Kama kawaida dereva kakwepesha kwake, kamtoa kafara konda wake
Kuhusu kuwa Dereva kapeleka upande usio wake ili agonge hapo nakataa.
Jinsi nilivyoona hizo picha na jinsi lori lilivyokuwa limesimama ni kuwa Lori liliharibika na kusimama barabarani bila kuwekwa pembeni.
Upande lliliposimama ndio upande ambao Shabiby ilikuwa inapita(gari zote gari zilikuwa zinaelekea Magharibi halafu ilikuwa usiku).
Dereva wa Lori hakuwa na Alama ya triangle([emoji3544]) badala yake akasimama nyuma na kawasha tochi kama ishara ya kuonesha hali ya hatari.
Kitendo kile cha kuonesha tochi hakikumpa Dereva Shabiby ishara ya kuelewa pindi alipokuwa anaendelea na safari akifikiri hamna tatizo. Ghafla baada ya kukaribia huku akiwa kwenye mwendo ndipo akagundua kuwa Lori limeharibika na lipo njiani.
Kwenye juhudi za kulikwepa kwa kutaka kupita upande wa kulia ikawa imeshindikana na kumgonga Dereva wa Lori aliyekuwa amesimama nyuma ya Lori na kuwasha tochi.
Sasa hizo juhudi za kutaka kulikwepa Lori kwa haraka ili apite upande wa Kulia ndipo akaligonga Lori kwa kutumia upande wa karibu na Konda anapokaa/simama. Kama angetaka kulikwepa Lori kwa kupitia kushoto, hapo angegonga kwa upande wa kulia alipo yeye na Bus huenda lineangukia mtaroni. Hii ilikuwa risk sana na kama angefanya hivi tungekuwa tunazungumza habari zingine sasahivi.
NB: Sikuwa kwenye eneo la tukio ila kwa kuona picha na kupata simulizi chache, huo ndio mtazamo wangu.