka kula pale msamvu
πŸ˜€πŸ˜€ Ni ngumu kumlizisha kila mtu. By the way mradi ndo unaanza, Ratiba zitakua zinafanyiwa mabadiriko kulingana na mwitikio
 
Mbona mabasi yapo kuanzia saa 9 alfajiri mpaka 11. Kuna watu watapanda treni wafike dom mapemaa ili wawahi sehemu nyengine kwa haraka.
 
Mbona mabasi yapo kuanzia saa 9 alfajiri mpaka 11. Kuna watu watapanda treni wafike dom mapemaa ili wawahi sehemu nyengine kwa haraka.
Ma bus yapo muda wowote alfajiri saa 2, 3 4,5,6 mpaka saa 8 na usiku yapo option ziko zote hapa naongelea SGR na sijasema wafute alfajir ila waweke option zaidi ya moja hata mbili tu sawa.
 
Hiyo express mbona haina kugeuza siku hiyo hiyo?
 
Kati ya ndege na train ipi ina risk ndogo zaidi?
Ndege unafunga mkanda wakati wa kuruka na kutua, ukiwa angani safari inaendelea sio lazima kufunga, ndiomaana kuna hadi siti za kulala
 
Safi. Pongezi kwa kila aliyohusika kulifanikisha hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…