Shabiki maarufu wa Simba Nabii Meja atangaza kuhamia Yanga rasmi

Shabiki maarufu wa Simba Nabii Meja atangaza kuhamia Yanga rasmi

Ukimsikiliza huyu jamaa ugundua kwa haraka tuu dishi limeyumba na watu aina hiyo lazima wakimbilie ngedere fc
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Kwa mnaotazama na kusikiliza EA radio na EATV muda huu, Huyu aliyekuwa shabiki kindakindaki wa simba ametangaza rasmi kuhamia Yanga.

Karibu sana kwenye kambi ya ushindi, Karibu kwenye kambi ya makombe! Karibu kwa MABINGWA! Kila mtu huzaliwa mwananchi ni ujeuri tu na kukengeuka huwapeleka kwingine😄

Ni suala la muda Mo dewji naye ataunga mkono juhudi.

View attachment 3070590View attachment 3070591
Shabiki wa ukweli hahami timu
 
Anajiita Nabii Meja, huwa anashiriki kwenye kipindi cha michezo East Africa Radio, kinachoanza saa 6 kamili mpaka saa 7 kamili mchana. Huyo jamaa huwa ni mtata na ana misimamo sana, ninapata ukakasi kama amehama kwa dhati kabisa.
Narudia tena Shabiki wa ukweli hahami timu labda kuna dili la hela amefuata. Pamoja na Arsenal kukosa kombe kwa zaidi ya miaka 20 lakini sijawahi kufikiria kuhama, hiyo ni timu ya ughaibuni ambayo nimeijulia kwenye screen tu sembuse timu nimekuwa naiona na kuipenda nihame kwa kukosa ubingwa miaka mitatu tu?
 
Hilo linajulikana kuwa atakuwa ana maslahi sehemu ndo maana amehama. Arsenal na mimi ni chama langu, kuna kipindi nilijiapiza sitoifutilia tena ila nikashindwa kujizuia mpaka sasa nimeizoea naishi nayo hivyo hivyo.
 
Anajiita Nabii Meja, huwa anashiriki kwenye kipindi cha michezo East Africa Radio, kinachoanza saa 6 kamili mpaka saa 7 kamili mchana. Huyo jamaa huwa ni mtata na ana misimamo sana, ninapata ukakasi kama amehama kwa dhati kabisa.
Kama ana misimamo why ahame timu? May be amefanya komedi. By the way kile kipindi nikishindwa kukisikiliza huwa naona wanafanya vurugu tuu na ubishi bila kusikiluzana.
 
Kama ana misimamo why ahame timu? May be amefanya komedi. By the way kile kipindi nikishindwa kukisikiliza huwa naona wanafanya vurugu tuu na ubishi bila kusikiluzana.
Hata mimi niliacha kukisikiliza kile kipindi ni fujo ty mwandaaji uwezo wake wa kubuni umeishia kuwaita watu wale wale wafanye malumbano na wengine unaona kabisa hata mchezo wa mpira wenyewe hawauji ni washabiki oya oya tu
 
Hata simfahamu, alikuwa maarufu kijijini kwao huyo.
 
Fala tu huyo, ana masifa ya kijinga, japo sometimes anaongea points.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Ni ngumu sana kuhama timu labda kama haipo kabisa au imeshuka daraja hapo kidogo afadhali.

Sasa unahamia Yanga upepo mzuri ukigeuka unarudi Simba.
Shabiki malayamalaya (kwa sauti ya J.K.N)
 
Back
Top Bottom