Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Inawezekana visiwani hamhitaji katiba mpya. Ila Tanzania bara tunahitaji mno.
 
Kwan katiba mpya ni jukumu la CCM au serikali? Au anasemea katiba ya CCM?
 
Hawa jamaa sijui huwa wanatuonaje? Sijui hii nchi walishajimilikisha? Katiba sio takwa la Chama bali ni la wananchi sasa hiki Chama kinataka kutufanya sisi ni mafala wanaamua kusema au kufanya wakitakacho,huu ni uzandiki wa hali ya juu!
Hiyo hasira yako haina madhara. Nchi kama tanzania inatawaliwa haiongozwi. Simple and clear. Uongozi upo ulaya china na marekani
 
Kwan katiba mpya ni jukumu la ccm au serikali? Au anasemea katiba ya CCM?
Haya malalamiko yenu huwa ni kelele tu. Wananchi hamna power tena. Cha msingi muwe wapole tu muliwe
 
Sera ambazo hazina tija zinatokana na katiba ambayo ina mapungufu
Ifike point tukubali tu kwamba wananchi hatuna sauti tena. Na tunachofanya saa hivi ni kama mayowe anayopiga panya anapokua amebananishwa na mbwa. Huwa mayowe hayo hayana madhara
 
Huyu naye akili kwenye kibuyu, kwahiyo kama hakuna mwananchi anayesema hayo yeye ameyapata wapi hayo anayosema au anamjibu nani au ana mapepo ndiyo anajibizana nayo

Anahitaji maombezi
 
Kutulia ndio mpango mzima

Kanyaga twende mama Samia

Katiba sio kipaumbele
 
Huyu BWANA nafikili kipo anachokitafuta, KWA watanzania ila vyema akaelewa

Tz sio ya ccm ni yawananchi, inajengwa nchi gani isiokua na misingi iliosimama katika katiba bora

Tangu Uhuru nchi imejengwa na itaendelea kujengwa hakuna jipya that's kenya uchumi wao unapaa lakini pia Wanayo katiba yao nzuri tu, tumewazidi nini wakenya mpaka Sasa

Vyema pia akaelewa hatudai katiba mpya just kuangalia ubinfsi WETU bali KWA kizazi kichacho ,ieleweke generation yetu ya Sasa tutakufa ila tz itabaki na itaendelea kuwepo,

Leo mtu yeyote hasiweza ona umuhim wa katiba mpya ,hafai hata uongonzi wa nyumba kumi, analazimisha uzalendo ambao Hana,ni mbinafsi KWA kuangalia alipo ila sio kesho ya Taifa Hili , na Mungu hatoruhusu watu wa aina hii mpate amani ya moyo ,mwili na hakili , atawanyoosha , na imekua
 
CCM YAVUNJA UKIMYA KUHUSU KATIBA MPYA.

✓Yasema kwa sasa sio kipaumbele chake.

✓Yajielekeza katika kujenga nchi kwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuboresha huduma za kijamii, kuboresha mazingira ya biashara, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda sambamba na kuheshimu haki za binadamu.

Hivyo hakiwezi kuacha masuala hayo ya msingi yaliyobeba mustakabali wa Taifa na kuanza kurudi nyuma kimaendeleo kwa maslahi binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee mbalimbali wa wilaya ya Tanga mjini katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Tanga.

Amefahamisha kuwa Serikali ya Rais Samia inakimbizana na vipaumbele vya msingi zaidi katika maeneo mtambuka ya upatikanaji wa huduma bora za afya, utoaji wa elimu bure na bora mashuleni na vyuoni, huduma za maji safi na salama zikiimarishwa katika maeneo hasa yasiyo na huduma hiyo, kuimarishwa kwa mfumo wa utoaji haki, kutoa mikopo ya riba ndogo na masharti nafuu, kuboresha kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao sambamba na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji huku mkazo zaidi ukielekezwa katika kukomesha rushwa na ubadhirifu jambo ambalo litasaidia katika matumizi yenye tija ya utajiri wa nchi kupitia rasilimali zake.

"Hakuna mwananchi anayesema serikali iyaache yote hayo ishughulike kwanza na katiba mpya hayupo. Madai ya katiba mpya sio agenda ya kisiasa hivyo wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi kuwa hilo ndio jawabu la changamoto zao jambo ambalo sio kweli" alisema Shaka

Shaka alibainisha kuwa Taifa linahitaji viongozi waadilifu, wazalendo, wanaothamini utaifa wetu, wanaotanguliza na kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuwanufaisha wananchi sio wanasiasa mahiri wa propaganda za kutafuta ushawishi wa kutafuta kuungwa mkono kisiasa bila kujenga misingi madhubuti.

Kaziinaendelea.
 
Huyu BWANA nafikili kipo anachokitafuta, KWA watanzania ila vyema akaelewa

Tz sio ya ccm ni yawananchi, inajengwa nchi gani isiokua na misingi iliosimama katika katiba bora..
Mkuu hili swala la KATIBA naona wanasiasa wanashidwa kuelewa tu hakuna Rais ambae atakubali kujipunguzia mamlaka kwa kiasi kile alafu ufike wakati wa uchaguzi aanze kuishi kwa pressure.

Hayo Mambo yamewezekana nchi za wenzetu tu ambako uongozi ni credibility sio nafasi ya kuvuna Mali na utajiri Kama nchi zetu za kiafrika.

Tena naimani hata hao chadema wanalilia iyo KATIBA sio kwa sababu wanawapenda Sana wananchi wa nchi hii big No Ila kwa sababu wanaiona Ni fursa kwao .
 
Back
Top Bottom