Shaka Hamdu Shaka atuma neno kwa Freeman Mbowe amsifu Rais Samia

Shaka Hamdu Shaka atuma neno kwa Freeman Mbowe amsifu Rais Samia

Kwani kwa mujibu wa kesi ya Mbowe anayemfanyia fujo mwingine ni nani! Ili tuheshimike ndani na nje ya nchi vijana viongozi wa baadaye mjifunze na kuzoea kutafuta na kusema ukweli. Ukweli ndiyo utawaweka huru,utawapa amani na maisha marefuu!!
Daaah,
 
sijaelewaga hadi leo kwanini sisiemu waliamua kumuweka huyu jamaa kama kiongozi wao.

Hata sijui kwanini.
 
View attachment 2140146

"Ibara ya 118 ya ilani ya uchaguzi ya CCM inaeleza Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuheshimu na kulinda misingi ya demokrasia na haki za binadamu kwa ajili ya kudumisha umoja, amani na ustawi wa Taifa kwa kuzingatia Katiba ya Nchi"

"Namshkuru Mhe Freeman Mbowe kwa kuonesha uungwana kwa sababu amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali na amemuahidi kumpa ushirikiano kwa ustawi wa Tanzania. Hiyo ndio siasa safi na hiyo ndio Tanzania tunayojivunia"

"Chama Cha Mapinduzi kinawahakikishia watanzania kuwa kitaendelea kuisimamia Serikali izidi kuimarisha Uhuru wa maoni, misingi ya haki na demokrasia ili kujenga taifa lenye upendo, umoja, amani na mshikamano wakati wote."

"Siasa safi inahusisha uzalendo, utu, heshima na kuweka mbele maslahi ya Taifa kuliko chochote. Rais Samia ni kielelezo katika hili na ameendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijenga Tanzania moja yenye ustawi kwa wananchi wote. Tumpe ushirikiano."

" Lengo la CCM katika kipindi hiki ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata haki kwa mtu mmoja mmoja na makundi
mbalimbali. Tunampongeza Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza maelekezo haya ya ilani kikamilifu hakika Kazi inaendelea vyema."

Hakika kwa sasa ccm-tanzania ina msemaji anayezungumza kwa hekima,akili,busara,Utu na Utulivu na anazungumza vitu vinavyoeleweka kama Msemaji Wa Chama Tawala, Heko Mhe Shaka Hamdu Shaka kwa kukibeba na kukiheshimisha vema Chama Chetu

View attachment 2140126
05 Machi 2022
Gymkana, Dar Es Salama
#366zaSamia
#KaziKubwaImefanyika
#KaziIendelee

<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Huyu kijana anaelekea kwenye njia ile ile yakina Polepole.....!!
 
Back
Top Bottom