Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!
Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!
Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!