SGR inapakia abiria wa Dar kushukia pugu na kuna malalamiko ya kukosa tiketi!

Mh sasa hiyo nayo kusema wa njiani na behewa lao mtawapa kazi watoa huduma.
Kama mkaguzi akiwa mmoja mbona sio usumbufu dada!?
Ikifanyika hivi walau hata wiki moja au mwezi italeta hofu watu hawatakua wakifanya huo ubadhilifu tena wakihofia kukaguliwa.
Mkagua tiketi awe mmoja kivipi? Kwamba hawana hela ya kuajili? Acheni kujilemaza akili. Umeleta mada yenye mashiko. Japo kosa lako ni kutotaka hao wa njiani wapande. Pengine kwenye ujenzi wa banda la abilia,ndo kuna changamoto. Kwa nini wasibuni au wanunue teknologia ya ku alert siti. Hii simple tu mbona. Waweke behewa la polisi. Akikamatwa mtu kavuka kituo,awekwe humo,arudishwe Dar,basi. Mpaka utakapopatikana utaratibu mwingine. Maana hata wo Dodoma anaweza akakata ya Morogoro
 
Hii imekaaje kwamba SGR inapakia abiria wa kutoka Dar kushukia Pugu halafu kuna watu wanaolalamika kukosa nauli za Dar kwenda Morogoro na Dodoma! Dar Kwenda Pugu si kuna ile treni ya Mwakyembe na Daladala? TRC inaelewa kweli inachokifanya?

Mimi nafikiri SGR kwa sasa ingewapa kipaumbele abiria wa ruti za Dar-Morogoro na Dodoma kwanza, waondoe ruti ya Dar-Pugu na wanaoenda vitu vya karibu kama Soga na Ruvu wakate tiketi masaa mawili kabla treni kuondoka, vinginevyo hizi taarifa za kwamba SGR inajaza sana itakuwa ni mbwembwe tu zisizo na mashiko.

View attachment 3071393
Nauli zipangwe kwa route, Dar to Moro Na Dar to Dom.
 
Zile tiketi waweke katika mfumo wa kuscan unapoingia kama pale stesheni unapojiandaa kuoanda treni, na unaposhuka unascan tena, ikiwa tiketi yako inaonesha mwisho ni ngerengere na umeshukia moro, basi inakugomea kutoka mule ndani inabidi ulipe nauli ya ziada. Ikiwa tiketi yako ni ya pugu na umeshukia dar, basi ushindwe kutoka mpaka ulipie kiasi cha safari uliyozidisha
Nafkiri hii ndo solution
 
Mkuu hili ndo suluhisho, wasipo fanyia kazi hili ndani ya mwezi mmoja, basi baada ya mwaka tutatafuta muwekezaji
 
Hawa majamaa wakamlipe Abood Kimbinyiko Klm Express etc wapate semina ni jinsi gani wana dhibiti tiketi za abiria wa njiani
 
Nje ya nchi huwa wanaenda kupiga picha tu? Huwa hawana cha kujifunza waendapo? Hawajaadapt mfumo?

Au ndio incompetent (kwa sauti ya Profesa Assad)
 
