Ukiwa na akili utajua kwanini mtu kama magufuli aliukataa Mradi huu.Naamini nyuma ya mradi huu kuna kitu.Na siyo kitu cha Siri kwamba China inataka kujenga military base yake Tanzania ili kukuza kukontrol biashara bahari ya Hindi.Magufuli Rais ambaye anapenda miradi mikubwa eti aukatae Mradi muhimu kama huu wa Bandari?alafu usifosi Mimi nifikirie kama wewe.I am a free thinker. I always think out of the box.
Unaongea na mtu mwenye data na anayejua huo mradi kijana. Wacha ninyamaze.
Kuhusu uwepo wa Military base huo mradi sio sehemu ya huo mpango that is what I can assure you 100%.
Huo no mradi upo facilitated na serikali ya Oman wao ndio wanatoa pesa Kama financier kupitia exim bank ya China ambapo anayekopa ni China Harbors it's purely intended for business.
Haiingii kichwani China wakope pesa kujenga military base hii ndio nataka ufahamu. Military base huwezi kujenga kwa pesa ya mkopo, never. China Kama wangetaka kujenga Military base wasingekubali kuingia Joint Venture na serikali ya Tanzania kupitia TPA ambapo wanaform a company itakayosimamia Bagamoyo port.
Naomba uhusishe uelewa wako vizuri. Otherwise Kama huelewi as long haya maandiko yangu yanaishi humu JF basi tutakuja kujadili hatuhitaji kubishana sana but nakuhakikishia ishu ya Military base haipo kabisa.
Kama wangetaka kujenga Military base kwenye majadiliano lazima wangekuwepo JWTZ Kama wadau lakini wakati wa majadiliano wadau wote wa mradi ni TPA Kama mdau mkuu, TRL, EWURA, Marine Services, Exim Bank China, Ubalozi wa Saudia, Wizara ya Uchukuzi, Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo, Government Chief Valuer, EPZA na SEZ. Sasa where is JWTZ ambao ndio wadau wa military base???
Mambo mengine tunakaa kimya tu maana Magufuli alikuwa na ishu zake anazojua mwenyewe nisingependa kujadili hayo kwa sasa hayana maana uzuri wake majadiliano yameanza upya tunaanzia tulipoishia serikali imepitia na imeona hayo yote hayakuwepo.
Nachoweza kukuhakikishia ni kwamba mradi hauna hayo mnayoambiwa watu waliona hawajapata ganji yao na mkwere ndio aliusimamia ili watu wa jimboni kwake wafaidike nothing much.