Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Shaka Hamdu Shaka: CCM haina mpango wa kushughulika na Katiba Mpya, kipaumbele ni kujenga nchi

Kazi iendelee na kwa sasa kazi kubwa inafanyika ya kujenga misingi madhubuti ya utawala bora yenye misingi ya kuheshimu haki za binaadamu, lkn pia kujenga demokrasia.

Sio mbaya nimewaelewa CCM awamu ya 6 hawataki kukurupuka, nia ipo ila muda bado haujafika.
 
Haya matamshi mengine yalitakiwa yatolewe kwa tahadhari sana,yaani CCM inaona inamiliki watu ambao ni RAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO?Watu hawana matakwa yao juu ya nchi yao mpaka iamue CCM?,Hivi munatuonaje?
 
Marekani imeendelea baada ya miaka mingapi?
Aisee unatakiwa kuwa well informed kama unahoji maswali ambayo hata mtoto wa darasa la pili anaweza kujibu.

BTW American Independence ilikuwa tarehe 04, July, 1776 unaweza kuona ni miaka mingapi mpaka sasa.

Halafu kumbuka US was independent wakati tayari kuna maendeleo na UK na Spain na wengine wakiamua kuinvest in America including Latin America usifananishe na miaka 50 ambayo Nyerere aliachiwa nchi mbovu sana maana huku walikuwa hawajengi permanent ventures aliyejenga no mjerumani ambaye ndio alikuwa mkoloni kabla ya kunyang'anywa makoloni yake yote under the league of nations in 1929.

Just read the history utarelate na huu umasikini wetu ambao CCM ndio wamebaki kuwa wakoloni instead ya kutukomboa.
 
Marekani imeendelea baada ya miaka mingapi?
Dubai, Singapore, Malaysia na Thailand, ziliendelea baada ya muda gani?

Tanzania, Singapore, Malaysia, Thailand na Indonesia, zilikuwa na viwango sawa vya maendeleo mwaka 1961.

Kwa taarifa ya UNDP, Singapore ikibalia mahali ilipo, Tanzania ikiendelea na speed yake ya maendeleo iliyo nayo, itaichukua Tanzania miaka 250 kuifikia Singapore.

GDP per Capita
Singapore $65,000
Malaysia $11,000
Thailand $8,000
Indonesia $4,000
Tanzania $1,000

Dubai iliyapata maendeleo makubwa ndani ya miaka 15. Tanzania miaka zaidi ya 60 bado maskini.
 
Hao wananchi walio wengi bado hawajajitambua na wala kuuona umuhimu wa katiba mpya.

Ndomaana swala la katiba mpya limeonekana kuwa ni takwa la wanasiasa au kikundi cha watu.

Kiujumla watanzania bado tupo kwenye usingizi mzito ulioambatana na mvua.
Kwani wewe unafikiri Katiba hiyo Mpya ndiyo itaondoa matatizo yako? Fanyakazi mkuu, pambana na maisha yako.
 
Hiki chama Kisha poteza mwelekeo hakijui hata kina simamia Nini hakika wajinga wakipewa nguvu hujiona Bora sana
 
Mimi nadhani hatma ya nchi yetu imo mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama. Siku vyombo hivi vikijitambua kama walivyofanya Malawi, nchi itakuwa kwenye mikono salama.

Nasema hivyo kwa sababu vyombo hivi pamoja na kwamba viliapa kuilinda serikali iliyopo madarakani. Ni vyema vikalinda usalama wa wanaotii sheria tu wakiwemo watawala wenyewe.

Ni ukweli usiopingika kwamba bila tume huru ya uchaguzi,haki kwenye uchaguzi haiwezi kutendeka kamwe. Haiwezekani mtu awe mshindani na awe mwamzi yeye, alafu atende haki kwa kujinyima ushindi, labda asiwe mwanadamu wa kawaida, yaani asiwe na asili ya kibinadamu maana kwa kawaida mwanadamu ni mbinafsi.
 
Dubai, Singapore, Malaysia na Thailand, ziliendelea baada ya muda gani?

Tanzania, Singapore, Malaysia, Thailand na Indonesia, zilikuwa na viwango sawa vya maendeleo mwaka 1961.
Afrika ni bara la hovyo kabisa mkuu, wakati nchi nyingine ziko serious kwenye maendeleo viongozi wetu wako bize kuitisha mikutano ya kina mama
 
Rafiki yako Sabaya anaendeleaje pale Kisongo[emoji23][emoji23]What Goes Around Comes Around [emoji28][emoji28]
 
Chadema bwana,wao wanaamin katiba mpya itawapeleka ikulu.

Pole Sana ninyi chadema,binafsi siungi hoja ya kuwa na mjadala wa katiba mpya ,iliyopo idumu hata miaka elfu moja

..katiba mpya ili waingie ikulu?

..au katiba mbovu ya zamani ili wasitoke ikulu?

..au katiba mpya itakayotoa HAKI SAWA kwa wananchi wote?
 
Katiba ya Nchi sio jambo la msingi ? Eti wanajenga nchi CCM hata wapewe miaka 2000 hakuna watakachofanya zaidi ya ufisadi .
 
