SGR impacts kwa biashara ya mabasi yaanza kuonekana. Abood Bus kaamua kujiongeza

SGR impacts kwa biashara ya mabasi yaanza kuonekana. Abood Bus kaamua kujiongeza

Siku ya kwanza tuu Sgr imeasafirisha Abiria zaidi ya 900 kutoka Dar-Moro-Dom ambapo hapo ingekuwa ni zaidi ya Mabasi 15.

Baada ya kuona hivyo Kampuni ya Mabasi ya Abood wameamua kujiongeza na kuanza route Mpya ambazo hazikuwepo hapo kabla baad ya kupokwa tongue lake nono la Dar-Dom

View: https://www.instagram.com/p/C90pz0eN2Ia/?igsh=MXRycWRjbzk2bm9pcQ==

My Take
Ile Mikoa ilikuwa inapata Mabasi ya hovyo hovyo Sasa itapata Mabasi mazuri maana SGR imewatia adabu huko.

View: https://www.instagram.com/p/C91QayHK-y4/?igsh=M2Jibndnd2dvaTBz

Mabasi yatatumika na abiria wenye mizigo mikubwa
 
Hana jipya
Waziri wake wa ujenzi alikuwa Shukuru kawambwa hajufanya chochote akamhamishia Elimu nako hakuwa na jipya
Kwa kweli... Mipango kila mtu huwa anayo utekelezaji na uthubutu ndio tofauti.. Ampe maua yake anayestahili
 
Kama mwendo wa kobe alifilisiwa na wahindi, basi hata hizi tunazosema ni za kasi tutegemee waarabu watapewa tu.
 
Ni moja ya mradi bora kabisaa ila tu yasijekutokea ya Mwendokasii..!! mfumo wa kidigital kununua na kuscan ticket usifee maana wahuni sio watu wanaua hizo system kwa makusudi mapato yanaanza kupotea.. Kwa hili samia nampaa hekoooo
 
Tukishamaliza kupigia picha hiyo train basi balaa ndio litaanza na abood tutamtafuta wenyewe.
 
We mama una akili za kijinga sana, unafurahia as if Abood walikuwa wanavunja sheria kuwa na hiyo route!
 
Wameshindwa mabasi watawezaje treni ???????

Hazijaanza bado kuhitaji oil change na wheel alignment na bushing replacement...

Utasikia wanatafuta mwekezaji wa kuziendesha... Na kwaba vichwa vimepelekwa India kwa scheduled maintanance. Na huko geleji wamekuta foleni ya treni zingine.

Watanzania memory finyuuuuu....
 
Serikali inapaswa kuwa macho na hii huduma wa treni kwa maana maharamia wako wengi sana kwenye hii nchi wanaweza kuhujumu hii biashara ya SGR, kitendo cha wafanyabiashara wa mabasi kuingiliwa katika biashara hii ya abiria sidhani kama kimewafuraisha, serikali kama serikali wawe makini na hii huduma ya usafirshaji wa abiria kwa njia ya reli ya kisasa, leo Dom to Dar chuma inatembea masaa matatu, DAR TO MORO dakika 90, kwanini wenye mabasi wasichukie hiki kitu? Tunahitaji huduma na ulinzi madhubuti kwa ajili ya reli yetu, Hii reli kama ikitumika kwa malengo yaliyokusudiwa italeta ufanisi mkubwa katika maeneo ya kijamii, kiutamduni na kiuchumi katika Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom