Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
CCM yasema haina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu, kipaumbele chake ni kujenga nchi.

- Wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi.

"CCM haina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda na kuheshimu haki za binadamu"SHAKA.

=====

1623735786414.png
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuboresha huduma za kijamii, kuboresha mazingira ya biashara, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda sambamba na kuheshimu haki za binadamu, hivyo hakiwezi kuacha masuala hayo ya msingi yaliyobeba mustakabali wa Taifa na kuanza kurudi nyuma kimaendeleo kwa maslahi binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wazee mbalimbali wa wilaya ya Tanga mjini katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Tanga.

"Hakuna mwananchi anayesema serikali iyaache yote hayo ishughulike kwanza na katiba mpya hayupo. Madai ya katiba mpya sio agenda ya kisiasa hivyo wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi kuwa hilo ndio jawabu la changamoto zao jambo ambalo sio kweli" alisema Shaka.

Shaka amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia inakimbizana na vipaumbele vya msingi zaidi katika maeneo mtambuka ya upatikanaji wa huduma bora za afya, utoaji wa elimu bure na bora mashuleni na vyuoni, huduma za maji safi na salama zikiimarishwa katika maeneo hasa yasiyo na huduma hiyo, kuimarishwa kwa mfumo wa utoaji haki, kutoa mikopo ya riba ndogo na masharti nafuu, kuboresha kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao sambamba na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji.

Aidha, Shaka amesisitiza kuwa Taifa linahitaji viongozi waadilifu, wazalendo, wanaothamini utaifa wetu, wanaotanguliza na kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuwanufaisha wananchi sio wanasiasa mahiri wa propaganda za kutafuta ushawishi wa kutafuta kuungwa mkono kisiasa bila kujenga misingi madhubuti.

ZAIDI SOMA...

CCM YAVUNJA UKIMYA KUHUSU KATIBA MPYA.

~Yasema kwa sasa sio kipaumbele chake.

~Yajielekeza katika kujenga nchi kwanza

Na mwandishi wetu Tanga.

Chama Cha Mapinduzi kimesema hakina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuboresha huduma za kijamii, kuboresha mazingira ya biashara, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda sambamba na kuheshimu haki za binadamu.

Hivyo hakiwezi kuacha masuala hayo ya msingi yaliyobeba mustakabali wa Taifa na kuanza kurudi nyuma kimaendeleo kwa maslahi binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee mbalimbali wa wilaya ya Tanga mjini katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Tanga.

Amefahamisha kuwa serikali ya ya Rais Samia inakimbizana na vipaumbele vya msingi zaidi katika maeneo mtambuka ya upatikanaji wa huduma bora za afya, utoaji wa elimu bure na bora mashuleni na vyuoni, huduma za maji safi na salama zikiimarishwa katika maeneo hasa yasiyo na huduma hiyo, kuimarishwa kwa mfumo wa utoaji haki, kutoa mikopo ya riba ndogo na masharti nafuu, kuboresha kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao sambamba na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji huku mkazo zaidi ukielekezwa katika kukomesha rushwa na ubadhirifu jambo ambalo litasaidia katika matumizi yenye tija ya utajiri wa nchi kupitia rasilimali zake.

"Hakuna mwananchi anayesema serikali iyaache yote hayo ishughulike kwanza na katiba mpya hayupo. Madai ya katiba mpya sio agenda ya kisiasa hivyo wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi kuwa hilo ndio jawabu la changamoto zao jambo ambalo sio kweli" alisema Shaka

Shaka alibainisha kuwa Taifa linahitaji viongozi waadilifu, wazalendo, wanaothamini utaifa wetu, wanaotanguliza na kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuwanufaisha wananchi sio wanasiasa mahiri wa propaganda za kutafuta ushawishi wa kutafuta kuungwa mkono kisiasa bila kujenga misingi madhubuti ya taasisi zao za kisiasa zinazotumika kubeba agenda hizi za wananchi.

