Seif tutamkumbuka,kwa tabia ya uongoNaliona la muhimu, Hili letu kuridhia,
Kapambana Maalimu, Zenji kaipigania,
Akamwage yake damu, ndicho kilichobakia?
Sefu kawapigania, nyie mmemsaliti!
Akapumzike Sefu, ale sasa kuku wake,
Huyu bwana si dhaifu, alipenda nchi yake,
Kwa hakika amekifu, kuwa wewe naye wake?!
Kwa nini alipigana, eti kuwa hamjui!
Aliye wapigania, kaachwa kwenye mataa,
Wengine mwamchukia, Hamjui yuafaa,
Mawaziri ulizia, nyote amewakataa,
Mtamkumbuka Sefu, Gwiji lile la Zanzibar!
Leo Zanzibar mkoa, macho mmeyatumbua,
Mawaziri mmenoa, Hivi mnajitambua?
Sefu angewaokoa, nchi wakaitambua,
Ilikuwa yarejee, ya wasisi wa Mwungano!
Anapenda kucharuka,wakati moyoni fyongo
Siyo wa kuaminika,fitina mwenye mipango
Cheo alikitamani,kwa nadhiri ya mandevu.