Senzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Senzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?
Kwangu mimi ni Unguja,nyumbani kwao HusseinSenzighe nyumbani wapi, Chatto au usukuma?
Makubwa hayo ni kupi, Au kwenye lile chama?
Kipaumbele ni kipi, ndege au wakulima?
Haya ya vyuma kukaza, leo ndiyo kusikia?
Kwangu mimi ni Unguja,nyumbani kwao Hussein
Hata bara ninakuja,kuyajenga ya chamani
Mojamoja sitataja,nikukabidhi ilani ?
Siraaj ng'aza siraat,tuondokwe na ghururi. I
Senzighe mnufaika, wa lile chama dhalimu!
Umekiri kwa hakika, kumbe kwako SiSi emu!
Kwenu kitu kusikika, hadi iwatoke damu!
Ama kweli mwenye shibe, ajuweje
Sitaapa kwa mitini,wala kwa mizaituniSenzighe mnufaika, wa lile chama dhalimu!
Umekiri kwa hakika, kumbe kwako SiSi emu!
Kwenu kitu kusikika, hadi iwatoke damu!
Ama kweli mwenye shibe, ajuweje wenye njaa!
Hahaha hii ndo inaitwa ngumi ya chembeSenzighe mnufaika, wa lile chama dhalimu!
Umekiri kwa hakika, kumbe kwako SiSi emu!
Kwenu kitu kusikika, hadi iwatoke damu!
Ama kweli mwenye shibe, ajuweje wenye njaa!
Unaipenda na unaijua, professional yako, I like it! Ongeza ubeti wa pili sasa unisifu na mimi kwa kukuonyesha mahali ambapo wewe hukuwa umepaona, nimepaona mimi wakati mimi ni laymanAlijikwaa malenga, uzuri hakuanguka,
Kwamba hakuweza lenga, ni gwiji huyu kumbuka!
Beti saba kazipanga, kwa hakika mtukuka,
Mizani iliyo paa, haimkwepi kombora!
Cc: missile-of-the-nation
Unaipenda na unaijua, professional yako, I like it! Ongeza ubeti wa pili sasa unisifu na mimi kwa kukuonyesha mahali ambapo wewe hukuwa umepaona, nimepaona mimi wakati mimi ni layman
Sitaapa kwa mitini,wala kwa mizaituni
Manufaa ni ya nini,chama kwetu ni imani
Tajiri na masikini,wote sawa kwa mizani
Ni mlezi wa wanyonge,ng'ara CCM ng'ara.
Nawashukuru malenga, nyote mliochangia
Mmesema ya kujenga, kukanya na kuusia
Hakika mmejipanga, Fani maudhui pia
Asante sana vipanga, Saluti nawapigia
Nyundo mmegongelea, kulinda demokrasia
Usaliti kuulea, si nzuri hiyo tabia
Kama msingeongea, Chadema ingejifia
Asante sana vipanga, saluti nawapigia
Tusisahau Mnyika, Na kamati kuu pia
Msimamo walishika, kuuondoa udhia
Wasaliti walitaka, kuipenyeza rupia
Asante sana vipanga, Saluti nawapigia
Ninaitua kalamu, wino umeniishia
Si kwa mwisho umuhimu, mkono kuwapungia
Mabingwa wataalamu, kofia nawavulia
Asante sana vipanga, saluti nawapigia
Stori za mbowe nahao makamanda wake inanikumbusha zile stori za kibwetele nawaumini wake. Wote wanaakili zinazofanana
Ndiyo chama kilekile,cha Nyerere juliasiChama hiki SiSi emu, ndicho kile cha Nyerere?
Au mnacheza gemu, kwani bora cha Mkwere!
Hiki cha hii awamu, madereva ni ngedere?
Kutwa kucha kukwapua, mkitaka mnauwa!
Ndiyo chama kilekile,cha Nyerere juliasi
Sera zake zilezile,za kukataa uasi
Ngedere ni kwenu kule,Vibaraka majasusi
Kama hambadliki ,dola kwenu marufuku
Astaghfirullah laadhim,Ashakum vina vyakoCCM ya Nyerere, Siyo hii m-Senzige!
Hata ile ya Mkwere, haikuwa ya kis*nge!
CCM ya ngedere, ni hawa hiki kilinge!
Leo tuna matabaka, awali hayakuwapo!
Umeyasema mwenyewe, sisi daraja la pili,
Ati ili kuwa yawe, hadi nyie mkubali!
Kwani nyie ni wenyewe, au lau madalali?
Kwamba dola marufuku, dawa yenu yachemka!
Watayamaliza. Mark my wordsWanaenda fungua kesi mahakama itazuia kufutwa kwao sababu kesi inasikilizwa na kesi itaenda mpaka 2025 na baada ya hapo wataenda sisiemu, loser ni chadema! Mdee, bulaya, matiko wana influence kubwa sana kwa kina mama, ambao ndio wapigaji kura wakubwa..
Astaghfirullah laadhim,Ashakum vina vyako
Lugha stara muhim,tughani yenye mashiko
Mwajitoa ufaham,kwenu mmekosa miiko
Eti mnata dola ,midomo yenu michafu.
Dola gani mnataka,kwanza nendeni jandoni
Wawatoe majitaka,adabu wakufunzeni
Mkirudi mnawaka,akili zimesheheni
Bado hamjakomaa,saizi yenu mitaa.
Haki hampati katu,kama hamna adabuYa Nyerere siyo hii, ati sisi au nyie,
Mnatutaka utii, hata mkatufukie?
Ya kuwa hatuingii, masikio msikie,
Sisi daraja la pili, staha ipi mwataka!
Staha ipi mwataka, sisi daraja la pili?
Haki zetu twazitaka, hili kwa hali na mali,
Ni ya umma madaraka, sote tunastahili,
Kenge kwenu kusikia, mtoke damu sikio!
ndan ya miaka 15 ntakua waziri mkuuAmeunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Nchi imekuwa dampo, La uchafu wa wahuni!
Mambo wayafanya simpo, Kiburi cha Firauni
Wamejifanya madompo, hawamuogopi nani!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Aibu yetu au yao?, Huu ni msala wao!
Wasaliti wana chao?, Chao ni ujinga wao!
Wameuza utu wao, Kwa uchu tamaa zao!
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Wananchi tunaona, Wananchi tunajua!
Hadaa tumeziona, Inda tunaitambua!
Mambo yao konakona, Akili zao vibua
Hongera sana Mbowe, wewe ni mtu makini!
Wewe umeona wapi, Dhulma ishinde haki?
Kwenye mwanga saa ngapi, Giza likatamalaki?
Maono yao mafupi, Kama yale mafataki.
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hima sasa wananchi, Kamanda kaweka sawa
Hila zote kazipanchi, mambo sasa sawasawa
Hadaa kapiga tochi, wamebaki kupagawa
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini!
Haki hampati katu,kama hamna adabu
Akili zenu fyatu,kila siku majaribu
Mtavisaga viatu,Ufipa hadi bububu
Hamtapata kitu Ng'o,mtakaa msubiri.