"Watu wasipotoshe, Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya uliendeshwa na ulifikia hatua ya Katiba inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo inasubiri kupigiwa kura ya maoni na wananchi pale ambapo serikali itaona inafaa kukamilisha mchakato wake hivyo upinzani uache hadithi za kusadikika. Huu ni wakati wa kujenga nchi kwanza kazi ambayo CCM inaifanya baada kuaminiwa na watanzania" Alibainisha Shaka

Hata hivyo katibu huyo wa itikadi na Uenezi Ndugu Shaka amekumbushia kuwa hata vyama vya MCP, KANU na UNIP viliondolewa madarakani kwa katiba ile ile na baadae MCT cha Malawi kikarudi tena madarakani kwa katiba ileile kutokana na uamuzi wa wapiga kura wala sio kwa katiba mpya au ya zamani kwani kinachoweka chama madarakani ni sera bora, utekelezaji madhubuti, na uwezo wa kuwaunganisha wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu kwa usawa kama ifanyavyo CCM.

"Hata ukiangalia hoja ya suala la tume huru ya uchanguzi nalo ni jambo la kikatiba ndio maana CCM inaendelea kushangaa upinzani wanavyozungumzia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kama ajenda mbili tofauti utadhani katiba ni jambo jingine na tume ni jambo jingine. Tume ya uchaguzi ipo kikatiba na haijawahi kubadilishwa, ni tume hiyo hiyo iliyowapa madiwani, wawakilishi na wabunge kwa zaidi ya miaka 20 tena hata wakati mwingine wakiongezeka kwa idadi ajabu tume hiyo hiyo wanataka iwe huru, sasa sijui ni uhuru upi wanautaka labda wanataka waiongoze wao japo bado watashindwa chaguzi maana hawataki kukubali wana vyama vya siasa dhaifu!" alisema Shaka.
 
Mwenyekiti wa chama ni mama Samia. Je, maamuzi haya wameyafanya wote?
 
CCM yasema haina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu, kipaumbele chake ni kujenga nchi.

-Wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi.
Miaka 60 tunajenga nchi kwa kutumia mifuko ya cement nyingi bila kuchanganya na mchanga ili ratio I we sawa.

KATIBA si mda mfupi tu kuna hasara gani kwa vyama vya siasa. Pia kwenye maendeleo ni wananchi siyo vyama
 
CCM yasema haina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu, kipaumbele chake ni kujenga nchi.

-Wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi.
Hiyo kauli katoa mpuuzi gani? Anaitwa nani? Au umeleta propanga? CCM ni genge la wahuni waliong'ang'ania madaraka na kupoka haki ya Watanzania milioni 60
 
Miaka 60 tunajenga nchi kwa kutumia mifuko ya cement nyingi bila kuchanganya na mchanga ili ratio I we sawa.
KATIBA si mda mfupi tu kuna hasara gani kwa vyama vya siasa.Pia kwenye maendeleo ni wananchi siyo vyama
Nchi inajengwa miaka yote. USA mpaka sasa wanajenga nchi yao. Wanajenga barabara, hospitas nk.
 
Lile bunge lililoibuka na kitu inaitwa Ukawa, walituingiza chaka sana,

sasa hii miradi mingi ya sasa, serikari itafute pesa tena ya bunge la katiba? hii nadhani hata angelikuwa Mbowe angeligomea tu!
 
CCM yasema haina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu, kipaumbele chake ni kujenga nchi.

-Wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi.
Kwa hiyo CHADEMA wamepewa jibu rasmi kuanza kampeni yao kutafuta Katiba mpya kupitia kwa wananchi!
 
Vijana wa bodaboda mixer makushabu.

Iandikie hioooo.
 
Hawa jamaa sijui huwa wanatuonaje? Sijui hii nchi walishajimilikisha? Katiba sio takwa la Chama bali ni la wananchi sasa hiki Chama kinataka kutufanya sisi ni mafala wanaamua kusema au kufanya wakitakacho,huu ni uzandiki wa hali ya juu!
 
Back
Top Bottom