Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais Samia kwa kutembelea nchi 22 kwa awamu 25 kwa muda mfupi ndio sababu ya kuimarika huku kwa Uchumi wa Tanzania

View attachment 2407619

Dar es Salaam

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa Taifa ikiwemo kufungua matumaini mapya, furaha na mwanga wa maendeleo kwa wananchi.

Shaka ametoa pongezi hizo leo Novemba 5,2022 wakati wa Kongamano maalum la kumpomgeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania katika maendeleo ambalo limeandaliwa na Jukwaa Jamii Mpya .

“Uongozi wake umefungua matumaini mapya kwa Watanzania, furaha na mwanga wa maendeleo kwao. Lengo kuu la Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ni kumkomboa mwananchi kutoka katika wimbi la umasikini. Katika kipindi chake cha Mwaka mmoja na miezi minane tunampogeza Rais Samia kwa kuimarisha diplomasia yetu kwa mataifa jirani na mataifa ya nje katika sekta za kiuchumi na kisiasa.

“Rais Samia amezitembelea nchi takribani 22 hadi sasa, nchi yetu imeendelea kufunguka kiuchumi kupitia biashara na nchi za nje. Takwimu za hivi karibuni zimerekodi ongezeko kubwa la mauzo ya nje kwa bidhaa na huduma za Tanzania katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki,” alisema.

Ameongeza takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya nchini Kenya (Kenya National Bureau of Statistics) zimeonesha kukua maradufu kwa mauzo ya Tanzania katika nchi huiyo kwa takribani sh. bilioni 20.5 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2021/2022 kutoka sh. bilioni 10.8 kwa mwaka uliopita wa 2020/2021.

“Nitumie fursa hii pia kumpongeza Rais Samia kwa ziara yake ya China ambayo imehitimishwa Novemba 4, Novemba, 2022. Tumeshudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa ikiwemo ya biashara, uwekezaji, uchumi wa kidigitali, masuala ya mazingira, uchumi wa buluu na kubadilishana uzoefu katika nyanja ya sayansi na teknolojia,” amesema.

=====
 
Kazi nzuri Sana Bwana Shaka Hamdu
 
Bado Nchi Ngapi Awe Amemaliza Zote Hapa Duniani?
 
Back
Top Bottom