Mkuu hili swala la KATIBA naona wanasiasa wanashidwa kuelewa tu hakuna Rais ambae atakubali kujipunguzia mamlaka kwa kiasi kile alafu ufike wakati wa uchaguzi aanze kuishi kwa pressure .hayo Mambo yamewezekana nchi za wenzetu tu ambako uongozi ni credibility sio nafasi ya kuvuna Mali na utajiri Kama nchi zetu za kiafrika .Tena naimani hata hao chadema wanalilia iyo KATIBA sio kwa sababu wanawapenda Sana wananchi wa nchi hii big No Ila kwa sababu wanaiona Ni fursa kwao .
Mkuu katiba naiona inakuja kiroho, na hakuna wa kuzuia, Tusitegemee kuwa na Taifa imara,lenye kupiga atua bila kutofikilia nyenzo zingine za kulisaidia Taifa, moja ikiwa nikatiba bora never ,kiongonzi mwenye nia njema katiba ataipa kipaumbele
 
Na Mwandishi Wetu,
Kutoka Tanga Mjini.

~Yasema kwa sasa sio kipaumbele chake.

~Yajielekeza katika kujenga nchi kwanza

Chama Cha Mapinduzi kimesema hakina agenda ya katiba mpya kwa wakati huu badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuboresha huduma za kijamii, kuboresha mazingira ya biashara, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda sambamba na kuheshimu haki za binadamu.

Hivyo hakiwezi kuacha masuala hayo ya msingi yaliyobeba mustakabali wa Taifa na kuanza kurudi nyuma kimaendeleo kwa maslahi binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee mbalimbali wa wilaya ya Tanga mjini katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Tanga.

Amefahamisha kuwa serikali ya ya Rais Samia inakimbizana na vipaumbele vya msingi zaidi katika maeneo mtambuka ya upatikanaji wa huduma bora za afya, utoaji wa elimu bure na bora mashuleni na vyuoni, huduma za maji safi na salama zikiimarishwa katika maeneo hasa yasiyo na huduma hiyo, kuimarishwa kwa mfumo wa utoaji haki, kutoa mikopo ya riba ndogo na masharti nafuu, kuboresha kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao sambamba na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji huku mkazo zaidi ukielekezwa katika kukomesha rushwa na ubadhirifu jambo ambalo litasaidia katika matumizi yenye tija ya utajiri wa nchi kupitia rasilimali zake.

"Hakuna mwananchi anayesema serikali iyaache yote hayo ishughulike kwanza na katiba mpya hayupo. Madai ya katiba mpya sio agenda ya kisiasa hivyo wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi kuwa hilo ndio jawabu la changamoto zao jambo ambalo sio kweli" alisema Shaka

Shaka alibainisha kuwa Taifa linahitaji viongozi waadilifu, wazalendo, wanaothamini utaifa wetu, wanaotanguliza na kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuwanufaisha wananchi sio wanasiasa mahiri wa propaganda za kutafuta ushawishi wa kutafuta kuungwa mkono kisiasa bila kujenga misingi madhubuti ya taasisi zao za kisiasa zinazotumika kubeba agenda hizi za wananchi.

"Watu wasipotoshe, Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya uliendeshwa na ulifikia hatua ya Katiba inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo inasubiri kupigiwa kura ya maoni na wananchi pale ambapo serikali itaona inafaa kukamilisha mchakato wake hivyo upinzani uache hadithi za kusadikika. Huu ni wakati wa kujenga nchi kwanza kazi ambayo CCM inaifanya baada kuaminiwa na watanzania" Alibainisha Shaka

Hata hivyo katibu huyo wa itikadi na Uenezi Ndugu Shaka amekumbushia kuwa hata vyama vya MCP, KANU na UNIP viliondolewa madarakani kwa katiba ile ile na baadae MCT cha Malawi kikarudi tena madarakani kwa katiba ileile kutokana na uamuzi wa wapiga kura wala sio kwa katiba mpya au ya zamani kwani kinachoweka chama madarakani ni sera bora, utekelezaji madhubuti, na uwezo wa kuwaunganisha wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu kwa usawa kama ifanyavyo CCM.

"Hata ukiangalia hoja ya suala la tume huru ya uchanguzi nalo ni jambo la kikatiba ndio maana CCM inaendelea kushangaa upinzani wanavyozungumzia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kama ajenda mbili tofauti utadhani katiba ni jambo jingine na tume ni jambo jingine. Tume ya uchaguzi ipo kikatiba na haijawahi kubadilishwa, ni tume hiyo hiyo iliyowapa madiwani, wawakilishi na wabunge kwa zaidi ya miaka 20 tena hata wakati mwingine wakiongezeka kwa idadi ajabu tume hiyo hiyo wanataka iwe huru, sasa sijui ni uhuru upi wanautaka labda wanataka waiongoze wao japo bado watashindwa chaguzi maana hawataki kukubali wana vyama vya siasa dhaifu!" alisema Shaka.

#ChamaImara
#KaziIendelee
IMG-20210614-WA0087.jpg
IMG-20210614-WA0089.jpg
IMG-20210614-WA0088.jpg
 
Back
Top Bottom