Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Mh! Tatizo suala la katiba mpya linashikilia bango na wanasiasa. Wanasiasa hujali maslahi ya kwanza iwe ni CHADEMA ama CCM, kwani watanzania tunasemaje? Mimi kama mtanzania mmojawapo naona ipitishwe kura ya maoni, tujue tunataka katiba mpya au tujikite na maendeleo?

Tatizo mchakato ukianza wasiasa huumiliki, maelezo ya shaka inaonekana kayatoa kama mwanaCCM na si kama mtanzania. WanaCDM na WanaCCM wote ni Watanzania lakini sio Wote watanzania ni Wanachadema ama CCM! Kati ya hivi vyama viwili vikubwa vinalipa suala la katiba mpya na tume huru uzito tofauti. Wananchi tunashangaa, kama kawaida yetu tunavuma na upande unaovuma-hili ni tatizo.

Hili si suala la CCM wala CHADEMA inatakiwa Watanzania tuulizwe “mnataka katiba mpya ama vipi?” lisiwe suala la wanasiasa!
 
Chadema bwana,wao wanaamin katiba mpya itawapeleka ikulu.

Pole Sana ninyi chadema,binafsi siungi hoja ya kuwa na mjadala wa katiba mpya ,iliyopo idumu hata miaka elfu moja
Jikite kwenye hoja Chief chadema imeingiaje?
 
Inashangaza sana kusikia kiongozi kama huyu anatamka maneno kama haya bila hata aibu. Kuwa eti taifa letu halihitaji katiba mpya? Mbona hata mwl Julius Nyerere alishawahi kusema kuwa hii katiba ya JMT ya mwaka 1977 ina mapungufu!

Achana na mapungufu ya kumpa raisa madaraka ya kuwa kama mfalme. Taifa letu lina raia wa kila aina. Wengine sio wanasiasa. Hivyo hitaji la katiba mpya sio kwa ajili ya vyama vya siasa pekee kushika dola.

Kuna uvunjifu wa haki za binadamu ambazo zinaathiri kila mtanzania kwa namna moja au nyingine. Hapa lazima watanzania wapate katiba mpya ili kudhibiti uvunjifu wa haki za binadamu.

Kwa ujumla katiba mpya ni hitaji linalogusa kila mtanzania sio wanasiasa tu pekee.
 
Mi nkadhani ni yule shaka kama shaka nguli mtangazaji wa VOA kumbe ni huyo ngumbaru
 
Inashangaza sana kusikia kiongozi kama huyu anatamka maneno kama haya bila hata aibu. Kuwa eti taifa letu halihitaji katiba mpya? Mbona hata mwl Julius Nyerere alishawahi kusema kuwa hii katiba ya JMT ya mwaka 1977 ina mapungufu!..
Unaonaje kwa sasa badala ya katiba mpya hayo maeneo yenye mapungufu yakafanyiwa marekebisho
 
Halafu akija rais mwingine akaamua kuuza miradi yote hiyo mnayoita mikubwa msilalamike kwa kuwa katiba inampa uwezo huo tena bila kushauriana na yeyote na hata akishauriana naye si lazima achukue ushauri wake.
 
CCM says it has no constitutional agenda currently.

June 14, 2021. TANGA.

CCM has said it does not have a new constitutional agenda at the moment but instead focuses on rebuilding the country through the completion of major strategic projects, fighting poverty, improving social services, improving the business environment, enhancing democracy, administering good governance, protecting parallel and respecting human rights, so it cannot abandon those fundamental issues that carry the future of the Nation and begin to look backward in development for the personal interests of one person or a minority group.
.
The statement was made by the Secretary of the CCM National Executive Committee Ideology and Publicity Shaka Hamdu Shaka while talking to various elders of Tanga district in the city hall of the Tanga City Council.

"No citizen is saying that the government should let all that be done first and the new constitution does not exist. Demands for a new constitution are not a political agenda so politicians should stop using that agenda as a trump card to deceive the people that that is the answer to their challenges which is not true" said Shaka.

Shaka noted that the Government of President Samia is pursuing more fundamental priorities in the cross-cutting areas of access to quality health care, the provision of free and quality education in schools and colleges, clean and safe water services being strengthened in areas without such services, enhanced through a system of justice delivery, low interest and concessional lending, improved agriculture and ensuring access to crop markets in parallel with creating a friendly and enabling environment for traders and investors.
.
In addition, Shaka stressed that the Nation needs honest, patriotic leaders, who value our nation, who put the interests of the Nation first for the benefit of the people and not the dynamic politicians of propaganda seeking political support without building strong foundations.
 
Hao wananchi walio wengi bado hawajajitambua na wala kuuona umuhimu wa katiba mpya.

Ndomaana swala la katiba mpya limeonekana kuwa ni takwa la wanasiasa au kikundi cha watu.

Kiujumla watanzania bado tupo kwenye usingizi mzito ulioambatana na mvua.
Ndo maana kuna wakati kulikuwa na uhitaji wa ELIMU YA URAIA kwa wananchi hasa kufundishwa shuleni.

Wananchi wengi hawajui haki zao ni zipi kutoka kwa serikali na wajibu wao pia ni upi na kinyume chake dhidi ya serukali.
 
Yeyote aliyeko madarakani ameapa kuilinda na kutetea katiba, kama unasema katiba sio kipaumbele tujiulize tunaongozwa na nini.
 
Back
Top Bottom