Mkagua tiketi awe mmoja kivipi? Kwamba hawana hela ya kuajili? Acheni kujilemaza akili. Umeleta mada yenye mashiko. Japo kosa lako ni kutotaka hao wa njiani wapande. Pengine kwenye ujenzi wa banda la abilia,ndo kuna changamoto. Kwa nini wasibuni au wanunue teknologia ya ku alert siti. Hii simple tu mbona. Waweke behewa la polisi. Akikamatwa mtu kavuka kituo,awekwe humo,arudishwe Dar,basi. Mpaka utakapopatikana utaratibu mwingine. Maana hata wo Dodoma anaweza akakata ya Morogoro
Hujaelewa mkuu pia umechanganya sana mada.
Kama umefuatilia mlolongo wa wa mjadala nilisema kuwa vituo vya njiani ni muhimu kwasababu havitumiki tu kushukia wapo wanaopandia Pugu ambao ni wakazi wa Gongo la mboto,huwezi ukamwambia aende Posta ilhali Pugu ipo karibu.
Ila waweke wakaguzi wa tiketi katika kila behewa awepo mkaguzi mmoja ILI KUONDOA DISCOMFORT.
Yani kila behewa moja mkaguzi mmoja,sio kama kwenye treni za Mgr behewa moja wakaguzi 6-7 inaleta kiusumbufu fulani na kuleta discomfort.
Ila kama ukiweka mkaguzi mmoja katika kila behewa moja sio tabu.
Laa sivyo kituo cha karibu zaidi Pugu wakati wa kutoka Dar kiwe cha kupandia na wakati wa kurudi kiwe cha kushukia.
 
Kuweka vituo vya Pugu,Msoga na Ngerengere sio kosa mkuu.
Ila kama ni hivyo itatakiwa uwepo ukaguzi wa tiketi kama ilivyo kwenye metre gauge.
Maana kwenye metre gauge huwa kila baada ya muda kituo kikifika tiketi inakaguliwa na kama tiketi huna ama umevuka kituo unachajiwa pesa.
Haina namna itabidi iwe hivyo.
Kwasababu wapo wanaopandia Pugu ambao ni wakaazi wa Gongo la mboto,ukisema ukitoe itakua mtihani.
Japo suala la kukagua tiketi kila mara nalo kidogo laweza likaleta discomfort fulani ila lifanyike kiustaarabu tu,kila behewa moja mkaguzi mmoja anatosha,na zikaguliwe kila baada ya kuvuka kituo kimoja.
Kukazia hoja yako, wangetoa ticket zenye rangi. Kila kituo na rangi yake. Pengine ingesaidia.
 
Hii imekaaje kwamba SGR inapakia abiria wa kutoka Dar kushukia Pugu halafu kuna watu wanaolalamika kukosa nauli za Dar kwenda Morogoro na Dodoma! Dar Kwenda Pugu si kuna ile treni ya Mwakyembe na Daladala? TRC inaelewa kweli inachokifanya?

Mimi nafikiri SGR kwa sasa ingewapa kipaumbele abiria wa ruti za Dar-Morogoro na Dodoma kwanza, waondoe ruti ya Dar-Pugu na wanaoenda vitu vya karibu kama Soga na Ruvu wakate tiketi masaa mawili kabla treni kuondoka, vinginevyo hizi taarifa za kwamba SGR inajaza sana itakuwa ni mbwembwe tu zisizo na mashiko.

View attachment 3071393
Wizi wa wananchi alafu serikali inalaumiwa kumbe kila mtu mwizi
Sio kiongozi wala raia wote wezi
Ndio maana nasema kikubwa amani
Maisha kila mtu apambanie
 
Issue ndogo inafunguliwa thread zaidi ya kumi. Hio ni kazi ya TRC kukagua tiketi. Sio issue ya kitaifa.
 
Hii imekaaje kwamba SGR inapakia abiria wa kutoka Dar kushukia Pugu halafu kuna watu wanaolalamika kukosa nauli za Dar kwenda Morogoro na Dodoma! Dar Kwenda Pugu si kuna ile treni ya Mwakyembe na Daladala? TRC inaelewa kweli inachokifanya?

Mimi nafikiri SGR kwa sasa ingewapa kipaumbele abiria wa ruti za Dar-Morogoro na Dodoma kwanza, waondoe ruti ya Dar-Pugu na wanaoenda vitu vya karibu kama Soga na Ruvu wakate tiketi masaa mawili kabla treni kuondoka, vinginevyo hizi taarifa za kwamba SGR inajaza sana itakuwa ni mbwembwe tu zisizo na mashiko.

View attachment 3071393
Hao hao watendaji wa Sgr ndio wahujumu
 
Back
Top Bottom